Je, wapinzani ni wakombozi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, wapinzani ni wakombozi?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 8, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 8, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya watu ambao wanataka tuamini kuwa siku Tanzania ikichukuliwa na wapinzani basi matatizo yote ya Tanzania yatatoweka kama ukungu! Baadhi ya watu hawa, hawaishi kuonesha udhaifu wa chama tawala na serikali yake iliyoko madarakani. Ni watu hawa ambao kwao hakuna jema lolote, na hakuna kitu chochote kizuri ambacho kimewahi kufanywa na serikali iliyoko madarakani. Kwa watu hawa, ili kuweza kuona angalau kitu kizuri basi inabidi utumie darubini!!

  Baadhi ya watu hawa wameonesha uwezo mkubwa wa kuonesha matatizo na udhaifu wa chama tawala ambao hahuitaji darubini kuuona kwano ni dhahiri! Ni rahisi kwao kuonesha mapungufu ya masuala ya mikataba mbalimbali, tuhuma za rushwa n.k! Ni kwa sababu hiyo basi baadhi ya watu hawa pamoja na wapiga debe wengine wa upinzani wamefikia mahali pa kudai kwa ujasiri kuwa CCM na serikali yake havijafanya lolote la maana zaidi ya kutudidimiza kimaisha.

  Ukweli wa mambo ni kuwa hoja zao nyingi ni za msingi na mambo mengine ambayo wanayaonesha ni ya wazi ambayo hata mtu asiye mpinzani anaweza kuyaona! Kwa mtu yeyote anayeipenda nchi yetu hatuna budi kuwashukuru watu hao kwa moyo wao wa kizalendo na kujituma kufichua maovu na ufisadi! Siyo jukumu la watu hao peke yao na vyama vyao kuonesha ubaya, upotofu, na ubovu wa serikali iliyoko madarakani! Si vibaya kabisa kwa wao kwa kutumia mwanga kama wa kurunzi kuangazia umma na kuonesha kuwa baadhi ya viongozi au wafanyakazi wa serikali ni wabadhirifu, wanatumia madaraka yao vibaya, na baadhi yao wamefanya vitendo ambavyo vinapakana kabisa na usaliti kama siyo uhaini dhidi ya jamhuri yetu.

  Viongozi hawa walioko upinzani na wapambe wao wamejitahidi miaka nenda rudi tangu kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi kuiamsha Tanzania ili wananchi waelewe kuwa kuna chaguo jingine na kuna chama mbadala wa CCM. Walijaribu kwa mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa 1995 na kutokana na mvuto wa mmoja wa wapinzani hao aliyewahi kuwa madarakani basi watu waliamua kuachana na CCM na kujiunga na upinzani wakitumaini kuwa hapo "wamefika nyumbani" kwani CCM imewachosha! Lakini katika chaguzi mbili zilizofuata baadaye (2000 na 2005) vyama hivi vimeendelea kufanya vibaya licha ya majina yao na itikadi zao kueleka zaidi!

  Pamoja na kudidimia kwa vyama hivyo kwenye sanduku la kura, viongozi wao bado wanapita kunadi sera zao wakiangazia udhaifu na ubovu wa CCM kuwa ni sababu ya wananchi kuwaamini kuwa wapinzani ndio mbadala wa uhakika wa chama tawala, na hivyo wananchi waanze kuwaamini kwa kuwapa madaraka!

  Swali kubwa na la msingi ambalo kila Mtanzania hana budi kujibu ni kuwa, je wapinzani wakipewa madaraka ya nchi leo hii (siyo kupewa kama hisani bali kutwaa kwa nguvu ya kura) matatizo ya Tanzania yatatoweka ghafla? Je wapinzain wakiwa Ikulu hospitali zetu zote zitakuwa za kisasa, wanafunzi wote watakwenda shule, mishahara italipwa kwa wakati n.k n.k? Je wapinzani wakitwaa madaraka ina maana umasikini wa Tanzania utatoweka ndani ya mwaka mmoja?

