Je, Yu wapi Dkt. Isaac Ndodi?

Je, Yu wapi Dkt. Isaac Ndodi?

Kuna radio moja nilikuta kipindi chake anaendelea na mafundisho yake!
 
Anakwambia:

Matumizi ya sukari siyo mazuri. Hizi soda tunazokunywa na sukari tunazoweka kwenye chai zinaharibu afya zetu badala yake inatakiwa utumie asali.
Kwanza asali siyo tamu kama unabisha lamba asali halafu sikilizia ule utamu wake mwishoni utaona asali ni chungu.

Kwahiyo jitahidini kutumia asali, achana na sukari achana na soda.

Kuna member humu akasema akiwa mgahawani mkoa fulani bwana ndodi akiwa na kitambi kimeiva alinunua ugali wa sembe(unga anaokataza), kuku nusu (wa kizungu na kaungwa mafuta anayokataza), alivyomaliza akashushia na fanta baridi.

kudadek umeua
 
Mmmmmmhmn so mababu na bibi zetu ambao wamekula dona maisha yao yote hiyo Aflatoxin haikuwapo au ndio mzungu ni kama MUNGU anachosema na asikilizwe?!

Unajua madhara ya kula masembe wewe?!

Unga wa dona unbalance virutubisho na ndio maana hata wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kutumia huo na sio ule wa sembe. Sembe sio nzuri kwasababu inasababisha mwili kuzalisha kiwango kikubwa sana cha sukari inayotokana na wanga wake. Na mwishowe ndio watu wanakuwa na mifuta mwilini na haieleweki inatokea wapi.
Wazungu na mawakala wao..wametuweza... ... vyetu vyote ni sumu... na sisi tumetiwa upofu .. na ma Dr. wetu ndio kabisaaa.. .. kinga lazima zishuke.. ..
 
Mkuu....
Zamani watu walikula dona, madhara pengine hayakuwa makubwa. Hii ni kwa sababu lifestyle ya zamani ilikuwa tofauti, watu wakila vyakula vya asili zaidi.
Kwa lifestyle tunazoishi sasa, ni wazi kwamba kuwa exposed kwa risks kama hizi huongeza hatari ya kuathirika.
Epuka kula dona ambalo hujui mahindi yake yaliandaliwaje kwanza.
Kumbuka, wafanyabiashara wasio waaminifu huandaa unga bila kuosha mahindi na mara nyingine mahindi hayo huwa yaliwekwa dawa za kuua wadudu ghalani.
Nafahamu. Mahindi yangu huwa nachukulia shambani
 
Dr. Ndodi yupo anaendelea na shughuli zake. Kwa sasa kama uko mbali na Dar huwezi kujua maana yule Waziri aliyekwepa Twiga akavunjika mbavu alibadili kanuni ili kumkomoa Dr MWAKA kwa kupiga marufuku watu wa tiba mbadala kujitangaza kwenye TV au kubandika mabango mitaani.
Wenawe umetisha
 
Dr ndodi alikuwa anakuambia ukiumwa malaria kunywa maji Lita tano kwa siku Saba unapona

Kuna mwamba mmoja tulikuwa tunasoma nae uboyizi so akajaribu hii mbinu alizidi ikabidi atafutie mseto ndio ulikuwa unaanza kuingia na haujawa officially kuwa dawa ya serikali

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Yule bwana aliyevuma kwenye runinga miaka ya nyuma kwa kutoa ushauri nasaha na tiba kwa maradhi tofauti ya Binadamu. Jamaa alikua mjanja mjanja fulani hivi nakumbuka alikuwa akipiga vita sana watu wenye vitambi lakini cha ajabu alipopata umaarufu na mambo kumwendea vema nae kitambi kikaja kwa Nguvu zote!

Tujuzane huyu mtu yupo wapi? Ina maana ameacha tiba zake mbadala?
Malamba mawili Daslam kituo,shusha kwa Ndodi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom