Acha kuwa mtu mzuri muda wote hakuna utengano wa maamuzi ya moyo na akili

Nov 2, 2023
60
50
Kila mtu anapenda kutenda uzuri kwenye kila kitu cha kumuhusu mwenyewe au watu wengine hasa anaowapenda asiopenda wahisi vibaya. Muda mwingi tunashungulisha akili zetu kufikiria matendo yapi yatakuwa mazuri kwetu ili tusijihisi vibaya. Muda mwingi tunaacha kuwa makini na kilichopo mbele yetu na kujiwazia kwanza sisi hali yetu itakuwaje au ya utae mtendea maamuzi fulani.

Tumefikia kutenganisha akili zetu kwenye uzuri na ubaya kwenye kila kitu na kuchukia kuwa upande wa ubaya. Ila kwaukweli huwa kuna tendo moja tu linalo hitajika bila kufikiria sana. Tumukuwa watumwa sana kwenye picha za nafsi zetu tunazozitengeneza kimawazo akilini mwetu. Muda mwingi tupo makini na picha ya tunavyojichukulia kimawazo na kuiweka kwenye kila kitu iwe inatutafsiri na kuamua kutokana na picha yetu ya kimawazo tujilinde tusiiumize kujihisi vibaya.

Tunaenda mbali hatutaki kuona ukweli wowote ule halisia mbele yetu ila tunataka picha yetu ya tunavyojijua kimawazo ibaki salama huu ni utumwa wa njozi. Vitu halisi vinatupita mbele yetu kuwamakini navyo ila tukipata tu kitu kinachotupa raha ya kujiona salama tunasahau kila kitu cha muhimu kinachotuhusu zaidi. Inatupelekea kuangukia kwenye ulimwengu wa kimawazo na hisia kupambania kupata faraja bila kujali chochote kuhusu ukweli wa nafsi zetu na chanzo cha tamaa zetu.

Kitu cha muhimu kujua huwa hakuna maamuzi yakusikiliza moyo wala kufikiri katika kutenda jambo. Kila utachofikiria picha yake lazima ihusishe hisia na inategemea mfumo wako wa usalama ulivyojiweka akilini mwako kutafsi hicho kitu. Ukisema utenge vitu kwa kufanya kwa hisia vingine kwa kufikiri lazima utaishia kujilaumu. Na ukitaka utende mema unayotafsiri usijiumize wala usimumize mwingine lazima kunasehemu utamua visivyotakiwa ili tu kuwe na hisia za usalama na hili si sawa.

Katika matendo yako hakuna kitu muhimu kama ufahamu wako na si hisia wala kufikiria tu. Na kama kufikiria kutakuja kutokana na ufahamu si kwa ubinafasi wako kuwako kati ya matendo lazima hutopata jibu sahihi. Unahitaji ufahamu ulio huru kwenye mawazo yako, unaweza kuona uhalisia wote bila kukupendelea nafsi yako au mwingine yoyote na hapo unaweza kutenda kambo kwa uhalisia wake kama lilivyo. Lakini kwenye maiaha yetu tumekuwa watumwa sana kwenye mawazo yetu kibinafsi nakuupa ufahamu wetu nafasi ndogo sana katika maamuzi yetu.

Tunahitajika kuwa makini na kwa utulivu wetu kuweza kuuinua ufahamu wetu kuweza kuwa huru kwenye akili zetu. Ufahamu ukiwa ni macho na masikio yako bila mawazo kati yake basi utaona uhalisia wa kila kitu cha mbele yako na maamuzi yatakuja kimatendo kwa jinsi ulivyoelewa jambo bila kujali hisia zake kwako wala kwa mtu mwingine. Na hapo utapata jibu sahihi lisilokuwa na upendeleo kwako wala kwa mtu mwingine. Na hutokuwa na majuto wala shaka kwakuwa hujatenda kujifurahisha ila inavyotakiwa kuwa.

Nb: Ufahamu utakuoelekea kuelewa na kufikiri pekee kutakupelekea kudhibiti bila uhalisia. Kutegemea hisia gani utakuwa nayo kwenye kutenda jambo au kulifikiria kibinafsi hutoweza kupata jibu kamili linalotakiwa katika uhalisia wa jambo hilo. Kama ni unatakiwa uumie ni lazima uumie usikwepe ndio njia sahihi kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom