Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,550
Kwa Maslahi ya Taifa Nipashe ya Jumapili ya 15 January 2023 ni swali
"hivi kweli sisi Tanzania tuna wanasheria wa ukweli au tuna wasomi tuu wa sheria, waliosomea sheria na kuhitimu?. Kama ni kweli tuna wanasheria, jee wanasheria waliopo ni wapo kweli au ni wapo wapo tuu?!. Kama kweli Tanzania tuna wanasheria, wa ukweli na sio tuu wasomi wa sheria, na ni kweli wapo kiukweli, ilikuwaje kuwaje, madudu makubwa hivi ya ajabu ya kisheria, yakafanyika ndani ya nchi yetu kuanzia kwenye serikali yetu, kwenye Bunge letu na kwenye Mahakama yetu?, yaliwezaje kufanyika vwakati tuna wanasheria wa ukweli?!, tena wengine ni manguli na wabobezi na wabobevu?!, huo unguli wao ubobezi na ubobevu ni kwenye nini?!
Screen Shot 2023-01-15 at 3.14.19 PM.png
Screen Shot 2023-01-15 at 3.14.42 PM.png

  1. Kwa Maslahi ya Taifa, leo, inawageukia kundi la watu muhimu sana katika jamii yetu, hili ni la Wanasheria, kila kitu kinachofanyika ndani ya nchi, lazima kifanyike kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni hivyo baada ya Mungu aliyekuumba, na wazazi wako waliokuleta duniani, wanasheria ni watu wa 5 kwa umuhimu baada ya madaktari na waalimu.
  2. Na kwa vile kwa Tanzania, ili mtu uitwe mwanasheria, ni lazima uwe msomi wa kiwango cha shahada ya Chuo Kikuu na kuhitimu shahada ya sheria, LL.B, kisha uende kusoma shule ya sheria Law School of Tanzania, ambapo muziki wake sii wa kawaida!, hivyo wanasheria wanaitana "the learned brothers and sisters", yaani "wakili msomi".
  3. Huku wanasheria kuitana wasomi, ukijumlisha na mavazi yao kikazi ni suti nyeusi na shati jeupe, ukijumlisha na remnants za colonial mentality kwenye kuvaa majoho, basi kuna wanasheria wanajisikia sana hadi kupindukia, kujisikia ni wasomi saana!, kumbe in reality baadhi yao hawana lolote, sii lolote, sii chochote, kiasi cha kujiuliza ilikuwaje, mambo ya ajabu kama haya, yakafanyika huku watu muhimu sana hawa wapo?!.
  4. Kazi kuu ya sheria ni kuhakikisha mambo yote yanatendeka kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni na kufanyika kwa haki, hivyo the bottom line kuhusu umuhimu wa sheria na umuhimu wa wanasheria ni katika kutenda haki!. Jee wanasheria walio achia haya yakatendeka kwa Watanzania, wamewatendea haki Watanzania?.
  5. Kwa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndicho chuo kikuu cha kwanza nchini, na shahada ya kwanza ya chuo kikuu kutolewa nchini ni shahada ya sheria!, hivyo wasomi wa sheria, ndio wasomi wa kwanza kabisa na wa mwanzo Tanzania!. Tena kwenye sheria, UDSM ndicho chuo kikuu cha kwanza kwa nchi za Afrika Masharaki kutoa shahada ya sheria, hivyo majaji wote na wanasheria karibu wote wa zamani wa Tanzania, Kenya na Uganda, walisomea Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!.
  6. Hivyo sisi Tanzania tunajinasibu kuwa tuna wanasheria manguli na wabobezi wa kitaifa na kimataifa!, wenye astashahada, shahada, shahada ya uzamili hadi shahada za uzamivu za kutosha ambapo tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, kitu cha ajabu ni kuna madudu fulani ya kiajabu ajabu sana ya kisheria, yamefanyika kwenye sheria zetu!, kwa kutungwa kwa sheria batili zinazokwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977!. Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatoa uamuzi kuwa hayo ni "madudu" ( neno madudu ni langu sio la mahakama), na madudu hayo yakachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Swali ninalojiuliza kwenye makala hii, ni ilikuwaje kuwaje haya madudu yakafanyika na wakati yakifanyika, hawa ndugu zetu wanasheria, manguli, wabobezi na wabobevu walikuwepo!, jee walikuwa wapi?!, hivyo kuuliza "Jee sisi Tanzania, tuna wanasheria kweli?! ni swali valid!.
  7. Sasa mpaka hapa ninapoandika, kuna moja ya haki kuu ya msingi ya kiraia ya Watanzania, iliyotolewa na katiba yetu, kisha ikaja kuporwa na sheria batili, na hata baada ya sheria hiyo batili kubatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kuwa ni batili kwasababu inakwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977, ubatili huo ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.
