Hali ya wanafunzi wengi wa vyuo kupunguza bidii katika masomo

Eloy Joel

Member
Aug 30, 2023
7
11
Kumekuwa na Situation ya wanafunzi wengi walio vyuoni kupunguza nguvu ya kusoma kwa bidii, Wanafunzi wengi wamekuwa wakijichanganya sana mtaani kwa shughuri za kuingiza japo pesa kidogo (Mishe Mishe).

Kwa Upande wangu naweza sema, Changamoto ya Ajira wanayo ishuhudia ndio inawakosesha nguvu ya kusoma kwa bidii.

Wengi wana dada zao wengine kaka zao waliosoma na kugraduate vizuri sana Lakini wanawashuhudia wakiteseka na Maisha.

Hii situation inaanza sasa kuharibu mind set ya wanafunzi japo Kuwa tokea awali walikuwa wakisoma kwa malengo Yani toka Shule za msingi, O level, Advance etc.

Wanachokifanya wanafunzi sasa ni kuanza kuzoea Mtaani kabla ya Kugraduate ili pengine isije Kuwa Tabu sana kwao, So automatically mwanafunzi huyo anajikuta tuu hana matokeo mazuri sana chuoni.

Serikali pamoja na wadau wengi waelimu waliosoma wamekazana kusema wanafunzi wapate kuanzia GPA flani za juu kidogo Lakini Pasipo kutazama kiundani zaidi nini wanafunzi wanapitia Miaka hii ya karibuni kwa kushuhudia waliowatangulia bado wanahangaika na walipata Hizo GPA zinazo tajwa.

Sijui Unaweza Sema kitu gani Wewe kama Mtanzania na Mwenye Uchungu wa Maisha na Mwenye kutamani Vijana wajikwamue na swala la Umasikini?
 
Hatuwezi kufanana.

Mfanya biashara ni tofauti na muajiriwa na wote wanategemeana maana hakuna anayeweza kujimudu mwenyewe.

Kuhusu suala la GPA nawashauri wapate kubwa maana hamna mtu ajuaye kesho yake. Unawweza idharau lakini itakuuma kweli kama mwenzako mwenye nayo akiajiriwa mapema kisa hiyo GPA nzuri.

Watie bidii masomoni maana ndo kilichowapeleka chuoni vingine vitakaa sawa huko mbele kwa mbele
 
Kumekuwa na Situation ya wanafunzi wengi walio vyuoni kupunguza nguvu ya kusoma kwa bidii, Wanafunzi wengi wamekuwa wakijichanganya sana mtaani kwa shughuri za kuingiza japo pesa kidogo (Mishe Mishe).

Kwa Upande wangu naweza sema, Changamoto ya Ajira wanayo ishuhudia ndio inawakosesha nguvu ya kusoma kwa bidii.

Wengi wana dada zao wengine kaka zao waliosoma na kugraduate vizuri sana Lakini wanawashuhudia wakiteseka na Maisha.

Hii situation inaanza sasa kuharibu mind set ya wanafunzi japo Kuwa tokea awali walikuwa wakisoma kwa malengo Yani toka Shule za msingi, O level, Advance etc.

Wanachokifanya wanafunzi sasa ni kuanza kuzoea Mtaani kabla ya Kugraduate ili pengine isije Kuwa Tabu sana kwao, So automatically mwanafunzi huyo anajikuta tuu hana matokeo mazuri sana chuoni.

Serikali pamoja na wadau wengi waelimu waliosoma wamekazana kusema wanafunzi wapate kuanzia GPA flani za juu kidogo Lakini Pasipo kutazama kiundani zaidi nini wanafunzi wanapitia Miaka hii ya karibuni kwa kushuhudia waliowatangulia bado wanahangaika na walipata Hizo GPA zinazo tajwa.

Sijui Unaweza Sema kitu gani Wewe kama Mtanzania na Mwenye Uchungu wa Maisha na Mwenye kutamani Vijana wajikwamue na swala la Umasikini?
Vijana mtaani wamekata tamaa sa ivi wanasoma basi ijulikane tu na yeye alipita University
 
Back
Top Bottom