Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

ADii
for real inaudhi kwa kweli watu tunapinga huu uovu mana ni kuwakosea heshima mke uliyemuoa kwa kiapo.

Ni kuikosea heshima jamii,watoto,familia n.k

Na pia unyanyasaji kwa wanawake then unakuja hapa unakuta wanawake hao hao wanashangilia huu ufedhuli.

Watoto wengi wanaishi mitaani baada wazaz wao kutengana/kufa kwa ukimwi chanzo ni nyumba ndogo.
Jamii inateketea na kuteseka kwa hili balaa kwa kweli hawa wanawake wanaoshangilia hili jambo hawana Huruma na always wanawake mtabaki kukandamizwa mana ninyi wenyewe hampendani.

Nani aliahidi hapa... Nitakupenda, nitakulinda, nitakuheshimu na "nikiacha wengine woote, nitabaki na wewe tu"...
Kwa hiyo unagundua kwamba source siyo nyumba ndogo, source ni hao wajenzi wa nyumba ndogo (kama alivyosema Asha)

Wewe Mpatanishi, anza kuwaambia wenzio waache... Mimi siwezi kuja kupiga hodi nyumbani kwako eti nasaka mwanaume...

Unyanyasaji..... sijaelewa unamaanisha nini hapo.... watu kupendana ni kunyanyasana... hata hivyo kuna bondage love pia, wewe ukiona mateso mwenzio kwake starehe

Does that mean nyumba ndogo ndo zina maghala ya ukimwi?
 
...marhabhaa darlingtone....nauma nikipuliza,....ukweli wauma, wape tahfifu wenzio bana,
nakuogopea utachukiwa kama da sophy 'kadogoo' wangu wee...!

Hapo ndo tunapokosea kaka Mbu, tunapotaka kuondoa tatizo lazima tulitambue, tulikubali then tutafute namna ya kuliondoa
lakini tukipingana na ukweli then tukigeuza mgongo tunafanya the same, haitusaidii
 
...lol....haya bana,...ila namna ya kuuondoa mfumo huu mnhhhh....i doubt!
haya, mjadala mwema mamie...
 
Kweli mama umelonga sana. Nakuunga mkono kwa asilimia 100. Ila napenda kutoa angalizo kwako na kwa akina dada na akina mama wengine. Wanapoona waume zao wanaenda nje waanze kwanza kuangalia ni mazingira yapi yamefanya mume wake aende nje. Nikiwa na maana wajiangalie kwanza wao kabla ya kuhukumu. Hizi ndoa mnazoziona jamani zina siri nyingi sana. NAWASILISHA

Siku kadhaa zilizo pita kuna member alitoa post kuhusu utaratibu wa ku-manage nyumba ndogo ili asi lete utata. Member huyo anaitwa The Boss.
Pamoja na kumshukuru kwa kutoa maoni na shauri zake kuhusu Nyumba ndogo, mimi kama mwanamke nimeona siwezi kujibu kwenye post lile ila nifungue tu thread mpya sababu mtazamo wangu na wake ni tofauti kabisa.
  1. Kwanza namlaumu kwa kutoa thread kama hiyo sababu ina halalisha kitu kilicho haram. nikijieleza kwa mfano, ni kama kusema inakatazwa kuua mtu ila kama utaamua kumchinja kumbuka kutoa carpet usilijaze damu. Mtasema hana influence ya kuhalalisha au kuharamisha kitu, na ni kweli, ila yeye ndie alitoa mwelekeo wa thread na kila alie changia kwa kumsupport (na kila alie “like” thread yake) ameongeza sauti lake kwenye mada na hivo msomaji wa kawaida (mimi na wewe) tunahisi kuna watu wengi sana wanamtazamo huo. Kwa mtu alie kua na nia ya kwenda nje, au Yule tayari anatembea nje ya ndoa, ni ruhsa tosha ya kuendelea katika njia hiyo.
  2. Pili, kama ikitokea mtu aanguke na atoke nje ya ndoa, shauri la kumpa sio namna gani aifanya hali hiyo iwe shwari na idumu, bali nikumshauri namna gani anaweza kujitoa katika mtego huo. maada ya thread hii sio kutoa huo ushauri, labda nitarudi baadae.
  3. La tatu na lililo nikwaza zaidi ni heshima ndogo ya utaratibu mzima kwa wanawake, iwe nyumba kubwa au nyumba ndogo. Kwa namna nilisoma thread (kama nilikosea naomba anikosoe) kila kitu kina husisha kugawa hela kati ya nyumba kubwa na nyumba ndogo (material distribution) na heshima/mtazamo wa ndugu na rafiki. sikuona katika thread hiyo mapenzi yanawekwa wapi, heshima ya muhusika kwa nyumba kubwa, au nyumba ndogo, watoto, tegemeo za watu wengine na kadhalika vikija katika hesabu.
Katika dunia ya JF, ni sawa kuanzisha thread kama hiyo ila dunia ya kweli ambayo ninaishi mimi, na wengine wengi, hivyo vitu vipo. Mtu anaheshima yake na akienda kwa nyumba ndogo conscience yake inamsumbua. kuna mapenzi kati ya yeye na nyumba kubwa, au kati ya yeye na nyumba ndogo, au yuko in transition, akitoa mapenzi kwa bimkubwa kwenda kwa nyumba ndogo(or whatever the case). Pia wanawake hao ni binadamu na wana akili, tumaini, na hisia zote za kawaida. wanapiga hesabu za maisha na kusema kesho nataka mimi na mpenzi wangu tuwe hivi, na hivi, na hivi. na wanatumia njia mbali mbali za kumshawishi mwanaume afate hizo njia.
Kwa kumalizia nataka kukumbusha kama kila mtu ana mtazamo wake wa haya mambo na nina heshimu mtazamo wa kila mtu. Huu hapa ni mtazamo wangu na naomba uheshimiwe pia. Sijakataza kutoa maoni yenye kupinga mtazamo, nimeomba tu tuchangie kwa heshima.
Asanteni.
 
Nani aliahidi hapa... Nitakupenda, nitakulinda, nitakuheshimu na "nikiacha wengine woote, nitabaki na wewe tu"...
Kwa hiyo unagundua kwamba source siyo nyumba ndogo, source ni hao wajenzi wa nyumba ndogo (kama alivyosema Asha)

Wewe Mpatanishi, anza kuwaambia wenzio waache... Mimi siwezi kuja kupiga hodi nyumbani kwako eti nasaka mwanaume...

Unyanyasaji..... sijaelewa unamaanisha nini hapo.... watu kupendana ni kunyanyasana... hata hivyo kuna bondage love pia, wewe ukiona mateso mwenzio kwake starehe

Does that mean nyumba ndogo ndo zina maghala ya ukimwi?

Sikiliza darlingtone
hata mm nakubali wanaume tuna makosa makubwa tena sana tu ingawa nakiri sijaoa bado ila kamwe siwezi kukubali mtazamo wako kuwa nyumba ndogo ziwepo tu.

Nyumba ndogo ninyi ni hatari na balaa kubwa kwa jamii yetu hii.

Ni ni nyinyi nyumba ndogo mnaofanya wanaume waache wake zao huku watoto wakiteseka na kutanga tanga mitaani.

Familia ngapi zilizokua strong i.e kipato n.k zimetengana/kuparaganyika na watoto kuishi kwa tabu,kukosa haki yao ya kusoma n.k

Narudia tena ninyi ni watu hatari sana ktk mustakabali wa kujenga jamii imara iliyostaarabika.

Always nyumba ndogo hutaka ku WIN mapenz pia hapo ndio hufanya ndoa za watu kutetereka.

Nimewahi kukuuliza hapo mwanzo je ww kama mwanamke ikitokea unaolewa je utakubali na kufurah mwanamke mwingine akuibie mumeo?

Abt nyumba ndogo kuwa maghala ya ukimwi YES.
Nyumba ndogo nyingi husambaza virusi kwa ndoa za watu mana mwanaume anaekuhudumia,kukupangia nyumba n.k na kukufanya nyumba ndogo yake uwezekano wa kutumia kinga na ww haupo.

