Jk-msijali Kuitwa Mafisadi!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
26,023
24,660
JK aliwaambia viongozi wasijali kuitwa mafisadi wakati wa kutolewa tenda pale wanapotoa tenda na kuwanyima wengine.

Swali hapa ni je Mh Rais anaamini kuwa kuna ufisadi?

Na pili..je ana uhakika kuwa hizo tenda huwa zinatolewa bila mazingira ya rushwa ama upendeleo?

Ama anasubiri kuunda kamati nyingine na kuikalia ripoti?

Pamoja na hayo..anasema sisi ni masikini huku akiwa hafuatilii issue ambazo zinatufanya sisi kuwa masikini licha ya kwamba wengi wetu sasa tumefunguka macho na kugundua kuwa sisi ni matajiri?
 
Kwa mwenendo wa kusuasua kuhusu kuwashughulikia mafisadi mimi nadhani JK na mafisadi lao moja tu! Sisi tuendeleze mapambano kwa sababu nchi hii ni yetu na wala si ya JK! Kama ni ya JK basi ni kwa sasa lakini si milele!
 
Mkuu hayo maneno ameyasema kweli kwa kufikiria?

Hivi waliomchagua anafikiri wanapenda UFISADI?

Hivi kumbe hachukii neno UFISADI? Basi kumbe tuna kazi au alimaanisha ATCL, nini?
 
Mh Rais haamini kama there's anything as such as "UFISADI"
Na hapo ndio tumekwama na ndio kwenye problem!
He simply think Watanzania wanaota!
Hayuko upande wetu period!
 
Bro, nakubaliana na wewe 100% JK hayuko upande wetu kabisa coz is one of them in one way or another!!! JK is not clean trust me its just a matter of time nature will reveal his evils!! hawezi akakosa kushiriki kati ya mascandal yote haya yaliyo hewani, na kianchonifanya niseme hivyo ni yeye kutojishughulisha kabisa na hizi shutuma za ufisadi; kama kweli anauchungu na nchi anayooiongoza amefanya nini so far kuhakikisha BALALI anakuja kujibu tuhuma za mabilioni aliyoiba!!!!! its been a while since the truth came out!!! what is he doing about it???? kingine mambo ya LOWASSA yamefikia wapi? what is going on? yeye kujiuzulu uwaziri mkuu sio malipo ya pesa alizoiba lazima wajibishwe!!!! na CHENGE je, kwani tulikuwa tunasubiri Uingereza ituambia Chenge mwwizi, we could use our own common sense na ushahidi uliotuzunguka to come up with that conclusion ila Rais anayajua haya yote na yuko kimya kama KAFA, kisa?? He is involved in all these scandals in one way, trust me na kama anabisha basi achukue hatua tuone hapo ndio tutamwomba msamaha kwa kumsingizia not otherwise!!!!!:mad:

Mh Rais haamini kama there's anything like "UFISADI"
Na hapo ndio tumekwama na ndio kwenye problem!
He simply think Watanzania wanaota!
Hayuko upande wetu period!
 
Kauli ya mh Rais the same day akisema kuwa sisi ni masikini huku akishauri gharama zisipewe kipaumbele bila kujali kama upandishaji gharama huo utamnufaisha mkandarasi,fisadi ama utainufaisha kazi/tenda/walengwa na kuona kama gharama zinaendana na quality ya kazi pamoja na mazingira ya utoaji wa tenda hizo!
Ufujaji ufujaji ufujaji...sasa hii ni signal ya kisirisiri kwa mafisadi kuwa waendelee kula na hamna noma?
Tena anawaambia wapandishe dau kwani chapaa ipo ya kumwaga!?(aliposema wasijali gharama!)
And then he turns around and say it loud!
Tanzania ni masikini?!
Doesn't he get it that ufisadi is serious like AIDS?
 
unajuwa wakati ule wa mkutano mkuu kule Kizota, walialikwa watangazaji kutoka (VOK)Kenya,
Walisema hawa Vingunge wa chama cha mapinduzi wanapanda kwenye viriri na kuonekana wamejiandaa vizuri kwa majibu, kwao ilikuwa Kingunge ni cheo kwenye chama, ufisadi ni moja kati ya CV kwasasa
 