  Kama mifano ya wapinzani kuchukua madaraka katika nchi jirani inaonesha lolote, basi mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye anadhania kuwa endapo wapinzani watachukua madaraka basi maisha ya mwananchi wa kawaida yatakuwa ahuei na yatabadilika kwa ghafla mtu huyo adhanie tena! Ni mabadiliko gani ya kimaisha wananchi wa Kenya wameyapata baada ya NARC kuingia madarakani? Vipi kule malawi baada ya chama cha MDC kuingia madarakani watu wa Bulawayo, Lilongwe, Blantyre, na Karonga maisha yao yamebadilika vipi? Je wapinzani walipochukua madakaraka huko Zambia, maisha ya watu wa Lusaka, Copper Belt, na Capri Mposhi yamebadilika vipi?

  Wapinzani wameendelea kudai kuwa CCM imejaa watu wafisadi wasioipenda nchi yao, wenye kutumia madaraka yao vibaya, je wao wakiingia madarakani na kujaza nafasi zote za utawala kuanzia Rais hadi mwenyekiti wa kijiji watatuhakikishia vipi kuwa hakuna mtu kati mamia ya watumishi hao atakayekula rushwa au kutumia madaraka yake vibaya? Je tuna uhakika gani kuwa vyama vya upinzani vitaweza kumsimamia kila polisi, kila mwalimu, kila meneja, kila Mkurugenzi, kila mwenyekiti wa bodi n.k na kuhakikisha hakuna hata mmoja wao atakayemziba raia kibao hadharani au ambaye atafyatua bunduki yake na kumlipua mpiga debe?

  Kama kweli wapinzani wataahidi kufanya haya yote na kutokosea kabisa, kutoharibu hata mara moja, na wakiahidi kuondoa kero zote na matatizo yote yanayoikabili Tanzania huku viongozi wake wote (Rais hadi mwenyekiti kata wa kijiji cha Mkata) wakiwa waadilifu wasiomezwa na ulafi, wasiolewa madaraka wakitumikia nchi yao kwa mapenzi makubwa, basi Tanzania lazima iwachague wapinzani!! Kwani kwenye vyama vya upinzani hakuna binadamu wote ni Malaika, na wote hawajali matumbo yao wala mifuko yao!! Ni katika vyama hivyo yule Musa Nabii yupo, na ni yeye ndiye atakayetutoa utumwani!! Kama kweli vyama vya upinzani vitafanya mambo hayo yote basi ndugu zangu Watanzania, inawezekana mkombozi yupo katikati yetu na hatujamgundua!!

  Kwa kuelewa hulka za binadamu bila kujali itikadi zao na mitazamo yao kutegemea wapinzani kuwa wakombozi wa Tanzania kwa vile tu ni Watanzania wanaotoka Chadema, TLP, CUF, NCCR, au vyama vingine ni mategemeo ambayo yatapeperuka kama unyasi upeperushwavyo na upepo, ni kama umande unavyopukutika kwenye majani asubuhi inapofika! Manabii wa upinzani wako wapi watutabirie?
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  naona unaishiwa kijana MwakaKJJ . Unarudi yale yale .Labda tukuulize sasa Swali kwamba kulingana na maandishi unataka Vyam vife na uendelee na CCM lako ? Unasema Wapinzani wakuhakikishie wewe nani ? Ndiyo maana nasema una jazba na haya unaleta ni mawazo ya kizembe ni si mapya . Unalinda nini hapa ?

  Pole weeeee. watakujibu ambao hawaja kuelewa.Rudi huku Kijijini Maghorofa naona yanakupa shida sana sasa maana upenzi wako umakufanya uwe kituko. Hivi hizi sudden changes kuna mtu kakueleza soon utaitwa kwa Serikali ya JK uendeleze mawazo ya kizembe kama haya unayo sema hapa ?Si kawaida mtu kuwa na mawazo ya aina yako mwaka 2007.Maana CCM hawajambo kwa ahadi na kuhongwa umesha lambishwa ama ahidiwa kulambishwa ?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,

  Nitakupa mfano mmoja tu wa mahitaji ya kuwepo upinzani imara katika demokrasia. Hapa Marekani rais Bush ameipeleka nchi katika vita vya Iraq kwa misingi ya uwongo. Alikuwa na majority wa chama chake katika mabaraza yote ya Congress.

