Anakwambia:
Matumizi ya sukari siyo mazuri. Hizi soda tunazokunywa na sukari tunazoweka kwenye chai zinaharibu afya zetu badala yake inatakiwa utumie asali.
Kwanza asali siyo tamu kama unabisha lamba asali halafu sikilizia ule utamu wake mwishoni utaona asali ni chungu.
Kwahiyo jitahidini kutumia asali, achana na sukari achana na soda.
Kuna member humu akasema akiwa mgahawani mkoa fulani bwana ndodi akiwa na kitambi kimeiva alinunua ugali wa sembe(unga anaokataza), kuku nusu (wa kizungu na kaungwa mafuta anayokataza), alivyomaliza akashushia na fanta baridi.