Wanafunzi wa vyuo wanaosomeshwa na Baraza la wafugaji (Ngorongoro) wadai hawajilipiwa ada na mahitaji mengine

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
138
229
Baadhi ya wanafunzi kutoka jamii ya kimasai, Wilaya ya Ngorongoro wanaosomeshwa na Baraza la wafugaji chini ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanadai kumekuwepo na kusuasua kwa malipo ya ada na mahitaji mengine kwa wanufaika waliopo kwenye vyuo mbalimbali nchini.
IMG-20240520-WA0004.jpg

Hayo yameelezwa leo Mei 20, 2023 kwenye tamko la Vijana kutoka jamii ya kimasai kutokea Wilaya ya Ngorongoro ambalo linaeleza kwamba kumekuwepo na changamoto nyingi kwenye malipo ya Wanafunzi wanaosomeshwa na Baraza hilo, wakitolea mfano kuwa kati ya Wanafunzi 154 ambao walipitishwa mwaka 2023 kufadhiliwa katika masomo yao karibia robo tatu hawajalipiwa ada kama ilivyopaswa kuwa.

"Pamoja na mambo mengine kumekua na changamoto kubwa ya ulipaji wa ada na pesa za matumizi kwa wanafunzi wanaosomeshwa na baraza la wafugaji chini ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,mwaka jana baraza la wafugaji kupitia kamati yake tendaji ilipitisha wanafunzi 154 na kati yao wanafunzi 55 pekee ndio wanasadikika kulipiwa ada hasa wa vyuo vya kati wengine wote waliobaki 99(55 vyuo vya kati na 44 vyuo vikuu) hawajalipiwa ada wala kupewa matumizi"

Tamko hilo linaeleza, kwamba suala hilo halijatimizwa licha ya kupewa barua na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ya kupokelewa vyuoni na kutambuliwa kama wafadhiliwa wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Ambapo vijana hao wamehoji uwezekano uliopelekea NCAA kutoa barua za kupokelewa kwa wanafunzi hao ingali bajeti yao ilikua hairuhusu.

Hata hivyo vijana ambao wamekuwa katika mpango wa ufadhili huo wamedai kuwa kutopatiwa stahiki hizo mapema ikiwemo ada na pesa ya matumizi ipelekea changamoto mbalimbali hususani kwa mabinti kukosa mahitaji muhimu.

Aidha wamedai kuwa awali malipo yalikuwa yakitoka kwa wakati lakini kwa sasa mchakato umekuwa wa kusuasua ambao unawanyima wengi kupata haki ya elimu katika mazingira rafiki.

Licha ya hivyo wamehusianisha jambo hilo na zoezi la wananchi wa Ngorongoro 'kuhama kwa hiari' ambalo limekuwa likiendelea kwa siku za hivi karibuni.Wanadai kuwa uenda suala hilo linatokea hili kuwashikiza Wananchi kuhama.

Kufuatia suala hilo wametoa wito kwa mamlaka husika hususani Serikali kusimamia suala hilo kuhakikisha changamoto hizo zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili kuepusha athari zaidi zinazotokana na wanafunzi hao kupata mahitaji muhimu.

Pia tamko hilo ambalo limetolewa na vijana nawaliojitambulisha kwamba 'wawakilishi vijana kutoka jamii ya kimasai Wilaya ya Ngorongoro' wamitaka jamii kupuuza kundi linalojitambulisha kama wao na kufanya 'propaganda' za kudai kuwa wananufaika na huduma, pamoja na kuwashawishi baadhi ya wakazi wa ngongoro kuhama.

Itakumbukwa Serikali imekuwa ikieleza kuwa suala la kuhamisha wananchi Ngorongoro ni zoezi linaloendeshwa kwa hiari bila shinikizo, lakini pia Serikali imekuwa ikikana baadhi ya madai ya kusitishwa kwa baadhi huduma kwa wakazi wa maeneo husika kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.
 
Back
Top Bottom