Je, wapinzani ni wakombozi?

Ukienda Somalia leo ukawakuta wale wenye shida kubwa ama darfur uka offer msaada wa masharti nafuu naamini wengi watakuja .Hawa wanao rudi CCM si wapinzani ni wenye njaa na walienda kwa kutumwa sasa wanarudi kwao waliko toka ila kwa kuwa wanakati wanaenda hawakusema walikuwa CCM sasa wanarudi wanaitwa Wapinzani ili CCM na Makamba wapate la kusema .Unasemaje ?
 
Matemegeo(lol)ya huyu Mwanasiasa ni kuwa waziri mkuu ama kiongozi mwengine yeyote wa serikali endapo CUF ingeshinda sasa kashaona ulaji hakuna ndio hivyo tena ananyoosha mikono juu na kurudi kuitumikia CCM ambayo ana uhakika atapewa hata ukuu wa wilaya
 
Poorman,

Nadhani nitakuwa nimepitwa na hiyo habari ya Marando kurudi CCM! duh! lini tena hiyo?
 
Ogah, mbona alirudi siku nyingi akapewa nafikiri Ubunge wa Afrika Mashariki or something..
 
Noo Mwanakijiji,

Kama Marando alirudi CCM basi itakuwa very recent (during/after 2005 elections) na sio kama unavyofikiri, hebu soma hii habari hapa (hii ilikuwa 2001)

Nine Tanzanian Parliamentarians Chosen for EAC Assembly

The National Assembly of Tanzania (Parliament), Friday elected nine members of different professions as legislators for the forthcoming East Africa Legislative Assembly (EALA), or the House of the East African Community (EAC).

Announcing the election results in the House in central town of Dodoma, the Returning Officer Kipenka Mussa said that three women and six men emerged winners.

Mussa, who is Clerk of the National Assembly, said that the three winners out of 10 women aspirants are Kate Kamba, a former cabinet minister, Beatrice Shelukindo from the mainland and Mahafuza Alex Hamid from Zanzibar. They are all from the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM).

The returning office said that five men from CCM, Ambassador Isack Sepetu, Said Bakari Jecha in Zanzibar, Abdulrahman Kinana, former defense minister, Dr. Harrison Mwakyembe, a lecturer at the University of Dar es Salaam's faculty of law and George Nangale in the mainland passed the voting.

The sole winner from the opposition party is the NCCR-Mageuzi candidate Mabere Nyaucho Marando, who defeated three opposition aspirants.

The arrangements for the swearing-in ceremony of the elected EALA legislators will be announced by the EALA itself in August.

Initially a total of 59 aspirants vied for the seats on CCM ticket, 46 of whom were from the mainland and 13 others from Zanzibar, and the list was filtered to 24 by the party's central committee. The opposition produced four candidates.

Each of the three EAC member states, namely Kenya, Tanzania and Uganda, is supposed to elect nine members to the Assembly, which is to be located in Tanzania's northern town of Arusha, but the method of electing the MPs is to be decided by member states.

In Tanzania, the ruling CCM, through the National Assembly, has decided that eight out of the nine EAC MPs will come from CCM and only one will be nominated by the five opposition parties that have MPs in the country's assembly.

House Speaker Pius Msekwa said that the number was arrived at on the basis of the ratio of party its in the National Assembly, where CCM has the majority.

As the original EAC, once the pride of east Africans, collapsed in 1977, mainly because of political, ideological and economic differences among the three neighbors during the regimes of Presidents Jomo Kenyatta of Kenya, Julius Nyerere of Tanzania and Idi Amin of Uganda.

Efforts to re-launch the new regional body started in 1992 when Moi, Museveni and ex-Tanzanian president Ali Hassan Mwinyi met in Harare, capital of Zimbabwe, during the Commonwealth Heads of State and Government meeting.

The new EAC was founded on November 30, 1999 when Kenya, Tanzania and Uganda signed a treaty to replace the then East African Cooperation.

