Sio kweli Kiranga,si swala la emotions,ni ukweli mtupu.Kwani Mkapa hakubinafsisha viwanda vyote na makampuni yetu yaliyokuwa yanafanya vizuri kwa bei ya kutupa ili kuwafurahisha mabeberu.
Mtibwa hakuiuza kwa Sh.600,000,000!NMB haikuwa inafanya vizuri akai-uza?Kiwira Coal Mine hakujigawaia?Madini yetu hakuwapa mabeberu kwa bei ya kutupa mpaka akasema Kasungura kadogo,kinyume chake tunaambiwa leo nchi yetu ni tajiri.Tumegeukaje overnight kutoka kwenye kuwa na Kasungura kadogo na kuwa matajiri?Bandari yetu je,si walikuwa wanapiga tu.Utalii,si walilala tu na kuuza vitalu kiholela nk.nk.
Usitukumbushe machungu Kiranga,au na wewe ni mmoja wao?Ndio yapo machache mazuri aliyofanya,lakini ni kama panya anayeuma na kupuliza.Waliingiza kwa mkono huu,wakachukua kwa mkono mwingine.Wewe acha tu Kiranga,Mkapa sina hamu naye.
Aliingia na gia nzuri sana,lakini akabadilisha gear angani,akaanza kupiga kinyama,sijui Khazarian Mafia Kingpins walimzungmatajiri overnight!Black Magic of Babylonian Talmudism maana they are very good at that.Wewe najua unayajua maloloso Hata sana.Si ndiyo wanayofanyiana wakiwa at the World Economic Forum kumbe ni World Talmudism and Occult Forum!
Raw I'ma give it to ya, with no trivia
Raw like cocaine straight from Bolivia
-Wu Tang Clan "Da Mystery of Chessboxin'"
Disclaimer. This post is unguarded. Straight from the heart. Kama alivyonifundisha Chinga One uwazi. Mpaka leo.
Labda sikuwa wazi.
Nilikusudia kumaanisha kwamba nilitegemea wanaomsema Ulimwengu wangekuja na fact. Mimi nipo kum support Ulimwengu.
Mimi Mkapa nimempinga tangu 1995. Nampinga kijiweni Upanga, nampinga huku mtoto wake akiwa hapo kijiweni. Kwa hivyo, mimi si mtu wa kumtetea Mkapa JF kisiasa.
Mimi Mkapa ni Mzee wangu. I am talking ile kukaa na watoto wa nyumbani kwa Mkapa tukiwa wadogo wananilalamikia Baba yao mnoko sana mezani kwenye chakula haruhusu kunywa maji mpaka mtu amalize chakula. I am talking mtoto wa Mkapa 1995 kuniambia "mmemchagua huyu rais, mama yangu, mtakoma". Mengine mengi sitaki kusema kwa sababu ni ya kifamilia zaidi.
Kwa hiyo huyu ni Mzee wangu. Na kama Mzee wangu, siku zote nitamuhifadhi. Mengi yake mabaya nitayaacha. Kwa sababu he deserves that break. Everybody deserves a break when they die. But, on tye othe r hand, Mkapa is not "everybody". He is "Mr. Mention". Ediror in Chief. Or, Chief censor as Ulimwengu would have it.
Mkapa nilimchukulia kama Mzee tu wa mtaani. Mpaka siku moja nilikumbushwa huyu kashakuwa mtu tofauti, si yule Mzee wa Sea View aliyekuwa anawapa access ya fax machine yake kabla ya email.
Mkapa alitegemewa na nchi miaka mingi sana kabla hajawa rais.
Ukisoma mpasuko wa kisiasa na ugomvi kati ya Nyerere na Kambona leo jina la Mkapa novigumu kuliona. Lakini kiukweli Nyerere alikuwa anaona Kambona ni rafiki yake tu, Mkapa ndiye aliyempa intelligence zote Nyerere mpaka Nyerere akabadili mawazo kuhusu Kambona.
Ukisoma jinsi Henry Kissinger, US Secretary of State, alivyobishana sana na Nyerere, hususan kuhusu uhiru wa Zimbabwe, utajua sana umahiri wa Nyerere,lakini hutakua kwamba umahiri wa Nyerere ulikaa juu ya kigoda cha umahiri wa Mkapa aliyeandika ripoti zote.
Leo nawamiss sana wazee wangu kina Hashim Mbita, Paul Sozigwa,Nsa Kaisi na Philemon Mahiga waliofanya kazi karibu na Mkapa. Maana kawaida ningewapigia simu niongee nao wanioe story zaidi za miaka ya zamani na kazi zao, lakini, bahati mbaya sana, walishatangulia.
Let's recollect the Mkapa years. Mimi nilikuwa a young whippersnapper na control Dar es salaam siku hizo.
Kuna siku nilitoka ofisini mjini, kuna kitu nilikuwa nampelekea mchizi wangu pale kwa Mkapa Sea View. Nilikuwa na drop off something ilikuwa akipate kabla ya jioni muhimu sana.Basi nikamchukua dereva wa ofisini l, alikuwa na some salespeople, katika mizunguko ya mjini, nikamwambia I wanna make a quick stop Sea View (hata sikusema Sea View kwa Mkapa, to me that was irrelevant) five minutes halafu tutaendelea na safari zetu.
Nikaenda mpaka pale nikafanya drop off kwa mchizi wangu. Mimi nilichukulia kitu simple tu kwa sababu mchizi wangu anajua mimi kichaa wake tangu mtu yeyote hajajua Mkapa atakuwa rais. Basi mimi nikaona easy tu. Kesho yake ofisini ikawa bonge la story. Yani wewe Kiranga umeenda nyumbani kwa rais kama unaenda kwenu?