  8. Ubatili huu, uliofanywa na serikali yetu, uliweza vipi kufanyika wakati tuna wanasheria serikalini wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu ni mwanasheria mbobezi na mbobevu?, na kwamfumo wa serikali yetu, Waziri wa sheria ni mwanasheria mbobezi na mbobevu!, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria ni mwanasheria mbobezi mbobevu, ubatili huu ulipate serikalini hadi ukaingizwa Bungeni?.
  9. Bungeni nako kuna wanasheria wabobezi, wabobevu akiwemo Mwanasheria Mkuu wa serikali, ubatili huu ulipitaje?.
  10. Na hata baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa uamuzi wa kutamka sheria hiyo ni batili, na kilichofanyika ni ubatili, ikawaje Mahakama hiyo hiyo, baada ya kuutamka ubatili huo, badala ya kuufuta ubatili ule there and then, bado ukairuhusu serikali kukata rufaa kuutetea ubatili?!. Hata baada ya serikali yetu kuutetea ubatili huo, bado Mahakama Kuu makini ya Tanzania, ikasimamia haki kuwa huo ni ubatili!, hivyo serikali ikashindwa, ikakata rufaa ikashindwa!, na baada ya kushindwa marambili ndipo serikali yetu ikafanya maajabu ya mwaka!, kwa kuuchukua ubatili huo, na kulitumia Bunge letu, kufanya mabadiliko batili ya katiba kwa hati ya dharura!, na kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba ya JMT!. Haya yote yakifanyika, tuna wanasheria wapo, wanashiriki na wengine wanaangalia tuu!, hivyo ninapouliza hivi Tanzania tuna wanasheria kweli?, huku ni kuwaonea wanasheria?.
  11. Hizi makala za haki za kikatiba zilizoporwa, zinaendelea kukujia mfululizo kwenye "Kwa Maslahi ya Taifa", ili kutetea haki za msingi za kikatiba za Watanzania ambazo zimeporwa na serikali yetu!, Bunge letu na Mahakama yetu!. Kama haki iliyotolewa na katiba ikaja kuporwa kwa mihimili hii yote mitatu, to collude, wananchi tuende wapi kulila haki zetu?.
  12. Uporaji huo kwanza tulianza kwa serikali yetu, yenye wanasheria lukuki, ikaandaa muswada wa sheria batili!, kisha serikali ikalitumia Bunge letu, lenye wanasheria wabobezi wabobevu kuitunga hiyo sheria batili!, Mahakama Kuu yetu angalau ikawatendea haki Watanzania, ikatamka wazi sheria hiyo ni batili!.
  13. Baada ya sheria hiyo kutamkwa ni batili, serikali ilipaswa kuifuta sheria hiyo, lakini serikali yetu ya wakati huo ilivyo ya ajabu!, badala ya kuifuta sheria hiyo batili!, yenyewe ndio kwanza ikapeleka Bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba, kwa hati ya dharura, ambayo nayo yalifanywa kiubatili! na sheria hiyo batili, ikaingizwa kwenye katiba kiubatili!.
  14. Kitendo cha kuingiza kwa ubatili kifungu batili ndani ya katiba ni kuinajisi katiba yetu!. Hivyo katiba yetu ina vifungu batili!.
  15. Wakati yote haya yakifanyika, yalifanyika huku tuna wanasheria manguli wabobezi na wabobevu Serikalini, Bungeni na Mahakamani!. Kama haya yote yalifanyika na washeria wapo!, swali ni hivi kweli Tanzania, tuna wanasheria wa aina gani?!.
  16. Miongoni mwa mabadiliko makubwa ya sheria tutakayo muomba Rais Mama Samia, ayafanye ni kuipa meno Mahakama!, Mahakama Kuu ya JMT, ikiisha toa uamuzi wa kuitangaza sheria fulani ni batili kwasababu imekwenda kinyume cha katiba, tangu baada ya uamuzi huo, hiyo sheria inakuwa imebatilishwa! kwa kuwa ni batili ab initio from there and then!.
  17. Nchi yetu inaendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kwa kutumia mihimili mitatu ya katiba, ya Serikali, Bunge na Mahakama. Kwenye medani za sheria, kazi ya Bunge ni kutunga sheria, kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria na kazi ya serikali ni kutekeleza sheria.
  18. Mihimili hii kila mmoja una nguvu na mamlaka yake inayojitegemea, haipaswi kuingiliana, kwa kiingereza inaitwa “ the doctrine of separation of powers”, yaani Serikali itayaheshimu maamuzi ya Bunge na Mahakama na kuto yaingilia, Bunge litayaheshimu maamuzi ya serikali na mahakama na haita yaingilia, na mahakama itayaheshimu maamuzi ya Bunge na serikali, haita yaingilia.
  19. Kwa vile vyombo hivi vinaongozwa na watu ambao ni binadamu na wanaweza kufanya makosa, mihimili hii mitatu, ikapewa kazi ya kila mhimili kuwa ni mlinzi na msimamizi wa mhimili mwingine, usikiuke mamlaka yake. Kazi hii ya ulinzi na usimamizi wa mihimili inatumia kanuni inayoitwa kwa Kiingereza “the doctrine of separation of powers, checks and balance", Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth!