JK aliwaambia viongozi wasijali kuitwa mafisadi wakati wa kutolewa tenda pale wanapotoa tenda na kuwanyima wengine.
Swali hapa ni je Mh Rais anaamini kuwa kuna ufisadi?
Na pili..je ana uhakika kuwa hizo tenda huwa zinatolewa bila mazingira ya rushwa ama upendeleo? Ama anasubiri kuunda kamati nyingine na kuikalia ripoti?
Pamoja na hayo..anasema sisi ni masikini huku akiwa hafuatilii issue ambazo zinatufanya sisi kuwa masikini licha ya kwamba wengi wetu sasa tumefunguka macho na kugundua kuwa sisi ni matajiri?

kumbe jk ni 0%
 
haa haaaa kuspin ni bomba tu

hebu isomeni ile habari nzima msikate maneno muyapendayo tu.

alichosema ni wazi kuwa katika kuchukua maamuzi waangalie maslahi ya taifa na wasiogope kuchukua maamuzi yenye kufaa kwa kuwa wataitwa mafisadi na hasa kuhakikisha wanampa tenda anaeweza kufanya kazi na sio kuangalia gharama ndogo alizoleta ili apewe tenda.

na hili limetokana na huko mwanzo kutoa tenda kwa wanaokuja na mahesabu hafifu na matokeo yake hutupa kitu kibovu au hawamalizi kandarasi na kuitia serikali gharama zaidi

ila kuspin kunaruhusiwa, masikitiko kwa wenye kurukia mkuki kwa mbele
 
haa haaaa kuspin ni bomba tu

(1)hebu isomeni ile habari nzima msikate maneno muyapendayo tu.

(2)alichosema ni wazi kuwa katika kuchukua maamuzi waangalie maslahi ya taifa na wasiogope kuchukua maamuzi yenye kufaa kwa kuwa wataitwa mafisadi na hasa kuhakikisha wanampa tenda anaeweza kufanya kazi na sio kuangalia gharama ndogo alizoleta ili apewe tenda.

(3)na hili limetokana na huko mwanzo kutoa tenda kwa wanaokuja na mahesabu hafifu na matokeo yake hutupa kitu kibovu au hawamalizi kandarasi na kuitia serikali gharama zaidi

ila kuspin kunaruhusiwa, masikitiko kwa wenye kurukia mkuki kwa mbele

Kama kawaida nime highlight na kuweka namba..na majibu yenye reference ni kama yafuatayo:
1)Tunajua habari nzima ni related na topic hii kwasababu alikuwa akizungumzia miundo mbinu ambayo ni crucial kwenye maendeleo ya nchi yetu!

2)Tayari wameshaitwa mafisadi na hajachukua hatua yoyote ile!
Tatizo hapa ni kuwa out of touch!

Kila mtu anajua tatizo sio wakandarasi bali ni wanaotoa tender hizo(ambao wengi wao ndio hao mafisadi!)

Rais pia anaonekana kutukejeli wananchi kwa kudai kuwa wasiogope kuitwa mafisadi!

Ikiwa ina maana kuwa yeye haoni kuwa kuna ufisadi bali ni kuwa wanatakiwa waongezewe zaidi ili hata wakila na nyingine zibaki ziende kwenye shughuli!?

Kabla ya kuwaongezea fedha ameshajua zile zilizokuwa zikitolewa zilitumika vipi?

je anajua kuwa kama ni rushwa ilitumika kutoa tenda and so therefore kuna mahesabu mengine ya nje ya vitabu halali?

3)Hili la tatu ni kama nimeshakujibu!
Wanatoa tenda kwa mahesabu hafifu kwasababu nyingine washaweka mfukoni so they have to come with a convincing and justifiable reasons ie gharama ndogo!

Kwani hilo ni siri Mtu wa Pwani?Where is the spin?
 
Wakubwa ni kwamba tulishalikoroga sasa hivi tunalinywa tu! Swali ni je tutathubutu kulimwaga, au tutavumilia tu tulinywe hadi liishe japo chungu? Na tutakapomaliza kulinywa, hali yetu itakuwaje?
 
