Madwari Madwari
JF-Expert Member
- Sep 16, 2014
- 1,185
- 2,077
Vijana wasome wapate GPA kubwa lakiniwasibaki chuoni kufundisha. Maana kuwa lecturer kutamfubaz akili. Hili ni mtazamo wanguHabari wanajamvi,
Inabidi tuzungumze uhalisia wanajamvi matokeo ya wanafunzi wengi wa vyuo wa miaka ya hivi karibuni yamekua duni ukilinganisha na vizazi vilivyopita vya miaka 90s,80s,70s, GPA kuanzia 3.8 ni za kutafuta na tochi vyuoni haswa haswa vyuo vya umma
Moja ya sababu ni kumekua na kasumba kwa wanafunzi wa vyuoni kwamba hata kama upate GPA nzuri kuanzia 3.8 haina maana kivyovyote kama hauna connection utabakia jobless milele, na unakuta kabisa kuna baadhi ya wanafunzi wanawajisifia kwa wanafunzi wenzao kwamba wewe soma tu sana na GPA yako nzuri lakini hutoboi mimi mjomba angu ni mwasibu TRA.
Shwain unakuta mjomba mwenyewe wa jamaa ni mwasibu wa kawaida tu kijana anajiharibia future yake akidhania kwamba mjomba wake ambae ni mwasibu wa kawaida TRA pengine wa ngazi ya chini anaeza mpa ajira.
Kiuhalisia nchi yetu connection zipo kwa zaidi kwa watoto wa vigogo kama mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na viongozi wengine wa ngazi ya juu nje na hapo kijana tafuta GPA na ishi na watu vizuri, Na vile vile kuna baadhi ya watu wametusua kupata ajira chap kutokana na GPA zao kua safi bila connection yoyote.