  20. Serikali inalisimamia Bunge na Mahakama kwa kuteua watendaji wakuu na kulipa fedha za uendeshaji. Bunge linaisimamia serikali kwa kuitungia sheria, kuipitishia bajeti na kuisimamia serikali na mahakama ya kuitungia sheria. Mahakama inalisimamia Bunge na serikali na kuzifuta sheria mbovu zitakazotungwa na Bunge na kutoa amri ambazo serikali ni lazima izitekeleze.
  21. Serikali ikivuka mpaka wa mamlaka yake, mfano mkuu wa serikali, akikiuka katiba, kama ilivyofanyika kwenye kuzuia mikutano ya siasa, Bunge lilipaswa kuingilia na kumuondoa raisi madarakani kwa kutumia Ibara ya 56. Au Mahakama to act on "suo moto" on its own volition kuipinga ile amri batili ya rais kwa kuiondoa na lazima serikali itekeleze. Hivyo serikali inasimamiwa na kulindwa na Bunge na Mahakama, Bunge linasimamiwa na serikali na mahakama, na mahakama inasimamiwa na Bunge na serikali.
  22. Katiba ya JMT ina misingi mikuu 4 ya uhuru, haki, udugu na amani. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
  23. Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  24. Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
  25. Katiba hii imetoa haki mbalimbali kwa Watanzania, haki kuu ni uhuru na haki!. Katiba imeeleza wazi kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, hii maana yake Bunge linapaswa kuwa na wajumbe waliochaguliwa na watu ambao ndio wawakilishi wa wananchi!, katiba haukusema vyama vya siasa, ndio vitawachagulia wananchi wajumbe wa kukuwakilisha!. Ni kina nani waliokuja kuamua ili mtu uchaguliwe kiongozi ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa?!.
  26. Katiba pia imetoa maelekezo mahusus kwenye mhimili wa Mahakama , Katiba inatamka Mahakama lazima ziwe huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, swali lile la wakati haki za msingi za Watanzania zilizotolewa na katiba, ziliponyofolewa huku mahakama imepewa jukumu la kuhakikisha haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, ipo na inaangalia tuu!, mahakama hizi zilikuwa na wanasheria kweli?.
  27. Kuna uamuzi fulani wa mahakama yetu unaosema “the court is not the custodian of the constitution” kama mahakama yetu inaweza kutoa uamuzi wa namna hii, na huku Tanzania tuna wanasheria manguli, na hawakufanya lolote, jee tuna wanasheria kweli?.
  28. Namalizia kwa lile swali la msingi la makala hii, "hivi kweli sisi Tanzania tuna wanasheria wa ukweli au tuna wasomi tuu wa sheria, waliosomea sheria na kuhitimu?. Kama ni kweli tuna wanasheria, jee wanasheria waliopo ni wapo kweli au ni wapo wapo tuu?!.
  29. Kama kweli Tanzania tuna wanasheria, na wapo kweli, ilikuwaje kuwaje, madudu makubwa hivi ya ajabu hivi ya kisheria, yakafanyika ndani ya nchi yetu kuanzia kwenye serikali yetu, bunge letu na mahakama yetu?, yaliweza kufanyika vipi wakati tuna wanasheria tena wengine ni manguli na wabobezi na wabobevu!, huo unguli wao ubobezi na ubobevu ni kwenye nini?!
  30. Tukutane Wiki Ijayo kwa muendelezo wa makala hii ili kuwafungua macho Watanzania wenzangu, muone jinsi haki kuu mbili za kikakatiba zilizotolewa na katiba yetu, jinsi zilivyokuja kuporwa na kuona jinsi tulivyo na wanasheria wa ajabu!, ili wanasheria tuji thathmini kama tupo kweli au tupo tupo tuu, na wakati huo huo kuendelea kumshukuru sana Mungu kwa ajili ya kutuletea Rais Samia, ile siku anaruhusu mikutano ya vyama vya siasa, pia alifungua milango ya marekebisho ya sheria hizi za kiajabu ajabu, na hadi marekebisho ya Katiba ambayo mwisho wa siku, ni Samia ndiye atakuja kutupatia katiba mpya!. Kwenye hili la Katiba mpya, tunamuomba Mama Samia ajitahidi sana alifanye ASAP!, before it's too late!, maana possibility hii ya katiba mpya, mimi niliiseme humu enzi za Magufuli, Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. but its very unfortunately Magufuli alitwaliwa kabla hajalitimiza hili, hivyo sasa tunamuomba Mama amtimizie!.
NB. Kwa faida ya wasomaji wapya wa Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ili waweze kuielewa makala hii kikamilifu, makala hii inabidi isomwe sambamba na makala hizi tatu zilizotangulia
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?