Then wanawake wengi nyumba ndogo hawaridhiki na huyo mwanaume tu wanaemuiba mana kuna muda wanamkosa so huwa wanakua na spare nyingine pembeni kufidia ule muda ambao mume anakua kwa mkewe.

Nimesikitika sana ww kushabikia UOVU unaoufanya. MUNGU akusamehe
 
.......Pia wanawake hao ni binadamu na wana akili, tumaini, na hisia zote za kawaida. wanapiga hesabu za maisha na kusema kesho nataka mimi na mpenzi wangu tuwe hivi, na hivi, na hivi. na wanatumia njia mbali mbali za kumshawishi mwanaume afate hizo njia.
......

RussianRoulette,

Naona watu wengi wametoa michango mbalimbali (inayokinzana) lakini kwa ujumla nikitizama sana naona hakuna hoja mpya zinazotolewa. Sasa inabidi "uchanganye na zako"((kama JK alivyowahi kusema!). Sina hakika kama wewe ni muumimi wa kusoma vitabu lakini kama ni hivyo nimeattach kitabu ("Mambo Ambayo Wanaume Hawataki Wanawake Wajue - Siri, Uongo, Ukweli Usiosemwa"...kimeandikwa na Smith na Doe) unaweza kukisoma kama utapa muda........naamini utapata mawili-matatu (but again subject to your beliefs, experiences etc). Pamoja na mambo mengine kitabu hiki kinatoa ushauri kwa kina mama/dada juu ya namna ya "kudhibiti" waume zao. Kitabu hiki kwa mara ya kwanza kiliwekwa hapa JF na "Robot" (kama kumbukumbu zangu zipo sahihi).
 
Attachments

Sikiliza darlingtone
hata mm nakubali wanaume tuna makosa makubwa tena sana tu ingawa nakiri sijaoa bado ila kamwe siwezi kukubali mtazamo wako kuwa nyumba ndogo ziwepo tu.

Nyumba ndogo ninyi ni hatari na balaa kubwa kwa jamii yetu hii.

Ni ni nyinyi nyumba ndogo mnaofanya wanaume waache wake zao huku watoto wakiteseka na kutanga tanga mitaani.

Familia ngapi zilizokua strong i.e kipato n.k zimetengana/kuparaganyika na watoto kuishi kwa tabu,kukosa haki yao ya kusoma n.k

Narudia tena ninyi ni watu hatari sana ktk mustakabali wa kujenga jamii imara iliyostaarabika.

Always nyumba ndogo hutaka ku WIN mapenz pia hapo ndio hufanya ndoa za watu kutetereka.

Nimewahi kukuuliza hapo mwanzo je ww kama mwanamke ikitokea unaolewa je utakubali na kufurah mwanamke mwingine akuibie mumeo?

Abt nyumba ndogo kuwa maghala ya ukimwi YES.
Nyumba ndogo nyingi husambaza virusi kwa ndoa za watu mana mwanaume anaekuhudumia,kukupangia nyumba n.k na kukufanya nyumba ndogo yake uwezekano wa kutumia kinga na ww haupo.

Then wanawake wengi nyumba ndogo hawaridhiki na huyo mwanaume tu wanaemuiba mana kuna muda wanamkosa so huwa wanakua na spare nyingine pembeni kufidia ule muda ambao mume anakua kwa mkewe.

Nimesikitika sana ww kushabikia UOVU unaoufanya. MUNGU akusamehe

This leads u men back to The Boss's thread... mmeshapewa guidance, kwa nini wewe mwanaume uchukue nyundo uvunje nyumba yako...
Nenda Kamsome tena The Boss... Kisha ukioa, tumia hizo guidance, U r no an angel...

And... asante kwa Maombi, kwa hiyo nimesamehewa na ninaweze kuanza upya... si ndio?
 