  Baada ya kubainika kuwa sababu za kwenda Iraq zilikuwa za uwongo Wamarekani wameghairi na katika uchaguzi uliopita wabunge wa chama cha rais Bush wameangushwa. Upinzani hivi sasa una majority tena.

  Badala ya kuangalia sijui upinzani utafanya nini tofauti mimi ningependa tuzungumzie njia za kuwezesha kuwepo upinzani imara Tanzania ambao utalazimisha sera mbadala wakati tunapoona kuwa sera za serikali inayotawala zinakwenda mrama. That should be the issue, as far as I am concerned.
   
 4. q

  quarz Member

  #4
  Jan 8, 2007
  Joined: Sep 3, 2006
  Messages: 82
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji sasa unaishiwa kabisa, to the extent kwamba sasa unataka tushawishike kuwa mfumo wa chama kimoja ndio suluhisho la matatizo yetu,

  Hiyo nchi unayoishi hapo Marekani unaona jinsi democrat wanavyo critisize republican, bado hujapata somo lolote kutoka marekani, basi ni bora urejee tanzania ulime mahindi.

  Serikali inapokuwa madarakani lazima iwe critisized, ili isijisahau,na iweze kuweka sera makini, na kazi ya vyama vingine vya upinzania ni kutoa alternatives kwa wananchi kama hawaridhishwi na serikali iliyopo,

  Mwaka 1961 uchumi wa Tanzania ulikuwa sawa na uchumi wa South Korea na Malaysia, lakini leo miaka 45 baadaye wenzetu wameweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo to the extent sasa hivi south korea ni donor kwenye mipango yetu ya maendeleo wakati sisi bajeti yetu inatemea mikopo na misaada kwa asilimia 40, unemployment ni kubwa kiasi hatuna hata statistics,what we know is more than 50% umaskini wa tanzania sasa hivi ni wakutisha.

  Kumbuka majority ya watanzania about 60% wanaishi vijijini na hawa wote hawana maji, umeme wala ajira, zaidi ya kutegemea kilimo cha kubabaisha.

  Sasa unataka kuniambia watanzania wameridhika na halii hii,hapana,

  Sasa, solution tuliyonayo ni hiyo ya kujenga vyama ambavyo vitaweza kuaminika na kutupa sera mbadala ambazo zinaweza kusaidia kutufikisha kwenye malengo yetu, mfumo wa chama kimoja tumeshaujaribu kwa karibu miaka 30 na tumeona jinsi ulivyoshindwa vibaya kutoa majibu. wewe unataka turudi kulekule?

  Jamani kwanza tujue watu wanaotaka kuuangamiza mfumo wa vyama vingi ni watu hatari na hawajari maslahi ya taifa hili, tunachohitaji ni kukusanya mawazo na kushilikiana na hawa wenzetu ili kufanya hivi vyama vifanane na vitu tunavyotaka nasio kutegemea nabii Musa aje kuvitengeneza vyama halafu sisi tujiunge.
   
 5. K

  Kulikoni JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2007
  Joined: Aug 28, 2006
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Labda Mwanakijiji atanisahihisha, kwa nilivyomuelewa hapo juu na katika maandishi yake mengineyo, hajadai kuwa turudi mfumo wa chama kimoja ... bali ni kuwa upinzani uliopo sasa BADO SANA, a view that I do share with him.

  Tunahitaji upinzani uwe imara. Concentration ya vyama vya upinzani kwa sasa iwe kujaza wabunge wengi.. urais in the next 10 years or so ni kujidanganya tu.