So Mkapa Mzee wangu.If I want to, I can draw a family connection. But I won't. Lakini, kuna mambo alifanya sivyo.
Na mimi najivunia kuwa mtu real, nasema mawazo yangu. Hata kama Mkapa mzee wangu.
Na hata mchizi wangu nilikuwa namwambia, wakati baba yake rais. Yani tunakaa maskani, picha ya baba yake iko juu, namwambia "ondoa picha ya mshua hapa maskani. Mshua wako mnoko tu". Anacheka. Machizi wengine wananiambia acha picha ya Mzee wetu.Na yeye mchizi wangu anajua msimamo wangu. Na, to his credit, aliuheshimu.
Kuna siku polisi walikuja maskani. Tukaona polisi kama 25 hivi wanakuja. Nikawaambia watoto, kama mnaogopa polisi, ondokeni. Ngoma ya watu wazima hii.
Polisi wakafika maskani. Wakaanza zao, nyie mnakaa wapi?
Mchizi mmoja akawawakia. Hivyo ndivyo mnavyosalimia watu? Ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu hivyo?
Wakayeyusha. Halafu wakaanza kurudia swali. Kwa mmoja baada ya mwingine. Wewr unakaa wapi? Wanajibiwa "Hapo". Wewe? Wanajibuwa "hapo". Wakamfikia mchizi. Wewe? Akawajibu "Kwa Ben". Ikabidi Polisi wamshangae kwanza. Wakamuuliza, kwa Ben? Ben gani huyo? Akawajibu "Ben hiyo hiyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani qewe unamjua Ben gani mwingine?
Polisi wakawa kama hawaam8ni hivi.
Mmoja wao akasema "Huyu namjua mtoto wa Mkapa, nimemuona nyumbani pale nilivyokwenda kulinda".
Basi hapo hapo tuka9na wale polisi wamekuwa wadogo wanaanza kama kutuomba msamaha. Wakawa wanasema "Mnajua wazee nibkatika kujuana tu, hakuna ubaya kujuana blah blah". Tukawa tunacheka sana walivyobadil8ka ghafla baada ya kusikia hina la Ben Mkapa.
Hiyo kumbukumbu ya Ben Mkapa siwezi kuisahau maishani nwangu. Ilinionesha unafiki wa polisi wa Bongo. Baada ya hapi polisi waliweka alama kwenye ramani yao kwamba kijiwe hiki msiguse kuna watoto wa rais wanakaa hapa.
Turudi kwenye rambirambi.
Watu wengi wanatoa rambirambi kiutamaduni.
Mimi Mzee wangu (Baba Mzazi) alikuwa serikalini siku hizo, na alimpaka Mkapa kisiasa kwenye ubinafsishaji. Na baada ya speech ya mzee wangu kumpaka Mkapa kwenye ubinafishaji, kesho yake, mtu wa kwanza kumpigia sifa mzee wangu kumsifu kwa kutoa speech ile, alikuwa Magufuli, enzi hizo waziri.
Mkapa namuheshimu sana kwa usomi wake, kwa kuweka taasisi kisheria kuanzia TISS mpaka TRA, kwa kuonesha mfano wa kurudisha seriousness kwenye urais baada ya "ruksa",kwa kurudisha heshima ya Tqnzania kimataifa pale iliposhuka, kwa kuandika mambo na kuweka msisitizo katika usomi.
Lakini, nasimama na Ulimwengu 90% katika aliyoyasema. Pengine kwa sababu namjua zaidi Mzee Mkapa kama Mzee wangu na si rais wa nchi tu.
It's one thing if you just read about Mkapa as the president, and quite another if you see your friend jump at the table of Salender Bridge Police due to home frustrations, you hear him tell escapades of his father's drunken stupors.
Mazee alinipa story kuna siku watu wa usalama walikuja nyumbani Sea View wanamtafuta Mkapa. Hapo Mkapa Waziri wa Mambo ya Nje. Rais Mwinyi. Rais anaenda ziara Saudi Arabia, anaenda na Mkapa. Rais yuko airport, Mkapa hajulikani alipo. Watu wa Usalama wameenda nyumbani Sea View wamemkuta mchizi wangu. Wanamtafuta Waziri. Waziri kashavunja itifaki, alitakiwa kuwa airport anamsubiri rais. Lakini sasa rais yupo airport anamsubiri Waziri.
Usalama wamefika nyumbani Sea View, lakini hawajui Waziri Mkapa yuko wapi.
Mchizi wangu akazama chumbani.
Kuzama kamkuta Mkapa kalewa Scotch Whisky tilalila, mchana kweupee, kalala sakafuni.
Ikabidi mchizi wangu apate shock, alifikiri mshua kaanguka kwa ugonjwa, kumsogelea akasikia harifu ya kinywaji.
Akamwambia kuna watu wa Usalama wanakutafuta wanasema kuna safari.
Ikaitwa helicopter ikamuwahisha airport.
Rais Mwinyi kwa kuwa alimpenda sana Mkapa, kwa kuwa Mkapa alikuwa mchapa kazi mzuri na anajua sana mambo ya diplomasia ya kimataifa na historia ya Tanzania, alifumbia macho makisa kama hayo.
Sasa hiyo story moja tu.
Sitaki kujaza zaidi stories za Nyerere alivyosuluhisha ndoa ya Mkapa kwa kumwambia Mkapa "sisi Wakatoliki hatunabtalaka, ongea na mkeo tumalize tofauti, nchi haina historia ya mtu mwenye talaka Ikulu".
So, mimi namjua Mkapa kama mzee wangu, na ukaribu umenionesha mazuri yake mengi na mabaya yake mengi.
Si mtu wa kumuimbia sifa tu kama vile namsoma magazetini tu.