It will expand and deepen economic, political and social cooperation among the three neighboring states with a combined population of about 80 million and territories of 1.8 million square kilometers.

The 153-Article Treaty for the Establishment of the East African Community says that a Customs Union will be established as the entry point of the Community, followed by a Common Market, subsequently a Monetary Union and ultimately a Political Federation of the East African States.

The main organs of the EAC are the Summit of Heads of State, the Council of Ministers, the Coordination Committee, Sectoral Committees, the East African Court of Justice, the East African Legislative Assembly and the Secretariat.

The efforts, since the effective resumption of regional cooperation in 1996, have been taken up mainly by laying the groundwork for regional integration.

source:http://english.peopledaily.com.cn/english/200106/16/eng20010616_72762.html
 
Ukienda Somalia leo ukawakuta wale wenye shida kubwa ama darfur uka offer msaada wa masharti nafuu naamini wengi watakuja .Hawa wanao rudi CCM si wapinzani ni wenye njaa na walienda kwa kutumwa sasa wanarudi kwao waliko toka ila kwa kuwa wanakati wanaenda hawakusema walikuwa CCM sasa wanarudi wanaitwa Wapinzani ili CCM na Makamba wapate la kusema .Unasemaje ?

Tibwilitibwili unajua sana kuwapigia ngoma kenge; uliyosema ni sahihi kabisa.

Watu wenye misimamo ya kiasiasa huwa hawahamihamai vyama mpaka pale inapoonekana kuwa mawazo yao hayakubaliki kabisa katika vyama vyao wakati yakubaliwa katika vyama vingine. Viongozi wote waliohama upinzani na kurudi CCM ilikuwa ni njaa tu. Hebu angalia Dr. Lamwai alinyimwa license ya uwakili pale Dar akahamia Zanzibar ambapo palikuwa ni adha sana kiutendaji hivyo akaamua kurudi CCM na leo ana licensse yake pale Dar Salaam. Dr. Kaburu baada ya kukosa ubunge wa Kigoma aliahidiwa na Mr. Makamba kuwa atapewa ubungea wa EA akiingia CCM. Tambwe alikwenda CCM baada ya kuonekana na CUF kuwa ni bomu baada ya evaluation ya muda mrefu. Sina uhakika kama Marando alisharudi CCM ila wakati akiwa mbunge wa EA alikuwa bado yuko NCCR-Mageuzi kisheria. Nsanzugwako alirudi CCM pia kwa kuahidiwa madaraka na ndiyo maana tangu ameenda CCM amekua anayeya kwa madaraka kama nini.
 
Marando ni NCCR hata sasa tena mwanaachama hai sema ubaya wa Marando bado ni shushu sasa hapa ndipo tujiulize kama ni CCM ama NCCR kweli ?Lakini hadi sasa ukimsikia anakata issue utalala chini na ni mtu ana heshimiwa sana ndani ya NCCR kama Mwalimu na CCM yake .
 
Suala la kuhamahama ni jambo muhimu sana ambalo vyama vya upinzani vinapaswa kuliangalia kwa makini.Kwa bahati nzuri nimekuwepo Kigoma kwa muda mrefu kushuhudia uchaguzi wa marudio na chaguzi zingine zilizo muhusisha Kaburu.Nashindwa hapa nitumie neno Ushamba au Ulimbukeni.Huyu Kaburu ambaye alikuwa mpinzani alitoa matumaini kwa watu wa Kigoma, lakini baada ya Kuonja visenti na ka-tittle kule bungeni alibadilika na kuwa jeuri na kiburi kwa watu waliompa kura,waliopigwa kwa ajili ya kulinda masanduku ya kura hadi yeye kupata ubunge.Zaidi hakutaka kukanyaga jimboni kwake hadi kipindi cha uchaguzi.
Bahati nzuri wananchi walimchoka na kulikuwa na kila dalili za kuwa na wasingeweza kumpa kura tena.Naamini hii ni hali ambayo imekuwa ikitokea katika sehemu nyingi za majimbo na hivyo kupelekea upinzani kupoteza majimbo zaidi mwaka jana. Baada ya kugundua kuwa hatapewa ulaji tena na wananchi wa Kigoma,aliamua kuhamia CCM ambako aliahidiwa kuendelea kupata ulaji.
Hali kama hii inawafanya wanachi wapate somo, na wajiulize mara mbilimbili kama kweli upinzani kweli upo kwa ajili wananchi au kukidhi haja zao. Hivyo wanawatumia wananchi kama nyenzo.
Mimi ni mmoja ya watanzania wanaopenda kuwaona CCM wakiondolewa madarakani.Lakini lazima nimuamini yule nitakayempa madaraka kuwa ataniletea mabadiliko ninayohitaji.
 