Wasalaam.

Paskali
Rejea kuhusu mada hii
  1. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  2. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  3. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  4. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  5. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  6. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  7. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  8. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  9. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  10. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Update
Mchango very objective
Mzee wangu, wakili mwenzangu Pascal Mayalla kuna vitu ama kwa makusudi umevieleza ili kutia chachu wanataaluma ya sheria lakini kuna namna na wewe kama wakili msomi umekuwa mlalamishi.

Kwanini nasema hivyo?
1. Umekwepa kabisa kueleza bayana hayo yaliyofanyika na hili naamini umefanya kwa makusudi, sasa hili linaleta hali ya taharuki, watu watashindwa kupima uliyoyasema na uhalisia.

Nijaribu kufungua hii pandora, kama unazungumzia mabadiliko ya BRADEA yaliyokwenda kubadili kinyemela baadhi ya Ibara za Katiba ya nchi, hakika utakuwa hujamtendea haki mwanataaluma nguli kabisa nchini Profesa Isa Shivji, kwani ameliongelea mara kadhaa swala hili hadi kuandika na makala.

Lakini pia kama utakuwa unaongelea kuhusu suala la haki ya dhamana ambalo nalo Mahakama ilikwishatamka kuwa kile kifungu cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuwa ni batili na kinyume na katiba, basi utakuwa hujamtendea haki mwanataaluma mwingine Mheshimiwa Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, kwani na yeye amekwisha kuwahi kulizungumzia.hili tena kwa kuandika makala kabisa juu ya dhamana kuwa haki kikatiba.

Hapo nimeharibu kufungua pandora kujua ni kipi hasa unachokilalamikia kama sio kukizungumzia, wakili msomi.

