JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

Ndio Kikwete huyo, dhaifu kifikra, dhaifu kimatendo, dhaifu kimaneno.

Mbona kwenye ishu nyingine vijana wake wa kazi ni wepesi sana kuwahushughulikia "wahalifu"? CCM wamelokoroga na sasa watalinywa tu.

Watanzania walikuwa na dini zao, walikuwa na makabila yao lakini walivumiliana na kuishi kwa maelewano na kupendana. Lakini kumbe Jakaya Mrisho Kikwete hakuwa anapendezwa na hilo ndipo alipoamua kuwatenganisha kwa imani na makabila yao.

Ninachokiona kwa sasa ni kuwa hana akili (kubwa) ya kutatua tatizo alilotengeneza kwa akili ya kiwango fulani. Kwani inamtaka awe na akili kubwa kuliko ile aliyotumia kutengeneza tatizo na hana hiyo akili.

Kwa unyenyekevu na kujiamini nasema tuko (Watanzania wazalendo) tayari kumsaidia na kuisaidia nchi yetu tuipendayo lakini akubali kuwa kashindwa na akae pembeni, maana asipokaa pembeni bado ataingilia na kuharibu.
 
Katika hili watanzania wenzangu tusikubari kuburuzwa na mtu yeyote! Tusimame kama taifa moja, ndugu moja na familia moja . Watanzania tumechangamana sana, hakuna familia au ukoo usiokuwa na waislam au wakristo au kuoleana au ujirani na urafiki pia. Hili suala tusikubari hata siku moja litugawe, ndugu zangu wanaJF nmekuwa nikiangalia post mbali mbali hapa zikipostiwa cha ajabu watu wengine wanaangalia ubinafsi zaidi kuliko kuangalia utaifa. Kwa hili hebu ndugu zangu tujaribu kuangalia wadogo zetu, watoto wetu, baba zetu, mama zetu, babu zetu, bibi zetu nk nk. Si busara kushabikia mauwaji eti tu tunashabikia dini zetu, hebu suara la imani zetu libakie kwetu kama sisi na imani zetu tusikwazane kwa masuala ya imani ndugu zangu. Viongozi wa dini mbali mbali, viongozi wa kada mbali mbali tafadharini kama ni tunalipenda taifa letu kwa dhati tuhubiri kutokomeza mauaji haya na kwa umoja wetu bila kuangalia itikadi zetu tulaani kwa pamoja mauaji haya yasipate kurudia tena. Imani yangu ni kwamba hakua sehemu kwenye quran au biblia inaporuhusu kuchinjana! Narudia tena ndugu zangu hapa tulipofikia tuseme kwa pamoja kuwa inatosha na tusikubari kamwe kutumiwa na watu wanaotafuta umaarufu aidha kidini au kisiasa! Si utamaduni wetu watanzania huu.

Asanteni na samahani kwa kuchukua muda wenu.

you sound preachy and boring
 
Fujo za Mbagala nilimsikia Rais akisema Aliyekojolea kuraani kakosea na aliyechoma makanisa kakosea - Rais alishindwa kumjua mkosaji na kumkemea. Akaamua kuwa Neutral.

Jana kuhusu mauaji ya Buseresere, Rais anasema wananchi wa imani tofauti wajenge kuvumiliana. Again hamjui nani anayestahili kukemewa. Akaamua kuwa Neutral.

Hivi kweli kauli hizi zinasaidia kitu? zinaweza kuzuia yaliyotokea yasitokee tena? Hivi kweli katika matukio haya Rais hajui nani anastahili kukemewa kulingana na katiba iliyopo?

Rais anamuoneaje aibu mhalifu na kunutralize issues kijuujuu. Rais unaposhindwa kutetea haki za kundi lililoonewa wananchi wanakujudge kuwa unabelong katika kundi la wachokozi/wahalifu. Haiwezekani ukawa neutral kama kiongozi asiyejua anachopaswa kukisimamia katika jamii anayoiongoza.

Mfano katika issue ya Buseresere ni nani alitakiwa amvumilie mwenzie? kwa nini Rais anatoa statements zinazotuacha hewani?

wezi wa epa warudishe
wauza unga anawajua
...........................
 
Ili tupate nini sasa? Do we understand well the christianity teachings in the holy bible? Kuacha kuchinja...is it something too much to allow? Kuacha malumbano kwenye issue kama hizo kunatugharimu nini? Hatuna mambo muhimu ya kufanya tuanze kugombania kuchinja wanyama?