  Pia nakubaliana nae anaposema kwamba, yeyote anaedai kuwa upinzani ukipatiwa nchi leo basi ndio matatizo yata-vanish within a short period of time, anajidanganya. Kuna anaebisha?

  It is also an extreme view kudai kuwa serikali ya CCM haijafanya lolooote! Imefanya mengi, but we all agree that it could have done better.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 8, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hoja hujibiwa kwa hoja!

  Lunyungu:

  Wapinzani wanataka tuwaamini, wanataka tuwape madaraka! Ina maana hadi hivi sasa wamejiamini kiasi cha kutosha na wameamini wameimarika kiasi cha kutosha hadi wamefikia kumsimamisha mgombea Urais. Walishindwa. Kwa wao, kufikia mahali kusimamisha wagombea Urais, Wabunge na wawakilishi kibao ina maana wako tayari kuongoza na kutawala, ama sivyo?

  Je kama wapinzani wangeshinda uchaguzi 2005 na kuchukua Ikulu, na Bunge je ni mabadiliko gani yangetokea Tanzania hadi hivi sasa (mwaka mmoja baadaye)? Mimi nawakilisha mawazo ya Watanzania ambao hawajaridhika na CCM na hawajavutiwa na upinzani! Lakini wakipewa uchaguzi wa pande hizo mbili wanaipa kura ya ndio (licha kusita sita) CCM! Ni jukumu lenu wapinzani kuwashawashi Watanzania ni kwa nini wawape madaraka ya kuongoza nchi yetu!!

  Msituambie tuwape madaraka ati kwa sababu CCM mbovu na inanuka, tunajua hilo, tuambieni kwanini tuwape nyinyi madaraka na tofauti ya viongozi mtakaowaweka nyinyi na wale waliopo CCM ni nini? Ninawapa somo la bure hapa, mkiweza kujenga hoja inayojibu swali hilo basi mnajitengenezea njia nyeupe kwenda Ikulu!!

  Jasusi:

  Kwa karibu miaka zaidi ya kumi Democrats walikuwa upinzani na Republicans wakishikilia vyombo vyote vya Ikulu na Bunge. Je, jukumu la kujiimarisha Democrats lilikuwa ni la Republicans kutengeneza mazingira mazuri ili Democrats washinde? Kwanini, unafikiri Democrats walishinda? Unafikiri ni kwa sababu watu wanadhani Democrats ni tofauti sana na Republicans? la hasha! Democrats walijenga hoja kuwa nchi inahitaji kufuata mwelekeo tofauti na wa Republicans na pia viongozi wa Democrats walishajulikana, hakukuwa na suprise!

  Ndo maana ninawapa somo la bure wapinzani wa Tanzania:

  a. Endapo wanasubiri na kuombea kuwa CCM itaweka mazingira mazuri ili wao wachukue nchi "kwa upole, kama kumsukuma mlevi" wafikiri tena. CCM haina nia wala wazo la kuona upinzani unaimarika Tanzania! It is not in their best interest!

  b. Jukumu la kuviimarisha vyama vya upinzani ni kwa wale waliomo ndani ya vyama hivyo! Tarehe 8/10/2005 Freeman Mbowe akizungumza wakati wa kampeni kule Mbeya alisema kuwa kukosekana umoja katika kambi ya upinzani kumedhoofisha upinzani kiasi kwamba wameshindwa kupigia kelele kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi! Alifanya nini kuunganisha nguvu zake na wapinzani wenzake? Je, anafanya nini leo ili kuunganisha kambi ya upinzani kabla ya 2010?

  Sheria ya kuruhusu vyama kuungana itajadiliwa baadaye mwaka huu na bila ya shaka itapita. Unafikiri itafanya vyama hivyo vikubwa kuungana na kuunda chama kimoja au yatakuwa yale yale ya NARC Rainbow ya Kenya?

