Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jibu kwa The Boss (Nyumba ndogo)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Roulette, Oct 17, 2011.

 1. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siku kadhaa zilizo pita kuna member alitoa post kuhusu utaratibu wa ku-manage nyumba ndogo ili asi lete utata. Member huyo anaitwa The Boss.
  Pamoja na kumshukuru kwa kutoa maoni na shauri zake kuhusu Nyumba ndogo, mimi kama mwanamke nimeona siwezi kujibu kwenye post lile ila nifungue tu thread mpya sababu mtazamo wangu na wake ni tofauti kabisa.
  1. Kwanza namlaumu kwa kutoa thread kama hiyo sababu ina halalisha kitu kilicho haram. nikijieleza kwa mfano, ni kama kusema inakatazwa kuua mtu ila kama utaamua kumchinja kumbuka kutoa carpet usilijaze damu. Mtasema hana influence ya kuhalalisha au kuharamisha kitu, na ni kweli, ila yeye ndie alitoa mwelekeo wa thread na kila alie changia kwa kumsupport (na kila alie “like” thread yake) ameongeza sauti lake kwenye mada na hivo msomaji wa kawaida (mimi na wewe) tunahisi kuna watu wengi sana wanamtazamo huo. Kwa mtu alie kua na nia ya kwenda nje, au Yule tayari anatembea nje ya ndoa, ni ruhsa tosha ya kuendelea katika njia hiyo.
  2. Pili, kama ikitokea mtu aanguke na atoke nje ya ndoa, shauri la kumpa sio namna gani aifanya hali hiyo iwe shwari na idumu, bali nikumshauri namna gani anaweza kujitoa katika mtego huo. maada ya thread hii sio kutoa huo ushauri, labda nitarudi baadae.
  3. La tatu na lililo nikwaza zaidi ni heshima ndogo ya utaratibu mzima kwa wanawake, iwe nyumba kubwa au nyumba ndogo. Kwa namna nilisoma thread (kama nilikosea naomba anikosoe) kila kitu kina husisha kugawa hela kati ya nyumba kubwa na nyumba ndogo (material distribution) na heshima/mtazamo wa ndugu na rafiki. sikuona katika thread hiyo mapenzi yanawekwa wapi, heshima ya muhusika kwa nyumba kubwa, au nyumba ndogo, watoto, tegemeo za watu wengine na kadhalika vikija katika hesabu.
  Katika dunia ya JF, ni sawa kuanzisha thread kama hiyo ila dunia ya kweli ambayo ninaishi mimi, na wengine wengi, hivyo vitu vipo. Mtu anaheshima yake na akienda kwa nyumba ndogo conscience yake inamsumbua. kuna mapenzi kati ya yeye na nyumba kubwa, au kati ya yeye na nyumba ndogo, au yuko in transition, akitoa mapenzi kwa bimkubwa kwenda kwa nyumba ndogo(or whatever the case). Pia wanawake hao ni binadamu na wana akili, tumaini, na hisia zote za kawaida. wanapiga hesabu za maisha na kusema kesho nataka mimi na mpenzi wangu tuwe hivi, na hivi, na hivi. na wanatumia njia mbali mbali za kumshawishi mwanaume afate hizo njia.
  Kwa kumalizia nataka kukumbusha kama kila mtu ana mtazamo wake wa haya mambo na nina heshimu mtazamo wa kila mtu. Huu hapa ni mtazamo wangu na naomba uheshimiwe pia. Sijakataza kutoa maoni yenye kupinga mtazamo, nimeomba tu tuchangie kwa heshima.
  Asanteni.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,254
  Trophy Points: 280
  Wanawake bwana......
  Mna vidumu, viserengeti boi, vipochi, lakini hamsemi.
  Nyie mnajua sana kuficha madhambi yenu, hata ukifumaniwa mkono mwekundu (red handed) unajikataa unasema sio mimi , mi ni pacha wake.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  RR

  Hata ulalame vipi

  Nyumba ndogo / cheating / infidelity haikwepeki!
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wengi tunao wajua na tusio wajua hawana nyumba ndogo. Na hata kama mtu anae, ushauri wa kumpa ni namna gani anaweza kuachana na tabia hiyo.
  Hivi unadhani ushauri wa the boss unasaidia nini zaidi ya kukupa confidence ya kufanya ujinga? The Boss kasema as if mwanaume yuko in charge, in control of the situation ila ukitazama katika maisha ya kila siku hana control yoyote. anafanya maamuzi kutokana na influence ya wanawake hao, na vitu vingine vingi ambavyo hawezi control.
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Roulette... Umeniwahi for nipo kuandika a Counter thread kuhusiana na Nyumba ndogo... On a Serious note.... Hilo hata Boss mwenyewe nimem-forwadia pamoja na Mwenyekiti wao (Darling Kaizer) Hamna lilillohaibika thou... Tutajion tu hizo forces.... ila kwa vigezo kua inabidi tukuabali kua Ndio reality na sasa tufanye vipi hawa wa kaka/baba wajue kua hatupendi na kamba tukiamua tunaweza tumia grader zetu ikabaki vumbi tu... Kigezo kikubwa kwanza ni kukubali... then we ATTACK!!!

  I feel where it is coming from for I am a woman tu... twaweza ongea kwa mzaha, twaweza kubali kua ndio ukweli BUT Ukweli unabaki kua inauma.... Hata hivo kuna threads nyingi saana zimeanzishwa za Nymba Ndogo na hii jamii ya MMU ina wanawake na wanaume... BUT Sidhani kama kuna thread isha wahi funguliwa kupinga ama kutoa msimamo wa sie wanawake tunafaikiria vipi (My thread imelenga hivo pia) Hivo basi Roullette nakupongeza kwa hii thread na nimefurahi....
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Shem hapa issue nafikiri sio kulalama tu... Nafikiri tatizo ni ile promotion i.e ilotolewa na Boss pamoja na zenu zoote na Sweetie pia...
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Haaaaaa,babu hujui bibi anapitaga humu?
   
