Jinsi kauli ya hauna connection na GPA haina maana inavyosababisha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kuwa na matokeo duni vyuoni

Habari wanajamvi,

Inabidi tuzungumze uhalisia wanajamvi matokeo ya wanafunzi wengi wa vyuo wa miaka ya hivi karibuni yamekua duni ukilinganisha na vizazi vilivyopita vya miaka 90s,80s,70s, GPA kuanzia 3.8 ni za kutafuta na tochi vyuoni haswa haswa vyuo vya umma

Moja ya sababu ni kumekua na kasumba kwa wanafunzi wa vyuoni kwamba hata kama upate GPA nzuri kuanzia 3.8 haina maana kivyovyote kama hauna connection utabakia jobless milele, na unakuta kabisa kuna baadhi ya wanafunzi wanawajisifia kwa wanafunzi wenzao kwamba wewe soma tu sana na GPA yako nzuri lakini hutoboi mimi mjomba angu ni mwasibu TRA.

Shwain unakuta mjomba mwenyewe wa jamaa ni mwasibu wa kawaida tu kijana anajiharibia future yake akidhania kwamba mjomba wake ambae ni mwasibu wa kawaida TRA pengine wa ngazi ya chini anaeza mpa ajira.

Kiuhalisia nchi yetu connection zipo kwa zaidi kwa watoto wa vigogo kama mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na viongozi wengine wa ngazi ya juu nje na hapo kijana tafuta GPA na ishi na watu vizuri, Na vile vile kuna baadhi ya watu wametusua kupata ajira chap kutokana na GPA zao kua safi bila connection yoyote.
Vijana wasome wapate GPA kubwa lakiniwasibaki chuoni kufundisha. Maana kuwa lecturer kutamfubaz akili. Hili ni mtazamo wangu
 
Hata tabia ya kuteua watu bila kufanya vetting ya kipengele cha maadili mema na historia ya mwenendo mwema inaharibu sana vizazi vya Taifa hili,

Vijana wanaona kuwa hata ukiwa mhuni unaweza kuteuliwa Kuwa kiongozi maana haiangaliwi hiyo.

Lakini wakijua inaangaliwa wangeambaiana ku-behave well.
 
Umeongelea upande mmoja, je viwango vya ufundishaji huko chuoni vipo vile vile, kila mwaka vyuo vinaongeza idadi ya wanafunzi je huko chuoni kuna walimu wa kutosha ? vitendea kazi vya kutosha, maabara , vitabu n.k ? Wahadhiri wenyewe ndio hao hao wanapambana na maisha kufanya biashara nje ya taaluma yao ili kusogeza siku mbele, tunategemea hao vijana wafaulu kweli ?
Miaka ya nyuma ukisika mtu ni mwanachuo anakuwa na uwezo kweli kweli wakuchanganua mambo, kuna baadhi ya vyuo hata hao wahadhiri wakifungua kinywa unajiuliza huyu aliwezaje hata kutetea huo utafiti wake uliopelekea kupata shahada ya juu. Elimu inachezewa acha vijana waruke amapiano
 
Tulipitia huko na first class tukapata!
Screenshot_20231005-205210.jpg
 
Yaaani asipo chakarika kutafuta hela , hato pata hela ya kulipia expenses so wengine wana engage in moneying
 
Je ! Kwa akili ya kawaida ni kweli BOT wote Wana GPA ya 4.....? Japo walio nazo wapo Kama sista hapo Ila connection ni muhim tusizembee
 
Back
Top Bottom