Nyangumi.. maneno yako ni kama mwiba.. lakini hilo la "hii inawafanya wananchi wapate somo" sina uhakika nalo! Tatizo la Wabunge kusahau majimbo yao hadi wakati wa uchaguzi halikuanzia na wapinzani! Wabunge wa CCM wamekuwa wakifanya hivyo miaka nenda rudi na wanazidi kutanua. Inaonekana hakuna mwananchi aliyejifunza lolote lile. Unafikiri Zitto atawakomboa watu wa Kigoma jinsi anavyosakamwa!! msishangae na yeye siku moja akaweka manyanga chini na kurudi "Kundini"!
 
Mzee mKJJ Zitto kurudi kundini umesema isivyo sahihi . Kaburu amewahi kuwa CCM kabla Zitto hawajahi kuwa mwana CCM . Ila akisakamwa sana na pamoja na kila dalili za kumnunua ambazo zinapitia kwa Waziri wa fedha aliyetumwa kumpa wa yeye kutakiwa na JK anaweza kuchoka. Zitto has been clear kwamba yeye anataka kuendeleza upande wa pili na ndiyo maana unaona sasa Sitta kaanza baada ya akina Meghji kujibiwa kwamba Mama nakuheshimu lakini sitaweza kuingia CCM.
 
Lunyungu... sijasema atahama.. lakini akishindwa kuleta maendeleo kutokana na mizengwe ya CCM halafu CCM wakatwaa jimbo hilo in 2010 atakula wapi?
 
Kwani kabla ya Ubunge alikuwa anakula wapi ? Mbona una mawazo ya kizembe ? Unapinga nini juu ya wabunge na unasema nini sasa ? Zitto kabla ta Ubunge alikuwa na kazi ambayo anapata mshahara zaidi ya huo wa Ubunge ama hujui ?Ubunge ni utumishi pamoja na kula lakini akiukosa bado anaishi. Je walio ukosa Ubunge kwenye CCM na upinzani wanakula wapi ama wote wamesha kufa ? Mawazo yako yananipeleka kuamini kwamba wewe na CCM yako ndiyo wagawa riziki hapa Duniani ndiyo maana mnawabana watu waendelee kuwaweke ili mle maana si kuongoza na kuitawala Nchi kwa mema. Pole kijana
 
Mwakjj.Hapo siwezi nikaweka Shilingi yangu ila mimi naamini kuwa kama kutakuwa na mwanamageuzi ya kweli ni rahisi kuleta ukombozi.Kwanza jua jimbo lako limezungukwa na watu namna gani? Wakulima au wafanyabiashara.Then jaribu kuondoa kero zao.Kaburu alikuja vizuri sana mwanzoni kwa kujua hilo na kujaribu kuwasaidia na ndo maana aliweza kushinda chaguzi zilizopita.Lakini baada ya pesa kumjaa kiburi kikajaa hakuona tena haja ya kuwakaribu na wananchi.
Ila kumbuka kama unanguo ya zamani yenye viraka usiitupe kwanza kabla ya kuwa na uhakika wa nguo nyingine nzuri.Hichi ndo kinachowafanya watanzania kusita kuwatema CCM.ILa pale wanapopata matumaini wanafanya hivyo.
 
Mwanasiasa,
Good question. Maana kuendekeza ile mentality ya "atakula wapi," ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Tunachoangalia ni kula tu na si kujenga nchi. Ask what you can do for your country and not what your country can do for you.
 
Stop!... Hammer....time!

Ebu kwanza bandugu nifamisheni vizuri kuhusu huyu Kabourou!...
Inaonyesha kwanza alikuwa akipendwa na wananchi wake kwa sababu ya ahadi alizotoa!... kisha alipopata Ubunge kawaacha ktk mataa!... jamani mwee hamuoni kama hii ni conviction tayari ya yale tunayozungumzia?...

Ndugu zangu wa Chadema ebu nambieni imekuwaje huyu mtu atumie jina la Chadema kupata kura kisha baada ya Ubunge awe na uamuzi wake binafsi kuhusu wananchi wake?...Ya CCM yanajulikana msianze kunipa mifano yao tena maanake hapa tunatafuta viongozi wanaoweza kutuletea mabadiliko.
Je, Chadema hawana Utaratibu wa kuhakikisha kuwa wabunge wake wanaoshinda/shindwa ubunge watakuwa wakitumia muda wao mwingi huko wilayani na sio kuwa na makazi Dar wakisubiri wakati wa Uchaguzi?..

Nadhani somo la kabourou liwe fumbua macho kwenu kiasi kwamba kila mbunge aliyeshinda hataruhusiwa kisheria (chama) kufanya mambo anayotaka yeye!.. na labda hata fungu la mshahara wake ama posho lichukuliwe na chama kufungua miradi midogo midogo kuwazawadia wananchi, hii ndiyo miujiza ya Mussa na Yesu nayozungumzia kila mara!
 
Mwanasiasa na Jasusi,

Kwa kuongezea tu nafikiri pia Kabourou ametuonyesha wazi jinsi mbunge mchaguliwa alivyombali na wananchi badala yake DC (mteule wa rais) ndiye anashinda na wananchi!..
Hii ni inatupa picha nzuri ya kumwondoa kabisa DC na kumfanya Mbunge awe karibu na wananchi!.
Mbunge awe DC
 
Mwanasiasa,
Nasubiri majibu ya hoja nyingine kabla sijazama zaidi ktk upimaji wangu.
hata hivyo, samahani mkuu nitapenda kufahamu hiyo KATIBA ambayo itawashirikisha wananchi inaundwa vipi? (process yake)..
Pili, hili swala la rais wa Zanzibar bado zito sana kwangu! nakuwa mzito kuamini kuwa Sharrif hamad akichukua urais wa Zanzibar chini ya CUF na bara iwe chini ya CCM, kutakuwepo na mfarakano mkubwa zaidi.
Hofu yangu kubwa ni kuwa vyama hivi vyote vinapigiwa kura sio kwa sababu ya sera zao (CCM) isipokuwa nani kasimamishwa. Na kibaya zaidi ni kwamba wananchi wepesi wa kusamehe chama makosa yake inapofikia kuwepo kwa utenganishi wa rangi.
Mwanasiasa, kumbuka tu sisi ni waafrika... tuna vijimila vibaya ambavyo haviwezi kuondoka kirahisi kwa hii demokrasia ya wazungu. Hata kama ndugu yako ni jambazi, siku akikamatwa mshikaji utamtetea kwa kila hali na pengine kuficha hata silaha zake!.. kwetu damu nzito sana na hakuna demokrasia inayoweza kuvunja mila hii kirahisi.. na ndio hapo by extension tunafika hadi kwenye makabila!..sielewi hayo marekebisho ya Katiba yamezingatia kwa kiasi gani mazingira yetu ama ndio sifa za Mzindakaya kuwa na ng'ombe wa kizungu 3,000!