Wakubwa ni kwamba tulishalikoroga sasa hivi tunalinywa tu! Swali ni je tutathubutu kulimwaga, au tutavumilia tu tulinywe hadi liishe japo chungu? Na tutakapomaliza kulinywa, hali yetu itakuwaje?
Heri nusu shari kuliko shari kamili!
2010 is coming by!
Wananchi waamke!
Asasi zote za kijamii,kidini etc ziwaelimishe wananchi kuhusu ufisadi!
Kampeni pia ianzishwe kama ile ya ukimwi ama vita dhidi ya ugaidi!
Kuna ugaidi kwa mtanzania zaidi ya ufisadi?
 
jmushi1..Jk anajua kinachoendelea na hao mafisadi yeye kama baba mwenye nyumba kila siku akiweka vijisenti vyake vinatoweka lazima atashuku miongoni mwa watoto wake ndio wanampiga bao... Mi nahisi huyu jamaa pamoja na kucheka cheka kwake huenda ana % zake zinakwenda mahali so hataki kuwatosa hawa jamaa wanaoingia FRONT na kujilipua yeye ametulia tu.

hata hizoo tenda sio siri wala nini hapo hakuna suala la gharama nafuu bali hata hao wakandarasi wengi wameshajua tabia za watendaji wetu kwa hiyo wanapo-bid wanaweka na fungu la contigency la kuwatia pilipili za macho jamaa then ngoma inalia..tatizo uroho wao hauna aibu tena wanakula kama hata wasivyoliwa eti na baba mwenye nyumba yuko kimya...Si bure
 
haa haaaa kuspin ni bomba tu

hebu isomeni ile habari nzima msikate maneno muyapendayo tu.

alichosema ni wazi kuwa katika kuchukua maamuzi waangalie maslahi ya taifa na wasiogope kuchukua maamuzi yenye kufaa kwa kuwa wataitwa mafisadi na hasa kuhakikisha wanampa tenda anaeweza kufanya kazi na sio kuangalia gharama ndogo alizoleta ili apewe tenda.

na hili limetokana na huko mwanzo kutoa tenda kwa wanaokuja na mahesabu hafifu na matokeo yake hutupa kitu kibovu au hawamalizi kandarasi na kuitia serikali gharama zaidi

ila kuspin kunaruhusiwa, masikitiko kwa wenye kurukia mkuki kwa mbele

Nasi tunataka waangalie masilahi ya taifa lakini tatizo limejitokeza ktk matumizi ya neno 'Maslahi ya Taifa' viongozi wamelitumia hili neno kwa maslahi yao binafsi. Mimi sasa nawaza kuwa neno hili limekuwa polluted sasa naomba tulibadilishe tuseme kwa 'Masilahi ya Wananchi' Hawa viongozi wakitoa tenda kwa maslahi ya wananchi kuna mtu atakuja na kusema kiongozi yule ni fisadi? hakuna hata kidogo. Mh Rais hapa anazidi kutukoroga tu badala ya kuwaambia wakati wanatoa tenda waepuke rushwa na kuitwa mafisadi yeye anasema wasiogope kuitwa mafisadi? He must not be seious at all.
 
alichosema ni wazi kuwa katika kuchukua maamuzi waangalie maslahi ya taifa na wasiogope kuchukua maamuzi yenye kufaa kwa kuwa wataitwa mafisadi na hasa kuhakikisha wanampa tenda anaeweza kufanya kazi na sio kuangalia gharama ndogo alizoleta ili apewe tenda.

Mtu wa Pwani,
sasa twende hatua kwa hatua kwenye maneno yako (ukimwakilisha JK)

Hivi ni wapi mtu aliitwa FISADI kwa kufanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa?? JK atuambie! labda bado kwake RICHMOND ni mradi wenye manufaa, kwa hiyo wale wote walioshiriki anaona wameonewa!!!! Je EPA, TICTS, Kiwira, ... safari ya mahujaji (serikali ilipoteza bilioni 5, bila sababu yoyote ya msingi!, au kwasababu aliyetenda kosa ni Mustapha na rafikie David!!!!!)

JK atuambie ni nani aliyefanya maamuzi ya kufaa taifa na akashutumiwa ni FISADI!!!
 
JK hana reputation ya kuchagua maneno yake kwa busara, atachaguaje maneno kwa busara wakati hana busara? Come to think of it kusema hana busara nampendelea, kwa sababu inawezekana mtu akawa na akili akakosa busara, JK hana hata akili.

