JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Ni kweli na namuunga mkono ni fedheha hasa hasa. rejea pia aliyoyasema akiwa Ethiopia kuhusu tatizo ili hivi karibuni!
 
Serikali ya Tanzania haina dini. Viongozi wote wa serikali wanatakiwa kusimamia sheria bila kujali dini. Mambo yanayohusu dini wawaachie viongozi wa dini.
Misuguano ya kidini iliyopo hivi sasa ni matokeo ya kuchanganya dini na siasa!
 
angalia hapo kwenye red, yaani wewe una matatizo makubwa, tena wewe ni muislam, acha kutuzuga hapa. kama huna cha kuongea you better keep quit!!!!!!
Mkuu mwandiko wake tu unaonyesha yeye ni nani!kachanganya point na pumba humohumo.solution ni bora kila dini itengewe machinjio na mabucha yake.period!
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Na je vipi kuhusu mauaji ya Mwangosi,kule Arusha,Morogoro,Songea,Tarime na kwingineko?je mateso ya Dr Ulimboka?USANII MTUPU.
 
Ninatamani sana kama ingewezekana kuweka hadharani hukumu ya watu wanapelekea migogolo ya kidini katika jamii yetu.
Inawezekanaje mtu anapokosea anahukumiwa mitaani kwa kuuawa na bado tunasema tunafuata utaratibu wa sheria?
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Kwani alitegemea matokeo ya zile kampeni ni nini?
 
Kugombania kuanza kuchinja wanyama ni fedheha maana miaka yote hii nani alikuwa ana chinja na mambo mbona yalikuwa yanaenda bila shida, na kupigana sababu ya kuchinja ni fedheha na kuuana sababu ya kuchinja ndio kabisaa. Udini unaoendeshwa na watu wasiojua dini tusiuvumbie macho! Utatuharibia Taifa letu.

si wanajulikana ccm ndo walioeneza na wanaoeneza huo udini!
 
Hakika ni fedheha na imetia doa serikali na nchi kwa ujumla.

Doa ni kubwa sana......suluhu ni kama alivyopendekeza jmushi1 .......ya kwamba kuanzia sasa tutumie utaratibu kama kwenye nchi nyingine......halaal na kinyume chake.......
 
Last edited by a moderator:
Huku kuchinja kweli sasa naona ni mtihani mgumu sana kwa Wakristo. Sisemi Wakristu kwa kuwa nimefuatilia thread hii inaonekana Biblia kidogo ni ngumu kwao kuelewa ndiyo maana wanadai hawajali. Wakristo walikuwa hawajali kwani Biblia inasema, Msiulize-ulize, na ikawa hivyo. Lakini alitokea Wassira akaeleza kabla ya kuulizwa kuwa kuchinja ni lazima Waislamu kwa kuwa wanafanya ibada. Sasa hatuna tena haja ya kuuliza kwani si sahihi kula chakula ambacho kinahusishwa na ibada ya miungu huku tukijua kwa dhahiri. Tumekatazwa kuabudu miungu mingine. Ninatamani wahubiri makini wa injili, siyo wakuu wa dini, wangelitolea jambo hili tamko ndipo malumbano yangeisha. Wakristo wangejua ni lipi sahihi.
 
Hapo kwenye red kama una uhakika hao viongozi wateule ndo wametoa maagizo yanayovunja amani basi hapo ndio kuna tatizo..Na raisi anawajibika kwa hilo kwa kuwa hao ni wateule wake.

Ninayo hakika kwa asilimia nyingi, na vyombo vya habari, hata humu jf wametajwa waliotoa maagizo yanayokiuka tulivokuwa tu naishi mwanzo, Pamoja na kutajwa bado hawajakanusha kutengua kauli zao zilitengua "tulivyokuwa tukiishi mwanzo"
 
unaonaje kama saa hizi waislam wakaanza kula vilivyochinjwa na wa kristu, kwa sababu wao wamechinja kwa muda mrefu?Hapo itakua ni kupokezana kijiti.

Nakubaliana na wewe mimi naoana kila mtu awe na bucha lake liandikwa na anuani kuonyesha ni la dini gani...
Pia waislamu wasikilizwe madai yao Ijumaa tupumzike isiwe siku ya kazi.....
 