2. Umeshindwa kabisa kutenganisha majukumu kwa kila eneo la kiutendaji walipo wanasheria, msomi umeshindwa au.umeacha kabisa kueleza kuwa kazi ya kubadili sheria hizo ipo kwa nani chini ya utaratibu gani ili watu wapime je tatizo lipo kwa nani hasa.

hapa nifafanue mchakato wa kubadili sheria hizo japo kwa ufupi kwa kuwaweka wahusika.

Msomi tutakubaliana kuwa Mahakama inatoa uamuzi wake kisha utekelezaji unafanywa na vyombo vingine kwenye.minajili ya mada hii. Sasa vyombo hivyo vinamjumuisha.wanasheria.Mkuu wa serikali, wizara husika na mpiga chapa mkuu wa bunge (sijui kama ni kiswahili sahihi) au Chief Parliamentary Draftman na mtu mwingine ambaye anajificha sana Wakili wa Bunge.

Sasa hawa wote ukiwaangalia wanatoka mihimili miwili, Serikali na Bunge. Kwa kuwashambulia wanasheria wote ukiwepo pia msomi na kuhoji kama wapo ni kukosea sana na kutupa mzigo kusikotakiwa kwani hata tukisema tuwenge nguvu sisi kama sisi sio watendaji wa hilo swala zaidi tutakuwa ama wahamasishaji au walalamikaji (vitu ambavyo vinafanyika kila siku), sasa tujiulize je misingi ya kitaaluma inatutaka tuwe hivyo?, jibu ni hapana kwani zipo njia sahihi juu ya hayo na huwa zinafuatwa.

Juu ya hili naweza kusema kuwa hoja yako wakili msomi umeielekeza hadi kwa watu ambao kimsingi sio watendaji wa maswala hayo.

Yapo mengi lakini kwa sasa naomba niishie hapa nitaeleza zaidi kadiri mjadala wa uzi huu utakavyoelekea msomi
 
Namalizia kwa lile swali la msingi la makala hii, "hivi kweli sisi Tanzania tuna wanasheria wa ukweli au tuna wasomi tuu wa sheria, waliosomea sheria na kuhitimu?. Kama ni kweli tuna wanasheria, jee wanasheria waliopo ni wapo kweli au ni wapo wapo tuu?!.

Kama kweli Tanzania tuna wanasheria, na wapo kweli, ilikuwaje kuwaje, madudu makubwa hivi ya ajabu hivi ya kisheria, yakafanyika ndani ya nchi yetu kuanzia kwenye serikali yetu, bunge letu na mahakama yetu?, yaliweza kufanyika vipi wakati tuna wanasheria tena wengine ni manguli na wabobezi na wabobevu!, huo unguli wao ubobezi na ubobevu ni kwenye nini?!

Tafakuri yangu
Tanzania tuna wanasheria wazuri ambao wanaijua sheria na practice zake kwenye field, tatizo lilikuwa ni mfumo uliwakataa kwakuwa hawakuwa ama hawakukubali kuwa sehemu ya mfumo usiojali wala kuheshimu taaluma na wanataaluma

Siasa ina nguvu sana Tanzania ni hili ndio kosa kubwa kuliko yote! Hakuna maamuzi yenye weledi wa kitaaluma hasa kwenye sensitive cases.. Maamuzi mengi yanaingiliwa na maslahi ya kisiasa hasa kwa chama kilichopo madarakani
 
we have people who have studied law, they are not lawyers, because many laws have mistakes and need to be improved, but they do not see that

For example, the child law states that a child is not allowed to marry under the age of eighteen, but the marriage law opposes that, saying that if a person reaches the age of eighteen, they are allowed to marry.

because until here you can know that we have legal scholars who were violating the law and not understanding their duties and what they are supposed to do and when
 
Wanasheria wapo wengi wazuri,hata hao waliotunga hizo sheria,au kuziacha zipite,hawakufsnya kwa bahati mbaya,wananufaika na mfumo huu,wanajua kabisa ukienda kiunyume na mfumo,ccm watakuzima utakosa ulaji,
Wabunge wa ccm wanajua kabisa sheria mbovu zinapopirishwa,lakini wanajua wakipinga,watafukizwa chamani na watapoteza ubunge na mapesa yake yote,swali ni nani yupo tayari kupoteza milioni 200+za ubunge,mshahara milioni 11 kila mwezi??Hata hao chadema haijawahi kusikia wakisema Mbunge akatwe Kodi,au posho ya kukaa ifutwe!!hawawezi kusema.
 