 8. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Huku kuandika kwa msisitizo na ukali kunaonyesha kwamba wewe una ndoa changa. Ngoja ipate umri kwanza ndiyo utajifunza mengi.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Duh napita tuu jama hapa hicho kismall house sijawa nacho na wala sitamani kuingia humo maana hii nyumba kubwa yenyewe ni msisitizo
   
 10. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133

  Inakwepeka ukiamua babu, wacha kumuumiza bibi kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu.
   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nkushukuru RR kwali nimefarijika kwa sred yako,japo najua wababa/wakaka wataishambulia sana ila msg send and delivered!
   
 12. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  me nadhan thr boss yupo sahii kabisa kama imeshaonekana ni ngumu watu kusubiri hadi ndo a ndo wafanye mapenzi basi atleast tuwaelimishe kujikinga kwa kutumia kondomu wasijepata maradhi na kadhalika....sasa wewe russian ukubali kabisa kwamba nyumba ndogo haziepukiki zilikwepo na zitaendelea kuwepo suala liwe ni namna gan ya kuzicontrol nyumba ndogo zisijeleta matata ,madhara kwa maza house original (mshikwa popote original)....
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We babu nawe...haikwepeki kwa nani???Wanaojihusisha nayo au wanaofanyiwa hayo?

  RR...you are right!!
  Mada kama ile inafanya watu wazidi kuona kwamba nyumba ndogo ni sifa/ni muhimu and worth maintaining.
  Hata kama ni kweli kwamba imekua sehemu ya maisha ya kileo sio sahihi kuipromote ili izidi kupanda chati.
   
 14. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  RR,

  Ni msimamo mzuri wa kuchukia infidelity na nikuunge mkono katika hilo. However wengi humu ukiangalia vizuri ni majeruhi wa tabia hizo. Ni kweli bandiko la Boss liliwalenga zaidi wanaume. Mie nilivyomwelewa Boss ni sawa na ule ushauri wanaoutumia wale wanaopambana na virusi vya ukimwi. Kuwa ingekuwa vizuri kila mtu akawa na mpenzi mmoja mwaminifu na si vizuri kufanya fanya ngono zisizo responsible! Lakini wanamalizia na msemo kuwa - ukishindwa tumia KONDOM.

  Sote twajua evil nature ya nyumba ndogo! However, wapo ambao tunaweza kusema kwenda kwao nyumba ndogo ni justifiable kutokana na kile wanachokumbana nacho huko nyumbani. Au to put it simple, sababu za kwenda nyumba ndogo aside, ukienda zingatia yafuatayo!

  Sioni ubaya wowote katika hilo. Kuna wengi (hasa wanaume) wanachangia kwa ushabiki tu na nature ya wanaume iko hivyo (Angalia ni wengi sana kwenye viwanja vya mpira) yaani ni washabiki. Wanaume wengi wanasifia vitu ambavyo hawajawahi hata kuvifanya, ila huwa wanapenda wengi kujulikana misimamo yao!

  The fact kwamba wewe ume-leta upande wako kama mwanamke, haina maana unawawakilisha wanawake wote! Ni mawazo yako tu. Wapo wanawake wengi sana walioko kwenye kapu hilo; hizo nyumba ndogo zenyewe au wanawake wenye wanaume nje. Ni wengi tu. Ila thread ile ilikuwa muhimu tu kama ilivyo muhimu hii ya kwako!!
   
 15. RR

  RR JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Sijawahi kupinga infidelity ujue....:eyebrows:
   
 16. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama unavo ema hamna kilicho haribika, hii thread ni ya kupinga ile ya Boss ila bado kuna vitu vingi wanaume wanatakiwa kuelewa. Nasubiri thread yako kwa hamu kubwa.
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni huu, japo unauma lakini ndio ukweli wenyewe.

  Tangu kuumbwa kwa dunia hii.......... hakuna kiumbe chochote cha kiume kilichoumbwa kwa ajili ya kiumbe kimoja tu cha kike......!

  Mitume na manabii karibu wote katika vitabu vyote walimiliki si chini ya mke mmoja........ Si ajabu tunaona wanawake wako radhi kuolewa mitala....Laiti wanawake mngekubaliana na hili la kuturuhusu tuoe zaidi ya mke mmoja, labda ndo lingekuwa suluhisho la kuisha hili tatizo. lakini kwakuwa hamtaki, na siye hatujaumbwa kwa ajili ya mke mmoja...........hamna jinsi lazima nyumba ndogo ziendelee ku-ezist.

  Nyie kinamama hamuyaoni hata majogoo mitaani kwenu? Khaa!...........wanaume hawariziki na kikojoleo kimoja, mbona hampendi kutuelewa!
   
 18. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I think walimaanisha RussianRoulette, ambae mimi napinga sana.
   
 19. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #19
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Napata wakati mgumu kuelewa hapa...je ni sahihi kupinga kwa nguvu zote hata jambo ujualo huwezi libadili? Au watakiwa kukubali uhalisia hata kama yauma....
  tafakari...
   
 20. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli sina miaka sana ndani ya ndoa ila naamini iwapo nitazungumza na mume wangu kuhusu mitazamo yetu ya haya mambo na nikamwambia nitakavo hisi kuhusu watu kua na nyumba ndogo mambo yetu yatakua sawa tu. Mbona kuna wengi waliweza?
   
Loading...