Suala hapa ni pale unapopewa favour wewe unaigeuza kuwa haki.Waislamu walipewa favour tu,ya kuchinja na wakristo, wao wameigeuza kuwa haki.Favour hiyo ilitokana na kuheshimiana.Sasa kwa sababu wamei abuse then, kila mtu achinje vyake.Kuendelea Kuentertain huu upuuzi hautaisha.Kuna watu kizazi kijacho watakuja kuhoji ,na litaleta matatizo pengine kuliko leo.So long as tatizo limetokea, sasa linahitaji suluhisho na wala si kufichaficha na kulihamishia kwa kizazi kijacho.Tumeona madhara ya mambo yanayofunikwa funikwa ndio yaliyotuharibia Taifa hili.Richmond,Kagoda,Meno ya tembo,Gesi, yote haya yanafichwa fichwa ndio maana tunapata matatizo.Lazima kuwe na solution ili mbivu na mbichi ijulikane.Ukweli ukiwekwa hadharani hata kama utaudhi upande mwingine ,ndivyo ulivyo.Ukweli huwa haubadiliki.sasa kwa nini ufichefiche mambo?Tuache Unafiki ndio uliotufikisha hapa tulipo.Mambo ya kupeana kauli za kufarijiana hata pale tunapoharibu, ili tusionekane wabaya ndio yanayowatia watu ujinga.Kwa hili kuna watu wamekosea, waambiwe wamekosea na si kwa umauma maneno.Kwani wanapata nguvu kuwa wanaogopwa ,hivyo kesho watazua jingine.

Tuacheni Unafiki.
 
Ndugu zangu watanzania kwa imani yetu ya kiislamu Quran inasema hivi

Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi. [108:2]
Sali na chinja kwa ajili ya mola wako mlezi hivyo kwa muislamu kuchinja lazima afuate misingi ya uchinjaji ya Mola wake mlezi kwani ni sehemu ya Ibada kwa mwislamu

Siabudu mnacho kiabudu; [109:2]
mwislamu hawezi kuabudu kile ambacho mwingine anachoabudu

Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. [109:3]
Wengine(wakristo na wapagani) hawaabudu kile ambacho waislamu wanaabudu hivyo hatuwezi kuwalazimisha wafuate sisi waislamu tunachoabudu hii ni pamoja na kutowalazimisha kuchinja
kwa ibada yetu kwani hawaabudu tunayemuabudu,

Wala sitaabudu mnacho abudu. [109:4]
hapa imesisitizwa kwa Muislamu kutoabudu wengine wanachoabudu na hi haki yao pia wao kutoabudu tunachoabudu

Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. [109:6]
Hapa tunaambiwa wao twanadini yao(zao) wanazofuata na sisi tuna dini yetu tunayofuate hivyo sijaona kwanini hili swala lifikie tupigane na kuuwana badala
kurejea kwenye mafundisho ya M.Mungu ili tuwe na amani katika Jamii yetu.

kumbukeni ndugu zangu waislamu Qurani inasema hivi kama tusipofuata maidha kama yaliyoonyeshwa hapo juu

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. (Taa-Haa: 124)
 
Mkuu mechard Rwizile
ni kweli na hakuna aliyekuwa akiharibu nyumba za ibada, au nyumba za bihashara za mwenzake au Kutukanana adharani japo tofauti zetu zinajulikana.

Hili linaweza kuwa linaonekana kwa juu lakini ni kilele cha uvumilivu wa mambo mengi.
Tujikumbushe sakata la Mbucha ya nguruwe pale Dar (namshukuru mzee Ruksa alitumia Busara zake), Makanisa Zanzibar.
Kuna haja gani ya kushirikiana na adui unayemjua?.

Tunashauriwa tuwapende lakini tujiepushane nao.

Sijui kama kuna mtu analazimika kula nyama asiyojua imechinjwa na nani na kama jamii yaweza kujiwekea utaratibu wa kupata nyama iliyostahili kwao bila mkwaruzano.

Kwanza wamesaidiwa kuelezwa kuwa sasa Wakristo nao wanachinja kwani wamekuwa wakila nyama hizo bila kujua maana ni nyama nyingi sana zinachinjwa mafichoni na kuletwa alfajiri mabuchani!.
 