Ninachofahmu mimi tangu tunapata uhuru waislam ndio wanachinja, hata katika machinjio yote ambayo nyama yake inatumiwa na umma, na hata katika masoko ya kuku wachinjaji ni waislam, sasa leo wakristu tunataka nini jamani, tuwaachie waislam waendelee kuchinja kwa dini yao inatoa elimu (ustaarabu) namna gani mnyama au ndege anavyotakiwa kuchinja, kwani mbali na hilo nyama hiyo itakuwa ni kibudu tu!
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.
najaribu kutafuta tofauti yako na Wassira nimeshindwa kuipata.......vichwa maji wote
 
Umoja na mshikamano wa watanzania ni zaid ya jambo lolote kwetu.

Tutaswali misikitini kama kunaamani

Tutasali makanisani kama kunaamani

Tusipende kuhukum na kunyoosheana vidole kwasababu katika misingi ya iman siku ya kiama mungu atatoa hukum

kwa kila mmoja wetu. Tutendeane mema kwa upole na unyenyekevu tukiamini kwamba motoni kupo. Kumsaidia mungu

kutoa
adhabu na kuhukumu ni kama kumfanya mungu hana uwezo na nidhaifu. Na huu ni upungufu mkubwa wa

kimaamuzi katika ubinadam wetu, mungu hasaidiwi wala hapiganiwi anajitoshereza kwa maana ni chanzo cha yote.

Tujipiganie nafsi zetu kwa kutenda mema ili siku ya kiama tupate kuingia peponi tukifanya hivi tutakuwa salama kwa

pamoja waislam, wakristu, wapagani wahindu nk na Tanzania itadum katika amani na neno kisiwa cha aman litadum

kinyume chake ni maafa na Tanzania itaangamia.
 
Hakuna ulicho toa suluhisho zaidi ya maongezi ya mzunguko. Ukweli ni kwamba suala la kuchinja ni suala la imani. Na katiba haitamki ni dini gani yenye uhalali wa kuchinja nyama. Nchi yetu inaongozwa na katiba na sio imani. Anayempangia mwenzake dini gani ichinje na dini gani isichinje ndiye mfanya fujo namba moja. Ugomvi unatoka wapi? Wakristo wachinje nyama zao na waislam hali kadhalika wachinje nyama zao. Tatizo liko wapi? Watu wasilazimishwe kufuata imani ya dini nyingine kwa suala la kiimani. Hakuna la maana kulazimisha wengine wachinjiwe nyama in the name of mshikamano wa kitaifa. Busara ya namna hiyo ni kuogopa ku face ukweli. Na busara isiyoleta tija ni hasara na hivyo iachwe au kutupwa kabisa.
 
[QUOT
E=mchongo;5684203]Ninachofahmu mimi tangu tunapata uhuru waislam ndio wanachinja, hata katika machinjio yote ambayo nyama yake inatumiwa na umma, na hata katika masoko ya kuku wachinjaji ni waislam, sasa leo wakristu tunataka nini jamani, tuwaachie waislam waendelee kuchinja kwa dini yao inatoa elimu (ustaarabu) namna gani mnyama au ndege anavyotakiwa kuchinja, kwani mbali na hilo nyama hiyo itakuwa ni kibudu tu![/QUOTE]

Tatizo ni Ibada ya Mungu wao Allah! Ambao wa kristo wanaamini ni shetani.
 
Wewe ni mkristo wa kurithi na sio wa imani na hata hujui Christian theology. Kuchinja tu peke yake ni tendo la ibada be it to Christians or muslims. Na ndio sababu waislam wanang'anga'ania kuchinja kwasababu ni ibada. Ukilitazama kibiashara utatupa hiyo picha yako ya makengeza. Watu wasilazimishwe. Unataka kusema wakristo wakikataa kuchinjiwa nyama na waislam basi walazimishwe kwa mapanga au kubembelezwa kwa kauli nyepesi nyepesi? Kuchinja ni suala la imani. Period!
 
Kwani yeye aliwatuma wakamuue!!Si wameamua wenyewe na akili zao zilivowatuma

Kama Rais alitakiwa atoe tamko kuhusu nani anayetakiwa kuchinja maana maneno aloongea hata wanangu waliongea hivyhivyo baada ya kusikia taarifa ya habari, Sasa kwa maneno hayo nimeshindwa kutofautisha kati ya wanangu na rais ni nani mwenye nguvu.
 
Back
Top Bottom