Aspirin, leo niko na wewe...
Sio kweli kwamba mambo lazima yaendelee kua the way yalikua kila siku. Kwanza mwanaume kua na wake wengi sio kawaida ya "kila siku". hata mwanzo kuna wanaume wengi walikua na mke mmoja tu. Tusichukulie mfano wa wayahudi na waarabu kua mfano wetu. Tuna historia yetu sisi kama waafrika. Babu yangu alikua na mke mmoja, baba yangu mke mmoja na mimi mwenyewe nina mume wangu ambae hana mke mngine.
Tukirudi kwa "nyumba ndogo" ambayo ni more ya kujiibia, kama unasema ni kitu kipo na kitaendelea kuwepo, mbona kuna wanaume wameshinda hiyo tabia, na ni wengi sana? Hao wanakua sio wanaume? kwa mtazamo wangu hao ndio wanaume wa kweli, sio hawa wasio kuna na msimamo na hawaheshimu ahadi yao waliotoa mbele ya ndugu, familia, serikali na Mungu.