Kwa hili Rais alitakiwa kusema kuwa WAISLAM ni wachokozi na wahalifu dhidi ya wakristo na uislam na wanastahili adhabu.
1. Hakuna aliyewakataza wao kujichinjia nyama zao kama watakavyo.
2. Hakuna aliyewalazimisha kununua nyama yoyote wasiyotaka.
3. Hakuna sheria inayowafanya waislamu kuwa wachinjaji pekee popote pale Tanzania.Aidha hakuna sheria inayokataza watu wengine wasio waislamu kuchinja.
4. Quran inawaelekeza waislamu kuwa vyakula wanavyokula wakristo na wayahudi ni halali kwao kula. Kusema akichinja mkristo ni haramu ni dhana potofu yenye mtazamo hasi wa kuficha choyo.
5. Biblia inakataza kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa miungu wengine isipokuwa Yehova. Kuchinja kwao huku wakielekezea Al-kaba (ambayo wanadai kuwa ni ibada) nisehemu ambayo inahojiwa na wakristo.Waislamu wa ukweli wanaweza kuuambia umma kile kilichopo ndani ya Al kaba kama ndiye Allah au ni nini.
6. Kuwavamia watu walioamua kujichinjia kitoweo chao na kuwafanyia fujo ni uhalifu usioweza kunyamaziwa kama ni kitu chema.
7.Kumuua mtu aliyetumia huru wake bila ya kuingilia uhuru waoni kosa ambalo Myngu Yehova atawalipa tu ujira wao.

Tungepata vitendo vikali zaidi ya maneno yake tungeona na kutambua serikali ina msimamo gani, hasa ukizingatia historia ya kuwakandamiza wakristo Tanzania.Kama aliweza kwenda misibani kwa watu kama Kanumba, kwa mtu wa dini nyingine angekuwa wa kwanza kuonesha haungani na watu wa dini yakr juu ya kile walichokifanya.
Haiwezekani kumfurahisha kila mtu lakini inawezekana kusimama upande ambao unadhani unahaki.
 
Hivi wale waliomuua Padri kule zanzibari walishakamatwa?
Na wale waliomtesa Docta Ulimboka vipi wamekamatwa?
Je waliochoma makanisa hivi walikamatwa!, na kama walikamatwa wamechukuliwa hatua gani?
Je waliochoma makanisa mbagala hivi walikamatwa! Na je walichukuliwa hatua gani?
Ukweli unabaki pale pale serikali iko nyuma ya waislamu wanafanya haya matuukio! Na tumeshazoea matamko yanayotolewa na Jk mara nyingi yanakosa mshiko ni yakawaida sana.
Hatuoni akichukizwa na hivi vitendo vinavyoshamira sana wakati huu wa serikali yake,
hatuoni kiongozi anaeweza kuongea wananchi wakamsikia!
Amekua akiogopapa upande mwingine watamfikiriaje!.
Nakumbuka mwalimu Nyerere alikuwa hang'ati na kupuliza ila jk anang'ata na kupuliza..
Amekuwa akimtumia waziri DHAIFU wasira kwenda kusuluhisha wa kristo na waislam kule geita! Matokeo yake tumeyaona.
Tusubiri tuendelee kusikia matamko thaifu yasiyo na mshiko ya huyu mr maendeleo.

acha kuongea kama kasuku,baadhi uliyotaja apo juu yapo mahakamani,na kama yapo mahakamanni,ww ulitaka jk akamuamuru akimu awafunge kabla ya kesi? maana waongea tu kama mwehu
 
kwanini tugombane Mwenyeezi Mungu anasema hivi

Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. (Al-Baqara: 62)

so kwanini tugombane kwa tofauti ya dini wakati wote malipo ni mamoja kama tukitenda mema

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. (Al-Mumtahana: 8)

ukiangalia kwa undani hapa wakristo waliamua kuchinja kwa imani yao wala hawakutaka mabishano au vita yeyote ndugu watanzania wenzangu hakuna Dini inayoweza kukubaliana na kitendo kilichotokea cha kukosa ustaarabu ulosababishwa na kauli ya serikali iliyoingilia mambo ya kidini badala ya kusimamia katiba ya nchi kuroa kauli kuwa waislamu wana haki ya kuchinja kwa serikali isiyofuata dini ndio chanzo cha yote. Niungane na watanzania wenzangu kuwatakia afya njema waliojeruhiwa na tusitumie dini kama sumu katika fikra zetu bali tutumie dini kama mfumo wa maisha katika jamii na kujenga jamii bora iliyostaarabika yenye amani na upendo kwani dini zote zinafundisha upendo
 
zama za Danieli na wakina meshak Jina la YESU lilikuwa bado halijakabiziwa kwa wanadamu, lakini tangu enzi za yohane mbatizaji mbaka sasa tumepewa jina lipitalo majina yote Jina YESU kwalo kila kicho dhaifu na kichafu kitatakaswa hata tukila vitu vya kufisha havitatuzuru,by the way sikatai kusema wao kwa iamni yao kuchinja ni ibada yaweza kuwa hivyo tambua hata nafaka na vyakula vingine vingi tunavyokula asilimia kubwa vimeunganishwa na ibada za miungu mingine ila kwa kuzitakasa na kubariki basi twaondoa roho chafu na kuweka afya na utakaso wake MUNGU WETU WA KWEKLI.lakini dhamira ikikusuta usule basi na usile.

JS wewe unakuwa kama hujui maandiko! katazo la kutokula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu liko kitabu cha Mdo yaani ni wakati huu wa agano jipya. je Paulo alipomwambia Timoth atumie maji kidogo kwa ajiri ya tumbo lake jina la YESU halikuwepo? usiwe na iman za kipuuzi.
 
Mimi nadhani kuwa na raisi kama Kikwete ndio fedheha kubwa kwa taifa letu.

May be next time tusichague RAIS mwenye 'Pass degree' maana watu wanaograduate na level hii vyuoni ni wachache sana na kwa kweli huwa hawajiwezi kimasomo na ktk kufikiri pia!
 
Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wajilindao. (Al-Baqara: 177)
 
Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka. (An-Nahl: 90)
Na wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa na mayatima na masikini, wapeni katika hayo mali ya urithi, na semeni nao maneno mema. (An-Nisaa: 8)
Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa. (Ar-Room: 38)
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. (Fussilat: 34) Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. (Al-Baqara: 215)
Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wachamngu. (Al-Baqara: 180)
Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. (An-Nisaa: 92)
 
Anasema hivyo akiwa jukwaani lakini akiwa msikitini na ndugu zake wanashangilia na kufurahia mauaji hayo na kuwahamasisha wenzake waendelee kufanya hivyo kwa ahadi ya kuwalinda. Lakini siku zao zinahesabika.
 
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni. (An-Nisaa: 1)


Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda. (An-Nisaa: 135)

Enyi mlio amini! Yanapo mfikia mauti mmoja wenu na akataka kutoa wasia, basi wawepo mashahidi wawili miongoni mwenu ambao ni waadilifu. Na mnapo kuwa safarini, na msiba wa mauti ukakusibuni, basi washuhudie wengineo wawili wasio kuwa katika nyinyi. Mtawazuia wawili hao baada ya Sala na waape kwa Mwenyezi Mungu, mkitilia shaka, wakisema: Hatutopokea thamani yoyote kwa haya hata kwa ajili ya jamaa; na wala hatutaficha ushahidi wa Mwenyezi Mungu; hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye dhambi. (Al-Maaida: 106)

Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri, (An-Nisaa: 36)
(hapa haikusemwa jirani mkristo Muislam au mpagani au mpita njia mkristo mpagani au muislam) ndio maana nasema dini zote zinaeneza upendo
 
so why tunagombana kwanini tugombane kwa sababu ya maustadhi na maustaadhati wachungaji na viongozi wa dini na wa serikali uchwara wanaotupa sumu kwenye fikra zetu kwa mgongo wa dini badala ya kufuata upendo aliotufundisha M.Mungu
 
Daahh hv tukila nyma c tunaend chooni sasa kwanini tupiganie mambo ya nnya?
 
Huyu ndiye mchochezi mkubwa na kauli zake hizi ambazo huzisahau pindi amalizapo kuzitoa.
Kwanini asimsahihishe Waziri wake (Wasira) aliyeletekeza yote haya kwa kauli za kichonganishi?
Kwanini asitibu chanzo cha tatizo?kweli kauli hii itaondoa chuki iliyojengeka baina ya dini hizi?
Inachukiza sana,tuibadilisheni Tanzania yetu kwa kuwaondoa viongozi wasiofaa kama kikwete.
 
Kuwasaka na kuwapa adhabu siyo kuondoa tatizo, kwa maoni yangu inabidi kuangalia chanzo au mzizi wa hili tatizo ni nini? Baada ya kujua mzizi wa tatizo tuuondoe. Kwa upande mwingine tatizo linafahamika ni CCM kupandikiza chuki za kidini kwa propaganda zao (CUFf-chama cha waislam na CHADEMA-chama cha wakristo), tusipo ondoa mzizi wa tatizo madhara yake ni makubwa zaidi ya haya ya mauaji ya mchungaji huko geita. Haya rais JK anza kampeni ya kuondoa mbegu ya chuki uliyoipanda.
raisi jakaya mrisho kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa cc jk alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.
 
Katika hili watanzania wenzangu tusikubari kuburuzwa na mtu yeyote! Tusimame kama taifa moja, ndugu moja na familia moja

Tanzanians of same blood are separated by foreigners' religions.
 
Back
Top Bottom