RussianRoulette,

Naona watu wengi wametoa michango mbalimbali (inayokinzana) lakini kwa ujumla nikitizama sana naona hakuna hoja mpya zinazotolewa. Sasa inabidi "uchanganye na zako"((kama JK alivyowahi kusema!). Sina hakika kama wewe ni muumimi wa kusoma vitabu lakini kama ni hivyo nimeattach kitabu ("Mambo Ambayo Wanaume Hawataki Wanawake Wajue - Siri, Uongo, Ukweli Usiosemwa"...kimeandikwa na Smith na Doe) unaweza kukisoma kama utapa muda........naamini utapata mawili-matatu (but again subject to your beliefs, experiences etc). Pamoja na mambo mengine kitabu hiki kinatoa ushauri kwa kina mama/dada juu ya namna ya "kudhibiti" waume zao. Kitabu hiki kwa mara ya kwanza kiliwekwa hapa JF na "Robot" (kama kumbukumbu zangu zipo sahihi).

"Smith and Doe wish to acknowledge Salman Rushdie, who with each passing day proves that you can write the truth and live to cash the check"
 
Gademu!

Yaani kwenda kuzimua mara moja huu msredi umekimbia namna hii?

Baada ya kusema hayo, mie ODM kwa mamlaka niliyopewa na PAW napenda kuwatunuku wapambanaji wafuatao udaktari wa falsafa wa heshima kwa mchango wao mkubwa katika sekta nyeti ya ndanganyifu a.k.a cheating na ujengaji wa nyumba ndogo lakini imara na za kisasa
1. Centre Forward Sarafina1
2. Right Winger Darlington
3. Full back right Ram

Pia nawatunukia nishani ya upambanaji usiokatishwa tamaa kwa maaskari wa nchi kavu
1. Sajenti Roulete wa Urusi
2. Meja AshaDii
3. Kapteni Nyumba kubwa
4. Koplo Kbd

Baada ya kuwatunuku nawasihi tuendelee na mpambano. Mie kazi yangu kubwa ni kugonga vi-LIKES tu!
Mungu awabariki sana!
 
This leads u men back to The Boss's thread... mmeshapewa guidance, kwa nini wewe mwanaume uchukue nyundo uvunje nyumba yako...
Nenda Kamsome tena The Boss... Kisha ukioa, tumia hizo guidance, U r no an angel...

And... asante kwa Maombi, kwa hiyo nimesamehewa na ninaweze kuanza upya... si ndio?

mimi nimepingana na The Boss tangu huko kwenye thread yake. Then elewa kwamba hapa siangalii guidance eti tu cheat responsibly wala nini hapa napinga huo uovu wa nyuma ndogo 100% na hii ni wajibu sisi kama jamii tukatae uovu wa mustakabali mwema wa jamii yetu.

It seems ww ulikubali kuchezewa na vidume enzi zako sasa muda wako wa kuwa on market umesha upoteza thus y unaona fair tu kuiba mume wa mtu tena kutamba hapa hadharani huku ukileta na mlologo wa hoja kutetea. All in all naeza kusema upo psychological affected.

Hapa naangalia tatizo angle zote, nimeanza kuwasema wake wenyewe wenye ndoa zao.

Sasa nimehamia kwenu waizi/nyumba ndogo then namalizia kwa wanaume wenye tamaa wanaokosa nidhamu na heshima kwa ndoa zao.

Darlingtone sidhani kama ww utafurahi watoto wa huyo mume unae muiba wakose shule,waishi kwa kuomba omba mitaani, kama utafurahi hayo basi wewe ni zaidi ya Shetani.
 
Gademu!

Yaani kwenda kuzimua mara moja huu msredi umekimbia namna hii?

Baada ya kusema hayo, mie ODM kwa mamlaka niliyopewa na PAW napenda kuwatunuku wapambanaji wafuatao udaktari wa falsafa wa heshima kwa mchango wao mkubwa katika sekta nyeti ya ndanganyifu a.k.a cheating na ujengaji wa nyumba ndogo lakini imara na za kisasa
1. Centre Forward Sarafina1
2. Right Winger Darlington
3. Full back right Ram

Pia nawatunukia nishani ya upambanaji usiokatishwa tamaa kwa maaskari wa nchi kavu
1. Sajenti Roulete wa Urusi
2. Meja AshaDii
3. Kapteni Nyumba kubwa
4. Koplo Kbd

Baada ya kuwatunuku nawasihi tuendelee na mpambano. Mie kazi yangu kubwa ni kugonga vi-LIKES tu!
Mungu awabariki sana!

Hehehe afazali fellow tablet umehuzuria. Nazani soon nitakuachia shift, maana hii sredi bila uangalizi wa kipharmacy inaweza ikapoteza mwelekeo kabisa yaani.
 
Nyumbani kwangu i am the law,nitatoka saa nnataka,nitaingia saa nnataka,what i do in between is my business.You live only once bana. Na huyo mwanamke atakayetaka kushindana na mimi kwanza huo ubavu ataupata wapi,subutu yake........We unalala pazuri,unakula vizuri,i gave a nice car,watoto nawalipia shule nzuri,wazazi wako nawahudumia kama wa kwangu,saluni unakwenda ya Sea cliff sasa kelele ya nini? Tell me why the longolongo????

Hahahaaaa imebidi nicheke kwa sauti wewe Bishanga sio mzima jamani......wenzio wako kwenye serious discussion! Kwahiyo unafikiri mwanamke anataka hayo tu????na mapenzi pia anyataka jamani kama mlivyokua mnaanza mwanzoni kabisa anayataka yale yale yaliyowafanya muoane.
 
"Smith and Doe wish to acknowledge Salman Rushdie, who with each passing day proves that you can write the truth and live to cash the check"

Yeah....hawa jamaa 'wamepinda' sana!

.....But if you are are a person who needs to know the facts, who wants to live in real world and solve real problems, who is not afraid to look at the underside of men and deal with them as they are, this book will tell you everything you ever need to know.
 
Mimi ni muhanga wa nyumba ndogo.
Mwanaume hata ufanye mazuri mangapi bado atakuwa na nyumba ndogo tu.
Hata mngonoke kila siku bado atakuwa na nyumba ndogo tu.
sijui ni nani aliyewalaani.
 
It seems ww ulikubali kuchezewa na vidume enzi zako sasa muda wako wa kuwa on market umesha upoteza thus y unaona fair tu kuiba mume wa mtu tena kutamba hapa hadharani huku ukileta na mlologo wa hoja kutetea. All in all naeza kusema upo psychological affected.

Punguza jazba....

Ukishasema mtu "kakubali" ina maana haoni tatizo... labda ndio maisha aliyoamua kuishi... na je? unajuaje kama yeye ndo anawachezea hao vidume.... "Why keep a cow if you only need a single sausage"

Sitambi mpatanishi, naeleza ukweli... Ni kitu ambacho kipo, kinafanyika na kitaendelea kuwepo... as long as wanaume na wanawake wanaishi... labda dunia iangamie...

Sasa nimehamia kwenu waizi/nyumba ndogo then namalizia kwa wanaume wenye tamaa wanaokosa nidhamu na heshima kwa ndoa zao..

Nakutakia kila la kheri kwenye kampaign zako... ila kumbuka wao ndo wanajiiba wenyewe...
They have time and resources za kujenga hizo nyumba.... we are just being cooperative...lol

Darlingtone sidhani kama ww utafurahi watoto wa huyo mume unae muiba wakose shule,waishi kwa kuomba omba mitaani, kama utafurahi hayo basi wewe ni zaidi ya Shetani.

Sasa ndo nakushauri kabla hujaenda kujenga hako kajumba kako kadogo (siku ukioa), uangalie kwanza hiyo nyumba unajenga masaki au manzese... ina facilities gani, n.k - "Changanya na za kwako"
 
Nina amini bado wapo wanaume ambao hawatoki nje ya ndoa zao, wapo tu naomba Mungu sana nikutane na mmoja wao

Tuendelee kujipa moyo Sara lakini kwa experience yangu mmhhh.........kuna utata hapo! Mimi natamani kweli ningemuona hata mmoja ambae hatoki nje sina maana nyumba ndogo maana tukisema nyumba ndogo ni kuwa ameihalalisha kiaina(kwa washkaji zake na baadhi ya ndugu). Sijui kama nimeeleweka hapo.
 
Hujaitendea haki thread ya the Boss. Kwa sababu msingi wa thread yako ni maoni ya Boss kuhusu nyumba ndogo ni vyema ukaiweka hapa ili watu waone alichosema na wewe ulichosema kisha wachambue mchele na pumba.
 
Back
Top Bottom