Jiulize haya ili uweze kufanya maamuzi haraka na ujipunguzie mzigo wa mawazo (stress)

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Maamuzi ndio yanachagua tufanye nini, tufanye nini na maisha yetu, au tufanye nini na wapenzi wetu. Ili kufanya maamuzi kwanza inabidi kujiuliza;

~ Ni kitu gani nataka?
~ Kitanifanya nijisikiaje?
~ Je, kitanisaidia kusonga mbele?
~ Ni kitu gani ningependa kitokee?

Ukishajipatia majibu ya hayo maswali utaanza kuona mwanga wa maamuzi unayotaka kuyachukua. Kama ni kumfata mwanamke unayemtaka kumtongoza, majibu yatakua hivi:

~ Nataka niwe naye nione kama atanifaa.
~Nitajisikia furaha kuwa na mwenza wangu pembeni.
~ Inabidi nimpe nafasi nijue kama atanifaa, ninampa nafasi kwa kumfata na kumtongoza. Ningependa nipate wa kuendana naye na tujenge maisha pamoja.

Hapo unapata nguvu ya kwenda kumfata, na mzigo wa mawazo kwamba utakataliwa au utachekwa na mashosti zake utaondoka. Maana hata akikataa kuwa na wewe utapata jibu la swali la pili kwamba, hawezi kukusaidia kusonga mbele kwenye maisha yako.

Jibu ambalo usingeweza kulipata kama usingefikia uamuzi wa kumfata, na kwenye maisha pia maamuzi ndo kila kitu. Itaamua uishie wapi, uwe na furaha/ huzuni, uishi utakavyo au la, uonewe au uwe na amani na kila mtu.

Maamuzi yatakupunguzia mawazo yasiyo na msingi. Mara nyingi ukiona unateseka na mawazo ujue ni kwa sababu hujafanya maamuzi kwa muda mrefu.

Wazo likikujia linataka ulifanyie kitu. Ukiyalimbikiza na yenyewe yanazidi kukujaa. Hata kikombe kilichojaa hakiwezi kujazwa tena, na kichwa chako hivo hivo, ukipata wazo lifanyie kazi, lifanyie maamuzi haraka.
Ili kupata nafasi ya mawazo mengine kuja.

Pia kadri unavyofanya maamuzi ndivyo unazidi kujinoa kuwa kiongozi bora. Ukiona mahusiano yako yanayumba, anza kuangalia je, unafanyaga maamuzi au huwa unaenda na kile mwanamke anakileta/ anakianzisha?

Tahadhari

Kufanya maamuzi kuna faida na hasara. Kuna matokeo mazuri na mabaya. Kuna maumivu na furaha. Kama vile ilivyo siku, ina usiku na mchana, na maamuzi pia yana pande mbili, lakini usiangalie upande mmoja, angalia faida ya kiujumla/ ya muda mrefu (miaka 10 mbele hivi).

Namaanisha, kuna maamuzi utayafanya sasa, lakini yatakuumiza mno, utatamani usingeyafanya. Lakini yana faida miaka kadhaa ijayo.

Kama vile kumkanya mkeo, kwa muda mfupi unaweza kuona kama unamuumiza mkeo anaweza kukununia kabisa, lakini faida yake muda mrefu ni kwamba atakuheshimu na kukupenda zaidi.

Hivyo, ukipata matokeo mabaya ya maamuzi, jikumbushe faida kubwa ya hayo maamuzi.
Na kama ulikosea, usijitukane/ kujiumiza, tambua kuwa sisi si wakamilifu tunafanya makosa. Alafu fanya maamuzi upya.

Nikutakie wiki njema na ufanye maamuzi bora sio bora maamuzi.
 
Nimeipenda saaaana hii ushauri mzuri asante sana
 
Back
Top Bottom