Anyway, yote tisa, kumi hamuwezi kuwa na mabadiliko yoyote ktk katiba bila kuchukua kwanza ushindi bungeni!..
Nasubiri majibu ya hoja nyinginezo

Mkandara: niliahidi kukujibu swali lako kuhusu mchakato (process) wa kutunga katiba inayokubalika na kuheshimika kwa wananchi wote. Wataalamu wameanishwa michakato mbalimbali ya kutunga katiba. Mimi, na nafikiri CHADEMA kama chama pia, ninakubaliana na ule mchakato uliotolewa na Profesa Issa Shivji. Mchakato huu una hatua 4 zifuatazo:

1) Kutoa vikwazo vya kisheria vya kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi kufanya kazi-hatua hii ilikwishatekelezwa
2) Kuruhusu uundwaji wa vyama na taasisi za kiraia-hatua hii nayo kwa kiasi fulani ilishatekelezwa
3)Mkutano wa Kitaifa: Hii ni hatua ya kisiasa katika kutafuta makubaliano kuhusu mambo muhimu ya kuingizwa katika katiba. Mkutano huu utajumuisha wa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wananchi yakiwemo: vyama vya wakulima, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wavuvi, wafanyabishara, vyama vya siasa, taasisi za kidini, raia mashuhuri, wasomi, n.k. Kazi kubwa ya mkutano huu itakuwa kupata makubaliana juu ya mambo na misingi muhimu ya kuingiza katika katiba
4) Tume ya kuandika katiba: Baada ya kukubaliana misingi ya katiba, mkutano wa kitaifa utateua wajumbe kadhaa wenye fani mbalimbali watakaopitia yale yaliyokubaliwa katika mkutano wa kitaifa na kuyaandika katika lugha ya kikatiba. Hatua hii itatoa juzuu ya kwanza ya katiba
5) Juzu ya kwanza ya katiba itarudishwa kwa wananchi kwa njia ya kura ya maoni ili wananchi waikubali hiyo juzuu kuwa katiba. Kura ya maoni ikikamilika na kama wananchi wataikubali hiyo juzuu ya kwanza, basi hatua ya mwisho inafuta, ambayo ni:
6) Bunge kukaa kama bunge maalumu kwa ajili ya kupitisha katiba (Constituent Assembly). Hiyo juzuu ikitika hapa imepitishwa tunakuwa na katiba ya nchi.

Hizi ni hatua muhimu sana katika kupata katiba ambayo ni 'fair, just and respectable'.

Nitaendelea baada ya maoni yako na wengine.
 
Marando ni NCCR hata sasa tena mwanaachama hai sema ubaya wa Marando bado ni shushu sasa hapa ndipo tujiulize kama ni CCM ama NCCR kweli ?Lakini hadi sasa ukimsikia anakata issue utalala chini na ni mtu ana heshimiwa sana ndani ya NCCR kama Mwalimu na CCM yake .

Well, Marando ni NCCR by card but not by heart. Na ndiyo maana kama unakumbuka wapinzani walishamjua hilo wakati wa kugombea Ubunge wa East Africa Wapinzani wote hawakumpa kura !! CCM pekee yao ndiyo walimpa kura na wapinzani hata zile vote of thanks walikataa kumpa kwani yule ni CCM damu na kwa kujua hilo wapinzani waligundua kwamba CCM wamewazunguka kwa kuweka watu wao mara mbili. Walitumia wanachama wao kuogombea na pia kuwatumia vibaraka wao kugombea. Unaposema Bwa Lunyungu kuwa Marando ni respectable person kwenye NCCR nadhani hapo umechemka, kwani ingekuwa hivyo basi hata NCCR wasingemnyima kura ya East African.

Kwa ujumala ndiyo maana humsikii tena YAMEKWISHA, amesharudi kwao CCM lakini by card mnamwona NCCR
 
Back
Top Bottom