Jeshi la Polisi Tanzania na tamko lake juu ya sherehe za pasaka April 2021. Je, mmewashirikisha viongozi wa dini husika?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari za muda huu jamiiforums

Leo muda kama wa saa 9 alasiri nikiwa ninapitia mambo kadhaa kule Facebook nimekutana na kauli ya Jeshi la Polisi juu ya sherehe za pasaka kwa mwaka huu wa 2021 ambazo zimeangukia katika kipindi ambacho nchi yetu ipo katika maombolezo mazito kufuatia msiba wa shujaa/jemedari wetu mkuu kamanda John Magufuli.

Jeshi letu pendwa la Polisi limesema kuwa halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za sikukuu ya pasaka. Mimi ninakubaliana nao kwa asilimia 100 kutokana na ukweli niliokwisha gusia hapo juu.

Sasa swali linakuja, je Polisi wamewashirikisha viongozi wa dini ya kikirsto (kama vile Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC) kabla ya kutoa tamko hili kwa umma? Vp kama wakristo wakianza kusema wanaingiliwa uhuru wao wa kuabudu?

Ni nani ataweza kuwasisitiza waumini kwa ufanisi zaidi kujiepusha na shamramshamra kama sio viongozi wao wa kiroho? Viongozi wa dini wamekuwa wakishirikiana na vyombo vya usalama katika kukemea vitendo mbalimbali viovu kama vile kula rushwa pamoja na ubakaji, leo kwanini mmeshindwa kuwahuhisha katika hili?

Mnajua ndugu zangu haya masuala ya dini siku zote yanapaswa kushughulikiwa kwa umakini na busara sana. Kama jeshi la Polisi wangeamua kukutana kwanza na viongozi wa dini ya kikirsto na kujadiliana namna bora ya kuhimiza waumini wao kuepuka shamrashamra zisizo za lazima, kisha kupewa media coverage kubwa, hii ngejenga picha nzuri sana kwa jeshi kuwa lina uhusiano mwema na viongozi wa dini nchini.

Polisi ngojea niwaibie siri hii moja, mnapotoa matamko kama haya yanayogusa imani za watu pasipo kuwashirikisha viongozi wao, mnakuwa mnawapa fursa watu wasio na nia njema na taasisi yenu kuanza kuwaundia hoja za kuchafua taswira yenu njema kwa kuanza kusema Polisi sasa wanaingilia uhuru wa baadhi ya watu wa kuabudu.

KUTOKA PAGE YA MILLARD AYO FACEBOOK;
==========
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka zilizozoeleka kipindi cha miaka ya nyuma katika kipindi hiki ambacho Nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

aswedfgtrfvbghy.jpg


MAONI YANGU INFANTRY SOLDIER;
==========
Jeshi la Polisi nchini limesema linapanga kukutana na viongozi wa dini ili kuona ni namna gani wanaweza kuhimiza waumini wao kuepuka sherehe na shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka zilizozoeleka kipindi cha miaka ya nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hatujashirikisha mtu. Fanya unachotaka tukuvunje hizo kuni.
PROFESSIONALISM: Mnapotoa matamko kama haya yanayogusa imani za watu pasipo kuwashirikisha viongozi wao, mnakuwa mnawapa fursa watu wasio na nia njema kuanza kuwaundia hoja za kuchafua taswira yenu kwa kuanza kusema Polisi sasa wanaingilia uhuru wa watu kuabudu.
 
Katika hili nimeelewa masuala kadhaa ikiwa ni;-

1. Polisi walicholenga ni kitanabaishe kama festival! Yaani sherehe zile zilizokuwa sherehe kweli.

2. Polisi hawakulenga watu kwenda katika ibada, kupiga kengele, kusoma misa kwa sauti na mambo yote ya hivyo.

3. Limekuwapo shinikizo la UVIKO kutoka kwa viongozi wa siasa na wanaharakati fahamika mfano, Bw. Godless Lema, Antipas Lissu, Bi. Maria Sarungi, Ex Mayor Jacob na wengineo walioshinikiza kwa kipindi kirefu kuchukuliwa kwa tahadhari za janga hili hivyo ni hatua zinaanza.

4. Kwa protokali za polisi, hadi msemaji atoke kwa jamii kuzungumza haya kunakuwepo go ahead kutoka kwa kiongozi mkuu wa taasisi hii ambaye ni Bw. IGP Simon Sirro.
 
3. Limekuwapo shinikizo la UVIKO kutoka kwa viongozi wa siasa na wanaharakati fahamika mfano, Bw. Godless Lema, Antipas Lissu, Bi. Maria Sarungi, Ex Mayor Jacob na wengineo walioshinikiza kwa kipindi kirefu kuchukuliwa kwa tahadhari za janga hili hivyo ni hatua zinaanza.
Ni jambo jema kwa case ya COVID-19
 
1. Polisi walicholenga ni kitanabaishe kama festival! Yaani sherehe zile zilizokuwa sherehe kweli.

2. Polisi hawakulenga watu kwenda katika ibada, kupiga kengele, kusoma misa kwa sauti na mambo yote ya hivyo.
Viongozi wa dini watawezaje kuwasisitiza waumini wao juu ya haya yote kama hawajishirikishwa rasmi? Kumbuka tamko la kwenye media sio formal means of communication baina ya taasisi moja na nyingine.
 
PROFESSIONALISM: Mnapotoa matamko kama haya yanayogusa imani za watu pasipo kuwashirikisha viongozi wao, mnakuwa mnawapa fursa watu wasio na nia njema kuanza kuwaundia hoja za kuchafua taswira yenu kwa kuanza kusema Polisi sasa wanaingilia uhuru wa watu kuabudu.
Nasema imani ni kuomboleza kifo cha mtakatifu meko, mambo ya yesu hatuyajui.

Jaribu tukuvunje taya
 
Huyo fortunate ambaye huwa unamtaja kils baada ya kufungua thread ni nani?
Inaonrkana ame join July 2011 lakini hajawahi ku comment, wala ku like wala kufungua uzi.
Na hiyo July, 2011 alipo join ndiyo ilikua last seen yake.
Mkuu, kwa heshima yako uliyonayo humu JF leo ndio mara ya mwisho kumtaja huyu dada. I'll tag her no more.
 
Ni jambo jema kwa case ya COVID-19
Ushauri wangu watu watumie akili na uelewa kuliko mihemko na utumwa wa fikra katika hili. Na ushauri wa ziada kwa polisi ni ZUIO hili liendelee kipindi chote cha UVIKO na kuimalisha hali ya usalama wa taifa na kupambana na ukoloni mamboleo ikiwa ni pamoja na wakati wa Eid el Fitr, Hanukkah, La Posada, Christmas na Happy Diwali.
 
Mkuu, kwa heshima yako niliyonayo humu JF leo ndio mara ya mwisho kumtaja. I'll tag her no more.
Hapana mkuu, kila uzi wako ni lazima niufungue so nimekua na udadis huu kwa muda mrefu kidogo tangu ulipoanza kumtaja. Leo nikajikuta nalazimika kumfuatilia bio yake, then nikauliza ili kujua zaidi.
Ila kwenye comment yako umeonyesha ni wa kike, she must mean something big.
Kukudhihirishia kuwa huwa nakufuatilia, siku hizi umeacha tabia ya kuamkia Wakubwa zako😀😀😀
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom