Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Habari za muda huu jamiiforums
Leo muda kama wa saa 9 alasiri nikiwa ninapitia mambo kadhaa kule Facebook nimekutana na kauli ya Jeshi la Polisi juu ya sherehe za pasaka kwa mwaka huu wa 2021 ambazo zimeangukia katika kipindi ambacho nchi yetu ipo katika maombolezo mazito kufuatia msiba wa shujaa/jemedari wetu mkuu kamanda John Magufuli.
Jeshi letu pendwa la Polisi limesema kuwa halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za sikukuu ya pasaka. Mimi ninakubaliana nao kwa asilimia 100 kutokana na ukweli niliokwisha gusia hapo juu.
Sasa swali linakuja, je Polisi wamewashirikisha viongozi wa dini ya kikirsto (kama vile Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC) kabla ya kutoa tamko hili kwa umma? Vp kama wakristo wakianza kusema wanaingiliwa uhuru wao wa kuabudu?
Ni nani ataweza kuwasisitiza waumini kwa ufanisi zaidi kujiepusha na shamramshamra kama sio viongozi wao wa kiroho? Viongozi wa dini wamekuwa wakishirikiana na vyombo vya usalama katika kukemea vitendo mbalimbali viovu kama vile kula rushwa pamoja na ubakaji, leo kwanini mmeshindwa kuwahuhisha katika hili?
Mnajua ndugu zangu haya masuala ya dini siku zote yanapaswa kushughulikiwa kwa umakini na busara sana. Kama jeshi la Polisi wangeamua kukutana kwanza na viongozi wa dini ya kikirsto na kujadiliana namna bora ya kuhimiza waumini wao kuepuka shamrashamra zisizo za lazima, kisha kupewa media coverage kubwa, hii ngejenga picha nzuri sana kwa jeshi kuwa lina uhusiano mwema na viongozi wa dini nchini.
Polisi ngojea niwaibie siri hii moja, mnapotoa matamko kama haya yanayogusa imani za watu pasipo kuwashirikisha viongozi wao, mnakuwa mnawapa fursa watu wasio na nia njema na taasisi yenu kuanza kuwaundia hoja za kuchafua taswira yenu njema kwa kuanza kusema Polisi sasa wanaingilia uhuru wa baadhi ya watu wa kuabudu.
KUTOKA PAGE YA MILLARD AYO FACEBOOK;
==========
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka zilizozoeleka kipindi cha miaka ya nyuma katika kipindi hiki ambacho Nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
MAONI YANGU INFANTRY SOLDIER;
==========
Jeshi la Polisi nchini limesema linapanga kukutana na viongozi wa dini ili kuona ni namna gani wanaweza kuhimiza waumini wao kuepuka sherehe na shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka zilizozoeleka kipindi cha miaka ya nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.