  Kuhusu njia za kuimarisha upinzani Tanzania, mbona zipo nyingi na tumezitaja sana. Je wapinzani wa Tanzania wanasikiliza? Haya, ngoja nizirudie hapa.

  a. Badala ya kunuia kupewa Urais kwenye uchaguzi wa 2010, wapinzani wadhamirie kuchukua Bunge, kwa kunyakua angala theluthi mbili ya Bunge zima. Kwa jinsi walivyo sasa hiyo itakuwa ni ndoto.

  b. Kama wapinzani kweli wanataka kuongoza nchi, njia rahisi ni kujiandalia viongozi watakaochukua nchi. Kwa idadi ya wabunge walionao sasa, hata baraza la mawaziri wasingetosha! Ushauri wangu ni huu. Mara tu sheria ya kuunganisha vyama itakapopitishwa baadaye mwaka huu viongozi wa vyama vya upinzani vikubwa (Lipumba, Mbowe, Mrema, na Mbatia) wakae chini kwa pamoja, waandike Memorandum of Understanding ya kukubali kuviua vyama vyao na kuunda chama kipya kimoja kikubwa cha upinzani, kushirikishana mali za vyama hivyo n.k. Halafu ceremonically, watangaze kuvunjika kwa CHADEMA, TLP, CUF, NA NCCR na kuundwa kwa chama kipya. Wapo viongozi watakaopoteza nafasi zao na kwa maoni yangu, wenyeviti wote wa sasa wa vyama hivyo wasipewe uenyekiti wa chama hicho kipya!!! guess why?

  c. Pindi wakishaunda chama hicho kipya, waandike ilani yao ya kuelekea 2010, wainadi kwa wananchi, na wana miaka karibu mitatu ya kuonesha ukomavu wa kisiasa na ya kuwa wanaweza kufanya kazi pamoja licha ya migongano ya huko nyuma na tofauti ya kimitazamo.

  d. Jambo la nne, waanze kampeni ya kupata wanachama wapya, na kuwashawishi hata wana CCM mashuhuri kuungana nao ili kuipatia Tanzania mwelekeo mpya, kwani ule wa CCM umeshindwa!!

  Quarz:

  Sijasema mahali hata pamoja kuwa turudi kwenye Chama kimoja isipokuwa kama kuwepo kwa vyama vingi dhaifu na visivyo na mwelekeo ni sawa na kuwa na chama kimoja! Jukumu la vyama upinzani siyo kukosoa chama kilichoko madarakani (of course, ni sehemu ndogo ya majukumu yake). Jukumu kubwa la chama chochote cha upinzani ni hatimaye kuchukua hatamu za uongozi wa nchi na kutengeneza sera za kuongoza Taifa. Ndiyo sababu nimeuliza wapinzani wa Tanzania kweli wanaweza kuwa ni wakombozi wa Taifa letu? Sijauliza kama wanaweza kuwa wakosoaji wa Taifa letu!

  Mimi hapa nawasaidia kimawazo ya jinsi gani vyama vya upinzani vinatakiwa kujijenga na kujiimarisha. Baadhi ya hoja ninazojenga, siyo kusudio langu kuipigia debe CCM bali kuwapa nafasi wapinzani wanaopitia humu wajue jinsi baadhi ya Watanzania wanavyowafikiria na hivyo kuchukua mikakati ya kuwashawishi kuwaamini. Hadi hivi sasa hakuna aliyenijibu angalau kwa kiduchu kuniambia ni kwa nini tuwaamini wapinzani badala ya CCM. Kung'ang'ania kusema CCM imeoza na haifai haitoshi! Tuambieni kwanini nyinyi mnafaa na hamjaoza?!!
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Choka mbaya na mawazo zembe
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jan 9, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  You know what, I thought I could engage you intellectually and honestly, it seems that you are not at par with me and in fact, you are well below my league. So from now on I would not lower myself to respond to your postings anymore. My back hurts. It might take time for you to get where I am so keep trying.
   