Nilichosoma kwatika kauli za JK kuanzia kuchaguliwa mpaka sasa, ni kwamba JK ana mentality ya "them against us".Na hii ndiyo inayonifanya niamni kuwa JK hana akili na pengine ana wazimu wa aina fulani, ujue nyumbani uchunguzi wa kisaikolojia bado uko nyuma na magonjwa mengi pamoja na conditions za akili bado haziwi diagnosed vizuri.

Huyu JK anaona kuwa akiwachagua watu basi uchaguzi wake ni vindication tosha, hata watu wapige kelele vipi hataki ku-budge.Ingekuwa vizuri kama angefikiri hivyo wakati hiyo ni facts, it is not.Kwa nini nasema hivi? JK teuzi zake zimekaa kimtandao tandao, akishateua wanamtandao wake anataka kuwapa backing itakayowapa clout na confidence ya kufanya wanachotaka.Which is a good thing, as a matter of fact hii ndiyo collective responsibility, lakini tatizo linakuwa objectives, commitments na abilities zao zinakuwa tofauti na what is required for the good of the country.

Kikwete anakuwaga na vi-subliminal messages ambavyo mpaka mtu uwe unajua ku "read between the lines" ndiyo utaelewa.Kauli kama hiyo ya kusema "msiogope kuitwa mafisadi" inasend message kwamba "I am not with the war against ufisadi, I am protecting mafisadi by camouflaging my protection as a brave and gallant stance support for my team of very accountable people who in the process of discharging their duties may fall under suspiciopn of ufisadi"

Kikwete alishawaambia Watanzania wa nje kuwa "hawawezi kuchangia serikalini kifedha moja kwa moja" kwa sababu "kwanza mna hela gani" na pia "mtawaletea viongozi lawama tu", the epitomy of a "us against them" mentality, badala ya rais kufanya kazi na raia wake ili kujenga rapport, yeye ana wa alienate.

Ndiyo maana nasema Kikwete siyo tu hama akili na busara, bali huenda akawa na aina fulani ya kichaa na anahitaji kwenda kwa Professor Kilonzo pale Muhimbili.Kwa sababu rais mwenye akili zake timamu never mind busara, in this time when ufisadi is the buzzword, hawezi kuja so openly against the anti-ufisadi movement, which is basically what he is doing in a roundabout way.

Rahisi tunaye!

Ananifanya nitake kusema "Billions of blue blistering barnacles" with rage kama Capt. Adolph of Tintin fame
 
Hapo umenena mkuu Pundit!
Ni mawazo na fikra nzito ulizonazo!
Nlikuwa pia nikifikiri kuanzisha thread yenye kutoa kipa umbele kwenye somo la saikolojia kwenye mitaala yetu kwani litawasaidia sana wananchi!
 
Psychology is the scientific study of behavior and mental processes! Therefore...
This will help wananchi to learn inside's our president's unpredictable behaviors and to get inside his mind and to undestand his super ego!

Both of these stuff can be learned and this will help build a more prosperous nation!
Kumbuka ni saikolojia inayotufahamisha kuwa njaa ni hitaji la kisaikolojia kama unaelewa Maslow Hierachy social needs before self actualization!
 
JK aliwaambia viongozi wasijali kuitwa mafisadi wakati wa kutolewa tenda pale wanapotoa tenda na kuwanyima wengine.
Swali hapa ni je Mh Rais anaamini kuwa kuna ufisadi?
Na pili..je ana uhakika kuwa hizo tenda huwa zinatolewa bila mazingira ya rushwa ama upendeleo? Ama anasubiri kuunda kamati nyingine na kuikalia ripoti?
Pamoja na hayo..anasema sisi ni masikini huku akiwa hafuatilii issue ambazo zinatufanya sisi kuwa masikini licha ya kwamba wengi wetu sasa tumefunguka macho na kugundua kuwa sisi ni matajiri?

Kwa heshima na taadhima naomba link ya ushahidi wa maneno ya JK .Ni mazito na yana maana pana na kuwa na nzito .Naomba link plizi .
 
Kwa heshima na taadhima naomba link ya ushahidi wa maneno ya JK .Ni mazito na yana maana pana na kuwa na nzito .Naomba link plizi .

