Je, Yu wapi Dkt. Isaac Ndodi?

Je, Yu wapi Dkt. Isaac Ndodi?

Nimeshawahi onana nae kariakoo anavaa baggy jeans hatari na ka tshirt kanabana hatari

Hivi ni tofauti na huyu rafiki yake Kigwangala aliyepo TBC kila siku akitudanganya? Sheria ya Kigwangala sijui iliishia wapi.
 
haaaahaaaahaaa hapo sasa unachemsha unataka nn kama sio umbea. mwee kama kuliwa tumeliwa sn na ndodi
Hahah kipindi kile sijui hata tulikua na ujinga gani kichwani.

Ila zamani watu walikua wanajua kupiga saundi aiseee,Kuna mzee mnajimu alikua anaitwa Shekhe yahaya Channel 10 aisee nae alikua sio haba kwa Saundi,anakwambia mpnz mtazamaji hebu angalia hio video hapo ni supermarket na hayo unayoyaona hapo ni majini yaliyonaswa na camera za CCTV yakiingia kufanya shopping,hahah.
 
Hafu Hawa kina Dr ndondi waliibuka enzi za kina Jakaya, Mara Dr Rahabu, Mara Dr. Mwaka Yani mtu anajiita Dr na hajaenda kusoma bachelor ya medicine Muhimbili na serikali Ina mchekea tu.
Sasa hv Kuna Dr kumbuka
 
Hivi ni tofauti na huyu rafiki yake Kigwangala aliyepo TBC kila siku akitudanganya? Sheria ya Kigwangala sijui iliishia wapi.
Kigwangala siku hizi yuko bize kuomba pikipiki za mkopo kwa Mo Dewji mpk wanamuita Hamisi Mikopo.
 
mambo mawili
la kwanza hao wadudu wamepandikizwa yaan wakuletwa wameundwa maabara

jambo la pili ambalo ndio kuu zaidi hawatumii mbegu za asili zile za zamani ambazo zilikuwa na uwezo wa kuhimili magonjwa kwa kiasi kikubwa unaweza mche 1 tu ukawa umeathirika na mingne ikawa poa lkn mbegh hizi za kisasa ugonjwa ukianza mche 1 tegemea shamba zima km ujamwagilia dawa zao

SOLUTION tutumie mbegu zetu za hasili za zamani kuepusha madhala

mana nimeshangaa siku hizi mpk mpunga unatiwa mbolea unapuliziwa na dawa aisee sasa hii si balaa inapoelekea mpk muhogo utawekwa mbolea aisee
Acha kupotosha watu. Sio kweli hayo uliyoandika
 
Ndodi mwenyewe inawezekana yumo humu anawacheki tu mnavyoumiza vidole vyenu kutype wakati mwenyewe anakuna kitambi chake...
 
Ebu pinga kwa hoja mkuu, kusema ninapotosha bado haitoshi
Unga wa dona hauna aflatoxin ungekuwa na hicho usemacho ungekuwa umepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu na wanyama. Aflatoxin inatokea pale unga unapopata unyevu wakati wa ku uhifadhi ambapo unazalisha utando.Na Pia kiini cha mbegu ya mahindi hakina aflatoxin kama kingekuwa nacho mahindi yasingekuwa yanatumika yangekuwa sumu.
 
Hahahahaa... mimi nilikuwa napenda kusikia kicheko chake..
Kicheko kama sauti ya cherehani ikishona nguo!!
 
NENDA PALE MAGOMENI MWEMBE CHAI ALIKUWA NA KITUO CHAKE KIKUBWA TU
Tulimpeleka mtoto kwake akiwa anasunbuliwa na minyoo akatuambia matibabu yake ni laki tisa......yani 900k au kwa jina lingine mia tisa elfu
Mtumishi wa Kisabato huyo.
 
Hahah jamaa mswahili sana yule.

Anakwambia kwny tendo mwanamke ni kama chungu kinachelewa kupata moto na kinachelewa kupoa huku mwanaume ni kama sufuria linawahi kupata moto na linawahi kupoa.
Hapo penyewe ni sahihi
 
Anakwambia:

Matumizi ya sukari siyo mazuri. Hizi soda tunazokunywa na sukari tunazoweka kwenye chai zinaharibu afya zetu badala yake inatakiwa utumie asali.
Kwanza asali siyo tamu kama unabisha lamba asali halafu sikilizia ule utamu wake mwishoni utaona asali ni chungu.

