JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
5,597
Reaction score
1,016
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.
 
Kugombania kuanza kuchinja wanyama ni fedheha maana miaka yote hii nani alikuwa ana chinja na mambo mbona yalikuwa yanaenda bila shida, na kupigana sababu ya kuchinja ni fedheha na kuuana sababu ya kuchinja ndio kabisaa. Udini unaoendeshwa na watu wasiojua dini tusiuvumbie macho! Utatuharibia Taifa letu.
 
Raisi Jakaya mrisho Kikwete amesema mauwaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani gaita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa cc Jk alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Anakimbia kivuli chake huyo!!!!!
 
Inasikitisha sana kuona haya yanaanza na kuendelea kutokea nchini mwetu
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Kwa kweli huyu baba kabalikiwa, kwa kauli tamu zenye kila aina ya matumaini, subiri sasa danadana zake kwenye utekelezaji!
 
Kugombania kuanza kuchinja wanyama ni fedheha maana miaka yote hii nani alikuwa ana chinja na mambo mbona yalikuwa yanaenda bila shida, na kupigana sababu ya kuchinja ni fedheha na kuuana sababu ya kuchinja ndio kabisaa. Udini unaoendeshwa na watu wasiojua dini tusiuvumbie macho! Utatuharibia Taifa letu.

unaonaje kama saa hizi waislam wakaanza kula vilivyochinjwa na wa kristu, kwa sababu wao wamechinja kwa muda mrefu?Hapo itakua ni kupokezana kijiti.
 
Katika hili watanzania wenzangu tusikubari kuburuzwa na mtu yeyote! Tusimame kama taifa moja, ndugu moja na familia moja . Watanzania tumechangamana sana, hakuna familia au ukoo usiokuwa na waislam au wakristo au kuoleana au ujirani na urafiki pia. Hili suala tusikubari hata siku moja litugawe, ndugu zangu wanaJF nmekuwa nikiangalia post mbali mbali hapa zikipostiwa cha ajabu watu wengine wanaangalia ubinafsi zaidi kuliko kuangalia utaifa. Kwa hili hebu ndugu zangu tujaribu kuangalia wadogo zetu, watoto wetu, baba zetu, mama zetu, babu zetu, bibi zetu nk nk. Si busara kushabikia mauwaji eti tu tunashabikia dini zetu, hebu suara la imani zetu libakie kwetu kama sisi na imani zetu tusikwazane kwa masuala ya imani ndugu zangu. Viongozi wa dini mbali mbali, viongozi wa kada mbali mbali tafadharini kama ni tunalipenda taifa letu kwa dhati tuhubiri kutokomeza mauaji haya na kwa umoja wetu bila kuangalia itikadi zetu tulaani kwa pamoja mauaji haya yasipate kurudia tena. Imani yangu ni kwamba hakua sehemu kwenye quran au biblia inaporuhusu kuchinjana! Narudia tena ndugu zangu hapa tulipofikia tuseme kwa pamoja kuwa inatosha na tusikubari kamwe kutumiwa na watu wanaotafuta umaarufu aidha kidini au kisiasa! Si utamaduni wetu watanzania huu.

Asanteni na samahani kwa kuchukua muda wenu.
 
Hivi wale waliomuua Padri kule zanzibari walishakamatwa?
Na wale waliomtesa Docta Ulimboka vipi wamekamatwa?
Je waliochoma makanisa hivi walikamatwa!, na kama walikamatwa wamechukuliwa hatua gani?
Je waliochoma makanisa mbagala hivi walikamatwa! Na je walichukuliwa hatua gani?
Ukweli unabaki pale pale serikali iko nyuma ya waislamu wanafanya haya matuukio! Na tumeshazoea matamko yanayotolewa na Jk mara nyingi yanakosa mshiko ni yakawaida sana.
Hatuoni akichukizwa na hivi vitendo vinavyoshamira sana wakati huu wa serikali yake,
hatuoni kiongozi anaeweza kuongea wananchi wakamsikia!
Amekua akiogopapa upande mwingine watamfikiriaje!.
Nakumbuka mwalimu Nyerere alikuwa hang'ati na kupuliza ila jk anang'ata na kupuliza..
Amekuwa akimtumia waziri DHAIFU wasira kwenda kusuluhisha wa kristo na waislam kule geita! Matokeo yake tumeyaona.
Tusubiri tuendelee kusikia matamko thaifu yasiyo na mshiko ya huyu mr maendeleo.
 