Ngoma hii hapa Mh Lunyungu! Kazi kwako!
Wakandarasi wababaishaji sitaki -Kikwete

2008-05-04 10:45:16
Na Lucy Lyatuu, Singida

Rais Jakaya Kikwete `ameicharukia` Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara nchini TANROADS kutowapa kazi wakandarasi wababaishaji, pia kutowalipa wanaojenga barabara chini ya viwango.

``Wakandarasi wababaishaji wasipewe kazi, wanatufikisha pabaya,`` alisema.

Aidha, aliwataka wizara ya ujenzi wanapotoa tenda wamchague yule aliyetoa hesabu kubwa na sio kuangalia mwenye hesabu ndogo kwani wao pia ukubwa wa kazi wanaijua.

``Hakuna sababu wizara, TANROADS kumchagua mtu mwenye hesabu ndogo, mnapotangaza tenda lazima kuangalia kama kazi ataiweza, ingawa wale watakaokosa watasema mnajali mafisadi,... hayo msiyajali!,`` alishauri.

Aidha, amesema yapo makampuni kadhaa hapa nchini ambayo kazi yao ni kudanganya pindi wanapokuwa wamepewa tenda za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati akizindua barabara ya Isuna hadi Manyoni yenye urefu wa kilomita 55 baada ya mkandarasi aliyepewa kazi ya kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kushindwa kazi kwa visingizio.

Rais Kikwete yuko mkoani humu kwa ziara ya siku sita kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka 2005.

Rais Kikwete alisema awali barabara hiyo ya Isuna-Manyoni, ilikuwa ikijengwa na mkandarasi kutoka China ambaye alishindwa kukamilisha kazi kama ilivyotakiwa.

Alisema kilichotokea hapo iwe ni fundisho na kwamba tatizo la namna hiyo lisijitokeze tena.

Aidha Rais Kikwete alibainisha kuwa kupewa tenda kwa mkandarasi mwenye hesabu ndogo ndiko kunakosababisha matatizo ikiwa ni pamoja na miradi kutokamilika kwa wakati uliotakiwa.

Alisema wakiendelea na utaratibu huo wa kuangalia hesabu ndogo watakwama wakati nchi bado ni maskini.

``Ninaomba sana, bure ni ghali sana, kwani angalia sasa tunaingia gharama nyingine tena kubwa zaidi kuliko zile za awali,`` alisema.

Aliongeza kuwa mzabuni atakayekiuka utaratibu unaotakiwa wanapaswa kumuita na kumuuliza ili wasimamie katika ukweli na haki na sio kuwachanganya.

Kuhusu makampuni yanayodanganya alisema hapa nchini yapo kadhaa na kazi yao ndio hiyo halafu badaye huhitaji majadiliano.

``Simamieni wataalamu mlio nao, makampuni yawe yanasema ukweli kuepusha hasara katika nchi,`` alisema.

``Nchi hii ni maskini, ujenzi huu unagharamiwa na fedha za wananchi, epukeni kuingia gharama mara mbili, kwani wanaofanya hivyo wanakuwa wanyonya damu,`` alisema.

Pia aliwataka kukasirika na kuwachukulia hatua makampuni yanayokiuka utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwaambia kwa herini (byebye) wakatafute tenda nyingine nje ya nchi.

Rais aliongeza kuwa mhandisi mshauri naye hatakiwi kulipwa malipo yake endapo ujenzi hautakuwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa kwani wasipofanya hivyo Tanzania itakuwa shamba la wajinga.

Lazima Watanzania waone uchungu na kutekeleza miradi ya wananchi katika kiwango kinachotakiwa, alisisitiza.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Bw. Omar Chambo alisema barabara hiyo itagharimu kiasi cha Sh. bilioni 30.43 na ujenzi wake ulisainiwa Desemba 11, mwaka 2007.

Alisema barabara hiyo ilisainiwa kati ya TANROADS na Kampuni ya China Geo Engineering kutoka nchini China na kwamba sehemu ya barabara hiyo inatarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2010.

Alisema mradi huo unasimamiwa na mhandisi mshauri Black &Veatch kutoka Afrika Kusini akishirikiana na Kampuni ya Mak Consult ya Tanzania kwa gharama ya Sh. milioni 857.23.
  • SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom