Kbd
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,260
- 450
Punguza ukali kidogo basi........... Ila ukweli ni kuwa Nyumba ndogo haziepukiki! Take it from me!
Zinaepukika tena sana kabisa, take it from me!
Hivi nyie na mwenyekiti wenu mnafanya wanawake hawana akili au kitu gani? Hebu tuone mfano huu mdogo............ wewe umeamua kuwa na nyumba ndogo ukiwa na strategies zako na nyumba ndogo naye anajijua yeye ni mwizi na ipo siku nyumba anayokalia inaweza kubomoka hivyo na yeye anastrategies zake pia. We unajiona mjanja na yeye anakuona mjinga na wala hata sikumoja hatakaa kukufikiria wewe na mkeo na watoto wako na especially akuone uko njema kiasi fulani hawezi kukubali kutumika bure hata kidogo. Atafanya juu chini kuhakikisha humuachi.........Wewe ukija na C yeye unamkuta yuko kwenye Z kabisa na mwisho wa siku familia zinasambaratika na watoto wanahangaika mbaya.
Hebu tafakarini hii kitu wababa na kuona kua starehe ya muda yaweza kukuleta shida na ikakukost maisha yako yoooote. Watoto wa mitaani wengi wanatokana na familia kama hizi, baba kaamia kwa kimada na watoto wanahangaika mwisho wanaishia kuwa machokoraa. Jamani ridhikeni na wake zenu, nyumba ndogo ni sumu na kama tulivyosikia sumu haijaribiwi kwa kuionja!! Wacheni ubinafsi wanaume na kujifikiria nyinyi tu....khaaaa!!!
Kwa nguvu zangu zoooote za ndani na za nje na pinga nyumba ndogo