Kwahiyo jitahidini kutumia asali, achana na sukari achana na soda.

Kuna member humu akasema akiwa mgahawani mkoa fulani bwana ndodi akiwa na kitambi kimeiva alinunua ugali wa sembe(unga anaokataza), kuku nusu (wa kizungu na kaungwa mafuta anayokataza), alivyomaliza akashushia na fanta baridi.
Kha!kha!,Umenivunja mbavu balaa,yaani anatuzuia sisi wengine halafu yeye anatumia.Kampuni za Soda inabidi zimshitaki Kwa kuwaharibia soko.
 
Unatakiwa kuandaa vema mahindi yako.... Na usipende kutumia mahindi ambayo haujui yametokea wapi. Mengine wameyahifadhi na masumu ya wa dudu so ukisaga dona unakuwa katika hatari.

Mahindi mazuri ni yale unayawahi shambani kabla hayajapelekwa ghalani na kuwekwa dawa.

By the way, wakulima wetu tu miaka hii ni washamba na malimbukeni. Back in a day haya madawa ya kuzuia wadudu waharibifu hayakuwako na mahindi yalihifadhiwa vema tu na yakawa salama mwaka mzima na hata miaka.

Matumizi ya mapipa, na zile ghala za jadi. Tujifunze namna salama za kuhifadhi mazao tuachane na usenge wa kuiga kila tunacholetewa........ Ufala tu
Sure mkuu.Ila siku hizi unaweza kutunza mahindi bila kuweka dawa,kwa kutumia mifuko ya Kinga njaa.
 
Unga wa dona ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.
Exactly
 
Huyu si yule tapeli alikuwa akidanganya kutibu kisukari?
Alikula sana hela za watu hadi wengine wakatangulia mbele ya haki kwa kuamini tiba zake! pambaf!
 
Mmmmmmhmn so mababu na bibi zetu ambao wamekula dona maisha yao yote hiyo Aflatoxin haikuwapo au ndio mzungu ni kama MUNGU anachosema na asikilizwe?!

Unajua madhara ya kula masembe wewe?!

Unga wa dona unbalance virutubisho na ndio maana hata wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kutumia huo na sio ule wa sembe. Sembe sio nzuri kwasababu inasababisha mwili kuzalisha kiwango kikubwa sana cha sukari inayotokana na wanga wake. Na mwishowe ndio watu wanakuwa na mifuta mwilini na haieleweki inatokea wapi.
Mkuu....
Zamani watu walikula dona, madhara pengine hayakuwa makubwa. Hii ni kwa sababu lifestyle ya zamani ilikuwa tofauti, watu wakila vyakula vya asili zaidi.
Kwa lifestyle tunazoishi sasa, ni wazi kwamba kuwa exposed kwa risks kama hizi huongeza hatari ya kuathirika.
Epuka kula dona ambalo hujui mahindi yake yaliandaliwaje kwanza.
Kumbuka, wafanyabiashara wasio waaminifu huandaa unga bila kuosha mahindi na mara nyingine mahindi hayo huwa yaliwekwa dawa za kuua wadudu ghalani.
 
Jamaa anakwambia Ukichukua Coca-cola ukaichemsha kuna vitu vinabaki kwny sufuri,zile ni sumu.

Sasa unajiuliza unachemsha Coca ili upate nini?Maana haikutengenezwa ili ichemshwe.

Pili inayobaki chini kwny ile sufuria si ni ile sukari ya kiwandani 'industrial sugar' au?

Ndodi anakwambia hio ndio ile sumu niliyokua nakwambia na ndio maana ukichukua msumali ukauweka kwny Coca baada ya siku kadhaa utaukuta na kutu au ukimimina Coca kwny choo kilichojaa inaenda inasafisha vzr kabisaaa.

Hahah jamaa aliwezaga kutupiga Saundi sana aisee.
Nilienda kufanya majaribio kwenye ishu ya msumari,nikakuta sio kweli,tokea hapo niliendea kutwanga coca km kawa.
 
Sumu ya Aflatoxin inatokea tu ikiwa mahindi yalivunda, kama yalikauka vizuri na hayakuingia maji mahindi hayana shida kabisa. Pia sumu hiyo inaua haraka, otherwise ungeona watu wanaanguka kila mahali kwa sababu ya kula ugali.

Sawa inabidi tuchukue tahadhari lakini sio kweli kuwa unga wa dona una sumu.
Mkuu hapa umetupiga fix, sumu kuvu (aflotoxin) haisababishwi na kiini bali uhifadhi mbaya ambao hupelekea mahindi kutengeneza kuvu hiyo kuvu sasa ndio huzalisha hiyo sumu

Pia inapatikana kwenye karanga na mazao mengine mengi tu ambayo hayakuhifadhiwa vizuri sasa na kwenye karanga utasema kuna kiini

Hata huo unga wa sembe (ukishakua tayari) kama haukuhifadhiwa mahali pakavu vizuri bada unaweza tengeneza kuvu na kisha kutokeza sumu ya aflotoxin
Ebu ngoja niwape darasa kwanza.....
Mahindi hushambuliwa na vimelea tofauti ikiwemo ukungu (fangasi) ambao baadhi yake hutoa sumu ziitwazo sumukuvu.
Mahindi ndio zao linaloshambuliwa zaidi na sumukuvu na kwa Tanzania takribani moja ya tatu ya mahindi yanapovunwa tu huwa yamesheheni sumukuvu.
Sumukuvu husababisha kansa hususani kansa ya ini na ya koo, apmoja na matatizo mengine hasa kwa watoto.
Fangasi wanaoshambulia mahindi na kutoa sumukuvu, hukua zaidi chini ya ngozi ya punje ya hindi. Na mahindi yakikobolewa, sehemu kubwa ya fangasi hawa na sumu zake huondoka na pumba. Kwa hiyo mahindi yakikobolewa, yakaoshwa kisha kusagwa unga huwa na kiwango kidogo zaidi cha sumukuvu kuliko mahindi yakisagwa hivyo hivyo.
Kwa hiyo, kama wewe ni mpenzi wa dona, hakikisha mahindi umeyachambua na kuyaosha kabla ya kuyasaga.
 
Mmmmmmhmn so mababu na bibi zetu ambao wamekula dona maisha yao yote hiyo Aflatoxin haikuwapo au ndio mzungu ni kama MUNGU anachosema na asikilizwe?!

Unajua madhara ya kula masembe wewe?!

Unga wa dona unbalance virutubisho na ndio maana hata wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kutumia huo na sio ule wa sembe. Sembe sio nzuri kwasababu inasababisha mwili kuzalisha kiwango kikubwa sana cha sukari inayotokana na wanga wake. Na mwishowe ndio watu wanakuwa na mifuta mwilini na haieleweki inatokea wapi.
Hiyo sumu siyo kila unga wa dona unayo. Inakuwa kwenye unga iwapo mahindi hayakukaushwa vizuri na kuweka fungus ambao wanazalisha hiyo sumu. Na pia inahitaji iliwe kwa kiwango kikubwa na mara kwa mara. Hata ukikoboa haisaidii. Nadhani solution ni kuhifadhi mahindi vizuri. Risk yake siyo kubwa sana kwani mahindi yamekuwa sehemu ya mlo wa aafrika wengi kwa uda mrefu.
 
Unga wa dona hauna aflatoxin ungekuwa na hicho usemacho ungekuwa umepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu na wanyama. Aflatoxin inatokea pale unga unapopata unyevu wakati wa ku uhifadhi ambapo unazalisha utando.Na Pia kiini cha mbegu ya mahindi hakina aflatoxin kama kingekuwa nacho mahindi yasingekuwa yanatumika yangekuwa sumu.
Mkuu, ebu acha kuniaibisha basi.....
Nakumbuka May 2019 msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi Gaudensia Simwaza amesema, ulaji wa vyakula vilivyochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu husababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu.
Madhara ambayo mtu anaweza kuyagundua baada ya muda mrefu kupita ni ya kuugua saratani ya ini, na madhara ya muda mfupi ni mlaji kuugua ugonjwa wa kuhara.
Tena aliongeza kwa kusema, sumu hiyo hupatikana kwenye mazao ya nafaka hasa mahindi na karanga, na kwamba walaji wa ugali wa dona wapo hatarini zaidi ikiwa hatua za uandaaji wa chakula hicho hautazingatiwa.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwaza alipoulizwa kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibiti waandaaji wa unga wa dona nchini na madhara yanayoweza kumpata mtu endapo atakula chakula hasa ugali wa dona ambayo imechafuliwa na sumukuvu.
Tena aliongeza kwa kusema kwamba.....
Dona ina lishe na ni sahihi kuliwa, shida ni maandalizi ya unga wa dona. Ni lazima anayeandaa aoshe kwa umakini na usahihi kwani wengi huhifadhi mahindi na dawa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom