JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

Mimi sina tatizo la nani achinje nani asichinje, ila ninachotaka kusema, nisisikie waislam wanasema kwao kuchinja ni ibada kwa vile mimi mkristo aslani siwezi kushiriki ibada ya waislam. Lakini siku wakisema wanachinja kwa ajili ya biashara tu hapo sitakuwa na sababu ya kutokula nyama waliyochinja.
 
Unalotaka kuaminisha watu sio sahihi, ukristo uko wazi kuwa " hatutahukumiwa kwa kundi", "kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe". Msalaba wako, uko katika amri kumi za Mungu. Na katika amri hizo hakuna ndogo na hakuna kubwa, zinatakiwa kutimizwa kwa ukamilifu wake na kwa ujumla wake. Katika amri hizo kumi hakuna ya "kuchinja au kutochinja mnyama". Jumuisho la amri hizo kumi ni "Upendo" na "uchaji Mungu wetu",usiokuwa na shaka na wala masharti. Kurithi au tafuta mwenyewe hakupo hapa.

Ukiamua kumkosoa mtu onesha eneo au neno au sentensi iliyokosewa au iliyotumiwa vibaya. Useme jumla jumla tu, hutamsaidia mtu.

mkuu, ukristo umejengwa juu ya amri kumi? kasome tena upya utaelewa kuwa ukristo ni zaidi ya amri 10. mimi sion tatizo muislam kama binadamu mwingine kuchinja alafu nikala. tatizo ni pale ambapo linaonekana kuwa ni ibada. hapo ndipo linapokuja suala nyama iliyotolewa sadaka kwa shetani.
 
Katika vita lazima mmoja afe, au kwa kuwa mtumishi ndio limempata? si walikuwa wanapigana..
Fujo za Mbagala nilimsikia Rais akisema Aliyekojolea kuraani kakosea na aliyechoma makanisa kakosea - Rais alishindwa kumjua mkosaji na kumkemea. Akaamua kuwa Neutral.

Jana kuhusu mauaji ya Buseresere, Rais anasema wananchi wa imani tofauti wajenge kuvumiliana. Again hamjui nani anayestahili kukemewa. Akaamua kuwa Neutral.

Hivi kweli kauli hizi zinasaidia kitu? zinaweza kuzuia yaliyotokea yasitokee tena? Hivi kweli katika matukio haya Rais hajui nani anastahili kukemewa kulingana na katiba iliyopo?

Rais anamuoneaje aibu mhalifu na kunutralize issues kijuujuu. Rais unaposhindwa kutetea haki za kundi lililoonewa wananchi wanakujudge kuwa unabelong katika kundi la wachokozi/wahalifu. Haiwezekani ukawa neutral kama kiongozi asiyejua anachopaswa kukisimamia katika jamii anayoiongoza.

Mfano katika issue ya Buseresere ni nani alitakiwa amvumilie mwenzie? kwa nini Rais anatoa statements zinazotuacha hewani?
 
Wakati mwingine hua tunashangaa mbegu tuliopanda inazaa mbegu nyingine nyingi, sijui ni kutokujua au tumevamia kilimo!
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

MNAFIKI!! kwani yeye sie yule muanzilishi wa UDINI Tanzania, kikiwepo chama cha waislamu kiitwacho BALUKTA??
 
Ninalosema hapa ni moja, kufanya jambo unaloamini kwamba halitamkwaza mtu. Inahitaji mtu kujiamini kuwa kwa vigezo vyovyote wewe haujahusika kufanya jambo kwa nia ya kutatiza imani ya mtu. Sitetei tabia ya watu kujichukulia hatua ya kuuwa wenzao, ndio maana nikasema hao ni wauaji wanastahili kuchukuliwa hatua bila ya kuhusisa madhehebu yao. Hayo ni mauaji na sheria ziko wazi.

Kuna jambo moja la msingi ambalo linakusumbua na ndiyo maana unajitahidi kujieleza lakini bado unapata upinzani. Kama ungekua umeisoma na kuielewa historia ni kwamba machafuko karibu yote,chanzo huwa ni jambo dogo ambalo kwa kawaida watawala wanakua wamepuuzia kiini cha tatizo! Ukristo umetukanwa sana hapa Tanzania kupitia redio,magazeti na kanda zinazosambazwa na ya makundi ya Waislamu lakini hakuna hatua za msingi zimechukuliwa na watawala. Watu tunatofautiana ktk uvumilivu hasa inapokua ni kudhalilishana. Kuna Wakristo wana hasira,sababu ndogo ikipatikana basi wataitumia kumaliza hasira zao! Rais Kikwete inawezekana hajui kwa kiasi gani dini hizi mbili sasa hatuaminiani,pengine ndiyo maana akamtuma mtu hasiye kuwa na busara kama Wasira kusuruhisha mgogoro wa kuchinja huko Mwanza!
 
Katika kikao chao hicho cha chama, wamempokea pia Juliana Shoza na Mwampamba, hawa watatumika sana kuiua CHADEMA, topic watakayo itumia ni hiyo hiyo, udini na ukanda, hizi ndio mbegu ambazo serikali yako mkuu ulizipanda, namshukuru sana Mungu mbegu hizi hizi, zimeota na kukua na hatimaye zinafunwa wakati wako, kingekua kitu kibaya sana kama mtu mwingine ambaye ni innocent aje avune matunda haya, dalili ninazo ziona ni kwamba kwa tukio lile la kule Geita, mabaya zaidi yanakuja, habari nilizozipata ni kua, polisi wamewakamata baadhi ya wachungaji kwa tuhuma za mauaji ya mchungaji mwenzao, kwahili sidhani kama Wakristo kama watalikubali hili, ccm wanahubiri kwamba wameleta amani, wanadhani amani ni kitu kinachokuja hivi hiv, amani huletwa kwa matendo ya haki, nje ya hapo ni kudanganyana, Juliana na Mwampamba wakihubiri hayo niliyoyasema hapo juu basi ujue kua magamba hawana shida na amani ya nchi, shida yao ni kua madarakani basi!
 
mimi tangu nazaliwa nakula nyama iwe aliyechinja ni mkristo au muislam i don't give a damn!! ila kinachonipa shida ni pale muislam anapoihukumu nyama kuwa ni haramu kwa kuwa mchinjaji ni mkristo ilhali nyama aliyochinja yeye muislam anataka mkristo aikubali kuwa ni halali!! hapo panaleta utata kwa kuwa inakuwa kama dharau, matusi na ubinafsi!! lazima serikali ikubali kuwa imetenda kosa kwa kupitia kwa akina ndikilo na wasira ambao walikosa busara ya kushawishi wakristo badala yake wakatoa kauli za ovyo za kujipendekeza kwa bosi wao jk ambaye ni muislam tena kauli zilizo kinyume na katiba yetu ambapo imepelekea mgogoro kuzidi makali, hawa viongozi wanatakiwa wachukuliwe hatua kali sana!!
 
Kama raisi anapaswa kuzungumzia swala lolote linalo gusa nchi,Jamani watanzania kujifanya mnaleta siasa na udini pasipo stahili kutagharimu kila mtu?uwe shekh ,padri,mumini au yeyote...Dini ya kislam kuchinja ni Ibada kwa msojua ikiwa kama sikuzote waislam wamechinja na sasa wa cristo mnataka nanyi mchinje basi Basi mabucha ya nyama za wa crosto yajulikane na nyama wanazo chinja waislam zijulikane kwa sababu kwa mujibu wa dini ya kisla ni haramu kula nyama ilo chinjwa na asie kuwa muislam...na ama kwa mauwaji yalotokea Ni haramu kwa muislam Kuiwa nafsi pasina haki ya kuwawa hivo basi muislam kama umetoa roho ya kiumbe kwa dhulma basi Unamajibu mazito yakutoa kwa mola walo....Wa billahi tawfiq
 
zamani hatukujua kwamba kwa wenzetu kuchinja ni ibada kwa mungu wao,saa kwa kuwa tumejua nyama yetu twataka tuchinje wenyewe maana hata sisi tunao huo uwezo

Kugombania kuanza kuchinja wanyama ni fedheha maana miaka yote hii nani alikuwa ana chinja na mambo mbona yalikuwa yanaenda bila shida, na kupigana sababu ya kuchinja ni fedheha na kuuana sababu ya kuchinja ndio kabisaa. Udini unaoendeshwa na watu wasiojua dini tusiuvumbie macho! Utatuharibia Taifa letu.
 
raisi jakaya mrisho kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa cc jk alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

mpuuzi tu, badala ya kutoa kauli na kutangaza sheria za uchinjaji ziwe wazi, anaendelea kumung'unya maneno? Poor president
 
Kama raisi anapaswa kuzungumzia swala lolote linalo gusa nchi,Jamani watanzania kujifanya mnaleta siasa na udini pasipo stahili kutagharimu kila mtu?uwe shekh ,padri,mumini au yeyote...Dini ya kislam kuchinja ni Ibada kwa msojua ikiwa kama sikuzote waislam wamechinja na sasa wa cristo mnataka nanyi mchinje basi Basi mabucha ya nyama za wa crosto yajulikane na nyama wanazo chinja waislam zijulikane kwa sababu kwa mujibu wa dini ya kisla ni haramu kula nyama ilo chinjwa na asie kuwa muislam...na ama kwa mauwaji yalotokea Ni haramu kwa muislam Kuiwa nafsi pasina haki ya kuwawa hivo basi muislam kama umetoa roho ya kiumbe kwa dhulma basi Unamajibu mazito yakutoa kwa mola walo....Wa billahi tawfiq

yajulikane vipi wakati bucha iliyochomwa na wakafanya vurugu, kwanza ilitangazwa lakini pia waliandika WAKRISTO BUCHA? Suala sio kujulikana, kwani waislam walitambua kabisa suala ni wao kupoteza nafasi ya kutoa kafara na tozo la 3000 kwa kila ng'ombe.
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.

