Msongo wa mawazo unaoletwa na misukumo ya fikra kwenye jamii zinazotuzunguka

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,143
32,889
Habari za mida hii ndugu jamaa na marafiki.

Sote tunaishi kwenye jamii...jamii ambayo imejaa watu wenye mitazamo, maoni na utashi tofauti tofauti.

Katika ya jamii hiyo ambayo tupo kunazaliwa viwango vya kimaisha na vigezo mbali mbali kwa mitazamo yao na kufanywa kuwa ndio vipimo na matarajio ya mambo yanavyotakiwa kuwa.

Kwa uchache nitaainisha baadhi ya mitazamo iliyozaa sifa na vigezo vilivyowekwa kama mizani kwenye jamii vinavyozalisha msongo wa mawazo na hata kujidhuru kama sio kujimaliza kwa wanajamii hasa vijana.

1)Kigezo kuwa hadi kufikia umri fulani uwe umeshapiga hatua fulani maishani.
-Kila mwenye akili timamu anaelewa na kutambua kizungumkuti cha maisha na changamoto zake...kwa kifupi maisha hayatabiriki na yana matukio mengi ya kushangaza kama sio kustaajabisha.

Ni shauku ya kila mmoja kuweka mambo yake sawa na kufikia mafanikio aliyojipangia, ikitokezea mambo kuwa kinyume huzaliwa sononeko....sio kutokana na hali ya maisha bali kutokana na namna jamii itamtazama kutokana na vigezo vilivyowekwa na wanajamii....kukomaa kwa hali hiyo huzaliwa msongo mkubwa wa mawazo na kujitoa thamani na kama asipopata msaada kimawazo anaweza kujitoa Uhai.

2)Kigezo kuwa hadi kufikia umri fulani uwe umeshaoa au kuolewa na kuwa na watoto.

-Bahati mbaya jamii imeweka Kigezo hiki cha kikatili pasi na kutaka kujua kinachoendelea kwenye mioyo au maisha ya watu hao, vijana wanaoonekana kuvuka umri elekezi huonekana kichanganyikiwa na wengine kuokota hata watu wasiofaa ili tu kuendana na vigezo vya wanajamii matokeo yake ni kuishi kwenye magereza yanayoitwa ndoa kwa kukosekana Kwa furaha baada ya kujua kuwa chaguo haikuwa sahihi. Hupelekea matatizo ya kiuchumi yanayopelekea kuvunjika kwa familia changa zilizoanzishwa kwa mipango ya kimsukumo wa kijamii. Pia Hali hii imezaa majuto vilio kwa vijana walioamua kufanya maamuzi Kwa kufuata mkumbo.

3)Kigezo kuwa hela ndio kila kitu na kama huna hela basi si kitu.
- Sasa hivi kila ukipitia habari au post inayoonyesha ufahari imekuwa kawaida kukuta kibwagizo cha kutafuta hela.

Hakika pesa inachukua sehemu kubwa ya maisha yetu lakini msukumo mkubwa kwenye hilo imepelekea vijana kujiingiza kwenye njia haramu kujipatia hela na matokeo wamejikuta majuto makuu ili Tu kuendana na msukumo wa kwenye jamii.

Nawasilisha
Wengine mtaongezea.
 
Back
Top Bottom