Jinsi kauli ya hauna connection na GPA haina maana inavyosababisha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kuwa na matokeo duni vyuoni

Dogo12

Member
Oct 5, 2022
45
140
Habari wanajamvi,

Inabidi tuzungumze uhalisia wanajamvi matokeo ya wanafunzi wengi wa vyuo wa miaka ya hivi karibuni yamekua duni ukilinganisha na vizazi vilivyopita vya miaka 90s,80s,70s, GPA kuanzia 3.8 ni za kutafuta na tochi vyuoni haswa haswa vyuo vya umma

Moja ya sababu ni kumekua na kasumba kwa wanafunzi wa vyuoni kwamba hata kama upate GPA nzuri kuanzia 3.8 haina maana kivyovyote kama hauna connection utabakia jobless milele, na unakuta kabisa kuna baadhi ya wanafunzi wanawajisifia kwa wanafunzi wenzao kwamba wewe soma tu sana na GPA yako nzuri lakini hutoboi mimi mjomba angu ni mwasibu TRA.

Shwain unakuta mjomba mwenyewe wa jamaa ni mwasibu wa kawaida tu kijana anajiharibia future yake akidhania kwamba mjomba wake ambae ni mwasibu wa kawaida TRA pengine wa ngazi ya chini anaeza mpa ajira.

Kiuhalisia nchi yetu connection zipo kwa zaidi kwa watoto wa vigogo kama mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na viongozi wengine wa ngazi ya juu nje na hapo kijana tafuta GPA na ishi na watu vizuri, Na vile vile kuna baadhi ya watu wametusua kupata ajira chap kutokana na GPA zao kua safi bila connection yoyote.
 
Vijana someni! Tumia common sense kuwa nimekuja hapa chuo kufanya nini kama sio kusoma? Na isiwe kusoma tu bali kufaulu! Na sio kufaulu tu bali kufaulu kwa viwango vya juu GPA kuanzia 4.0 hadi 5.0. Kwa mwanafunzi anayejitambua atazingatia hili vinginevyo utajutia muda na fursa uliyoipoteza
 
Shida ya vijana wa sikuizi ndugu ujinga mwingi wanaenda chuo kula bata na kujiita wafanyabiashara mwisho wa siku kuishia kupata gentlemen GPA ata interview kuitwa hautwiti
 
Huko vyuoni Kuna matatizo mengi sana zaidi ya ulichosema, lakini kinachosumbua na kuharibu elimu ya Tanzania ni sexual marks.pamoja na malecture kuwa na vinyongo kwa kuwatengenezea wanafunzi GPA za kuku ili wasifike mbali kielimu na hata kuwazidi kimafanikio.
 
Well said.. unajua kuna baadhi ya kozi mpaka watoe 4.0 ni kimbembe unakuta mwanafunzi bora wa hiyo kwa mwaka husika kozi ata 3.8 hajafika sometimes departments katika vyuo vikuu vinaona sifa kufelisha ili waonekane wanatoa watu nondo
 
Elimu ya Tanzania inaupumbavu mwingi sana, yaani hata ukitofautiana kidogo tu na lecture, unapigwa tukio hata la kufelishwa kabisa.
 
Kuna baadhi ya fani kupata hizo Gentleman GPA sio kwamba wanapenda ni mazingira tu.

Mfano, tuliosoma Engineering kupata Lower Second Class ni mafanikio makubwa.

Maana Walimu wenyewe wanasema kwenye darasa la wanafunzi 100 basi angependa kuona watakao graduate hawafiki 50.

Huoni hizo Lower Second class ni zaidi ya First class 🤗

Ila connection pia ni muhimu kuwa nayo, kuna watu walipata first class wakaishia kufundisha huku waliopata Second Class wakiishia kufanya kazi kwenye Makampuni makubwa yanayolipa vizuri.
 
Back
Top Bottom