Wanasheria feki wapo wengi, tena ajabu zaidi ipo kule bungeni, ambapo kiongozi wa muhimili wa kutunga sheria anapoamua kuwakumbatia wanawake 19 wasiowakilisha chama chochote kinyume cha katiba, kwa manufaa ya chama na serikali yake.

Halafu ajabu kubwa zaidi kupita yote, ni huyu mwandishi anayeuliza kama tuna wanasheria wa kweli, ambaye nae kila siku huwatetea wale wanawake 19 kule bungeni kwa manufaa ya chama chao, lakini chakushangaza, amekuja hapa kutuuliza kama Tanzania tuna wanasheria wa kweli au vibogoyo..

Jibu langu kwake ni fupi tu, tuna wanasheria vibogoyo, na mfano wao ni yeye mwenyewe..
 
Wanasheria feki wapo wengi, tena ajabu zaidi ipo kule bungeni, ambapo kiongozi wa muhimili wa kutunga sheria anapoamua kuwakumbatia wanawake 19 wasiowakilisha chama chochote kinyume cha katiba, kwa manufaa ya chama na serikali yake.

Halafu ajabu kubwa zaidi kupita zote, ni huyu mwandishi anayeuliza kama tuna wanasheria wa kweli, ambaye nae kila siku huwatetea wale wanawake 19 kule bungeni kwa manufaa ya chama chao, lakini chakushangaza, amekuja hapa kutuuliza kama Tanzania tuna wanasheria wa kweli au vibogoyo..

Jibu langu kwake ni fupi tu, tuna wanasheria vibogoyo, na mfano wao ni yeye mwenyewe..
Umemaliza yote
 
With due respect; hoja moja unairudiarudia sana, sijui ili kuwa na paragraphs nyingi au ndio msisitizo!!? I suggest you work on that.
Mimi nimelazimika ku skip nione hoja mpya na hitimisho. Pia mwandishi haendi moja kwa moja kwenye point anayotaka hadhira ijue maana mwisho anahitimisha kwa kurejea mada ya nyuma hivyo kufanya mjadala wake uwe km vipengele vilivyopita na vinavyokuja..namna hii ya uandishi si nzuri sana kwa msomaji mpya wa mada zake maana anaandika kichwa cha mada kinachovutia lakini habari ina marudio rudio ya hoja.
 
Mada safi ya kuanzia mwaka, JUDICIARY yetu sio huru, haina uamuzi wake wenyewe, kila maamuzi yake yanategemea politicians, mfano mzuri kesi nyingi zimefutwa baada ya political will na sio kisheria, narudia tena ,wakati utakapofika wa judge's kujichagua wenyewe na kuwa na maamuzi yao ndio mhimili huu utasimama wenyewe
 
Mada safi ya kuanzia mwaka, JUDICIARY yetu sio huru, haina uamuzi wake wenyewe, kila maamuzi yake yanategemea politicians, mfano mzuri kesi nyingi zimefutwa baada ya political will na sio kisheria, narudia tena ,wakati utakapofika wa judge's kujichagua wenyewe na kuwa na maamuzi yao ndio mhimili huu utasimama wenyewe
Katiba mpya natumai itarekebisha haya madudu yote
 
Mada safi ya kuanzia mwaka, JUDICIARY yetu sio huru, haina uamuzi wake wenyewe, kila maamuzi yake yanategemea politicians, mfano mzuri kesi nyingi zimefutwa baada ya political will na sio kisheria, narudia tena ,wakati utakapofika wa judge's kujichagua wenyewe na kuwa na maamuzi yao ndio mhimili huu utasimama wenyewe

Ukiona taaluma unavamiwa na wanasiasa tambua viongozi wake wapo kimaslai yao binafsi

Wamesoma sheria na bado wanafanyiwa maamuzi hiyo sawa kweli
 
Back
Top Bottom