Kaka nakupongeza kwa uliyoyanena. natamani akili zako ungewaazima kidogo hao wacungaji waliokomaa na hilo. na ninakuomba usichoke kuwaelewesha hata humu humu jf wamo wakristo ambao wanahitaji uwaazime akili zako. Bro umeandika vizuri kabisa na mwenye akili timam kakuelewa
 
Kwani yeye aliwatuma wakamuue!!Si wameamua wenyewe na akili zao zilivowatuma

msingi umejengwa na kikwete, baada ya ikulu yake kuruhusu dini yake kuikashifu dini nyingine, cd za kuchafua dini za wakristo zimezagaa mitaani nani asiyelujua hilo, upotoshaji wa kukashfu dini nyingine unashika kasi kila kukicha kupitia radio imani, hii dhambi itawatafuna viongozi walioleta udini kama sera za kupondea chama kingine, wataficha ukweli lakini MUNGU anajua kweli, viongozi wa ccm mtajua nguvu ya MUNGU ikoje wakati umefika sasa kwani, wanatembea na kucheka bila kujali, poleni wafiwa huko katoro, majeruhi MUNGU atawapa faraja la matumain ili mpone haraka
 
Kugombania kuanza kuchinja wanyama ni fedheha maana miaka yote hii nani alikuwa ana chinja na mambo mbona yalikuwa yanaenda bila shida, na kupigana sababu ya kuchinja ni fedheha na kuuana sababu ya kuchinja ndio kabisaa. Udini unaoendeshwa na watu wasiojua dini tusiuvumbie macho! Utatuharibia Taifa letu.

Usimung'unye maneno JK ni muasisi wa udini ndizo ahadi alizowapa waislamu, kwa udhaifu wake hakufikiria matokeo yake. NA BADO!!
 
Tunamjua muasisi wa hizi ***** ***** za kidini, madaraameayapata kwa njia ya kuwagawa watanzania lakini adhabu yake itakuwa hapa hapa duniani
 
suala hapa siyo fedheha wewe kama mkuu wa kambi umechukua hatua gani katika suala hilo kwani ukisema ya kuwa mauaji haya ni fedheha nani sasa unayemtaka achukue maamuzi? kwa rais wetu wa jamhuri imeonekana mara kwa mara ya kuwa pindi zitokeapo vurugu za kidini kmuu wa kambi huwa anajitoa na kuwatupia raia rawama kana kwamba yeye hana cha kufanya katika hilo
kwangu mimi hili suala naliona tofauti na kama mkuu wa kaya ataendelea kukaa benchi akisubilia muujiza wa kutuliza hizi vurugu za kidni zinazoendele itafikia hatua raia nao watakosa uvumilivu maana hawaoni hata chembe ya juhudi inayofanywa na mkuu wao wa kambi na hapo ndipo utasikia amani ya taifa hili mashakani
na sijui siku hiyo atasema nini maana dhambi zote zitakuwa juu yake na wale watakaouwawa damu zao yatakuwa ndo machozi yake
 
Wambagala walisakwa. Wa Mtwara wanasakwa. Wa Geita watasakwa. Sidhani kama kusakana kunajibu maswali magumu. Lets face the reality.
 
Kwa hiyo akina Daniel,Meshack na Abednego walikuwa na imani haba kiasi cha kushindwa kutakasa chakula cha mfalme kiasi cha kuchagua kula mtama tu?
zama za Danieli na wakina meshak Jina la YESU lilikuwa bado halijakabiziwa kwa wanadamu, lakini tangu enzi za yohane mbatizaji mbaka sasa tumepewa jina lipitalo majina yote Jina YESU kwalo kila kicho dhaifu na kichafu kitatakaswa hata tukila vitu vya kufisha havitatuzuru,by the way sikatai kusema wao kwa iamni yao kuchinja ni ibada yaweza kuwa hivyo tambua hata nafaka na vyakula vingine vingi tunavyokula asilimia kubwa vimeunganishwa na ibada za miungu mingine ila kwa kuzitakasa na kubariki basi twaondoa roho chafu na kuweka afya na utakaso wake MUNGU WETU WA KWEKLI.lakini dhamira ikikusuta usule basi na usile.
 
Back
Top Bottom