Kwani yeye aliwatuma wakamuue!!Si wameamua wenyewe na akili zao zilivowatuma
Nasikia ni janja ya ccm ili kupooza suala la gasi ili watu wa mtwara kwa kuwa wengi ni waislam wakisikia mchungaji kauwawa basi roho zao zitakuwa zimetulia! Huku bomba likichimbiwa fasta fasta! Hii ni taarifa ya siri.
 
unaonaje kama saa hizi waislam wakaanza kula vilivyochinjwa na wa kristu, kwa sababu wao wamechinja kwa muda mrefu?Hapo itakua ni kupokezana kijiti.

Ili tupate nini sasa? Do we understand well the christianity teachings in the holy bible? Kuacha kuchinja...is it something too much to allow? Kuacha malumbano kwenye issue kama hizo kunatugharimu nini? Hatuna mambo muhimu ya kufanya tuanze kugombania kuchinja wanyama?
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Mimi nadhani kuwa na raisi kama Kikwete ndio fedheha kubwa kwa taifa letu.
 
Fujo za Mbagala nilimsikia Rais akisema Aliyekojolea kuraani kakosea na aliyechoma makanisa kakosea - Rais alishindwa kumjua mkosaji na kumkemea. Akaamua kuwa Neutral.

Jana kuhusu mauaji ya Buseresere, Rais anasema wananchi wa imani tofauti wajenge kuvumiliana. Again hamjui nani anayestahili kukemewa. Akaamua kuwa Neutral.

Hivi kweli kauli hizi zinasaidia kitu? zinaweza kuzuia yaliyotokea yasitokee tena? Hivi kweli katika matukio haya Rais hajui nani anastahili kukemewa kulingana na katiba iliyopo?

Rais anamuoneaje aibu mhalifu na kunutralize issues kijuujuu. Rais unaposhindwa kutetea haki za kundi lililoonewa wananchi wanakujudge kuwa unabelong katika kundi la wachokozi/wahalifu. Haiwezekani ukawa neutral kama kiongozi asiyejua anachopaswa kukisimamia katika jamii anayoiongoza.

Mfano katika issue ya Buseresere ni nani alitakiwa amvumilie mwenzie? kwa nini Rais anatoa statements zinazotuacha hewani?
 
unaonaje kama saa hizi waislam wakaanza kula vilivyochinjwa na wa kristu, kwa sababu wao wamechinja kwa muda mrefu?Hapo itakua ni kupokezana kijiti.

Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.
 
Hilo ni tamko tu sio jawabu la tatizo walilokoleza yeye na makamba wake ili arejee ikulu.MBONA HIYO NGOMA MIE NINAIONA BADO MBICHI,kwani chama dhaifu hakina nia ya kulimaliza.KWAO NI DILI.
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.
nitakula nyama nitakayonunua buchani sijiulizi wala cjali nani kachinja nitaitakasa kwa jina lipitalo majina yote na kuibariki kama itakuwa na mafungamano ya ibada za yoyote isiyo ya mungu ninayemuamini basi kwa jina YESU itatakaswa, tuache malumbano am,bayo kimsingi ni uhaba wa imani
 
Nimekuwa
nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa
na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu
mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi
iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa
uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi
tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila
tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye
familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji
ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na
ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao
zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam
mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya
biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake.
lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo
kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha
ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara,
mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu
atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni
mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu
mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha
kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema,
muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono
yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.
Nina mashaka na ukristo wako
 
Huu unaitwa ukosefu wa akili na busara,miaka yote tumeishi kwa amani leo tugombane na kuchinjana sababu ya kuchinja wanyama,ni nani wa Ishmael na ni nani wa Isack,hayo ndiyo yanawapiganisha wapalestina na waisrael mpaka leo,mwanzo wa jambo siku zote huwa mdogo,njiti ndogo huwasha msitu mnene,
 
Back
Top Bottom