TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 31,669
- 18,874
They don't have balls to do thatShujaaa halilii bunduki. Wacha wampigie kur ya kutokuwa na imani tuone
They don't have balls to do thatShujaaa halilii bunduki. Wacha wampigie kur ya kutokuwa na imani tuone
Wana jamvi
Hapa Dodoma kimenuka. JK kafika kutoka MWZ ili kuonana na wabunge. Wabunge wa CCM wakaitwa na kuingizwa ukumbini ili kumsubiri. Awali Katibu wao Jenester Mhagama alitoa tangazo kupitia Naibu Spika kuwa wabunge wote waache simu zao wazi ili kuitwa wakihitajika.
JK aliendelea kupata briefings na kuambiwa hali ni mbaya. Akashauriwa afanye reshuffle upesi ili kupoza moto. Kama kawaida akawa mbishi, lakini pia akasita kuingia ukumbini kuonana na wabunge. Mwishowe wabunge wameambiwa waende kulala kwa sababu JK bado ana kikao na watendaji.
Kuna hatari kesho ya reshufle. Mawaziri wote matumbo moto hususan Afya, Nishati, Fedha na Ujenzi. Vijana wa TISS wamemweleza kuwa baraza zima ni kama haliko kazini isipokuwa wizara moja tu- Ya Pombe Magufuli.
Vijana wa TISS wameingia kazini kwa kasi sana usiku huu kujaribu kubadili upepo miongoni mwa wabunge.
Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Dodoma mjengoni.
hao wabunge wa ccm ni wanafiki (ukimtoa january makamba) wangeni waliobaki hawana uwezo wa kupingana na serikali.
kuwa mbunge wa CCM unafungwa speed gavana, hupewi nafasi ya kupumua mimi nisingeweza wakuu. bora nikalime matikiti rufiji ijulikane moja.
wabunge wa CCM, sijui wapo mjengoni kwa maslahi ya nani? Badala ya kusimamia mambo ya msingi wao wameng'angana na posho, hivi watakua na ujasiri tena wa kurudi majimboni kuomba kura kwa wapiga kura wao???
Mimi nadhani hii ni nafasi pengine ya mwisho kwa JK kurudisha hadhi yake na ya CCM mbele ya umma. Anahitaji kufanya mabadiliko makubwa na kuondoa mawaziri legelege wote; pia mwanasheria mkuu wa sasa hatoshi, huyu hafai katika mchakato wa kupata katiba mpya. Pia ni muhimu kwa rais kubadili mfumo wa serikali, hasa sekta ya elimu na afya. Pia apunguze ukubwa wa baraza la mawaziri kwa kufuta wizara nyingine au kuziunganisha ili iwe ishara kwa umma ya kuanza kubana matumizi tunapoelekea bajeti mpya mwezi juni. Na katika hotuba yake kuunda baraza jipya, awe mkali na awe tofauti kabisa, na ashike uzi huo huo kwa kipindi chake kilichobakia. Akiachia nafasi hii imponyoke, atakuwa na shughuli nzito sana ya kukipa CCM uhalali mbele ya umma, na pia mawaziri wengi wataendelea kumchukulia kama mshijaki. Hili litakuwa janga kubwa kwake hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM, Novemba mwaka huu.
ili kulinda heshima hata jk anapaswa kukaa pembeni........mtu mbishi sana huyu!!!!