 9. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2007
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Pole Mzee MKJJ!
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jan 9, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu,

  Jamani msitake kuliharibu jina la Chadema!... ikiwa ndio mpango wenyewe ni huu basi sidhani kama mtafika huko muendako. Yaani mnatoa majibu kama ya wana CCM. Nyie ndio mlosoma na wenye akili wengine wote ngumbaru!! - Ya nini kuwaona waandishi kuwa wajinga wanapotoa hoja zao..

  Nitawakumbusheni kuwa hapa hoja ndio inayozungumza... Jibu kwa hoja na sio Mzee Mwanakijiji kuwa hoja!...

  Ameuliza swali muhimu sana, na kila nchi vyama vya upinzani hutoa ahadi zao kwa kuonyesha mbinu na vipaumbele vyao kwa miaka mitano ya kwanza.

  Demokratic wameshinda kwa sababu wamewahakikishia wananchi kuwa their first priority - Ni kuwarudisha vijana wao nyumbani - period. Tena hata baadhi ya Republican walioshinda walijitengua na Bush na wao kudai kuwa watapiga kura kupinga kuendelea kuwa na majeshi yao Iraq...

  Hii ndiyo sababu kubwa iliyofanya Demokratic washinde na sio Kumpinga Bush tuuu bila kutoa suluhisho la makosa ya Bush!..
  Ni kweli kabisa hata mimi napenda sana kujua jinsi gani mtakavyoweza kubadilisha maisha ya wananchi kwa miaka mitano ya kwanza.

  Kumbukeni sio wote humu ni Chadema wengine hatufahamu kabisa mpangilio wa vipaumbele vyenu kiuchumi... mathlan majimbo halijanivutia. sasa nikupeni kura yangu wakati sikubaliani na yale mnayokusudia kuyafanya?..

  Vijana wa Chadema ikiwa hamna jibu basi yaacheni wazi tumsubiri huyo J.J Mnyika au Zitto watupe darasa hapa, sio kumshambulia mtu kama Mzee Mwanakijiji kupotosha hoja!...
   
 11. M

  Mgumu Senior Member

  #11
  Jan 9, 2007
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji unanichanganya umeuliza swali halafu unatoa hitimisho wewe mwenyewe, ungejenga hoja halafu usubiri majibu ya wanabodi.

  Kwanza unatakiwa kujua mpinzani ni nani, kisha ungetoa hitisho, kwa taarifa yako hata ndani ya vyama kuna upinzani, ndio maana CCM ilikuwa na wangombea 10 wakitafuta nafasi ya uraisi wa nchi, jiulize kwanza upinzani ndani ya chama ni ukombozi, kama si upinzani ndani ya chama kwani kila mtu alikuwa na agenda zake au chama hakina agenda kuu.

  Mzee mwanakijiji usukurupuke, siku moja chama cha mapinduzi kitakuwa chama cha upinzani.
   
 12. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Wanabodi nahisi mmemuelewa vibaya Mzee Mwanakijiji. Sidhani kama anaipaka mafuta CCM au kuponda upinzani. Yeye ameweka forward hoja kuwa It seems waTZ tuna high expecations kuwa pindi upinzani uchukuapo nchi basi tutaona rapid changes. Maybe I got him wrong??

  And to my view he is very right, we shoul look on all sides of the coin, Yes we need changes on leadership and we definately we need a different party BUT ON WHAT GROUNDS??? is it bacause CCM can not perform or is it because UPINZANI can do much, much better.

  That should be our point of discussion, Ni aje upinzani utapambana na changamoto zilizopo na si tu kwa kutumia weakness za CCM. kama kweli tunaexpect changes hizi ndio idicators sahihi za kutuashiria je upinzani utamudu.

  Mimi sipingi upinzani ninaupenda sana lakini hofu ni juu ya mtazamo ya watanzania wenzangu wanavyohisi upinzani ukija basiii tumekomboka.

  Nafikirikwa hoja zetu hizi tutasaidia upinzani kuja na mbinu nyingi tena bunifu zitakazowawezesha kutuweka sawa kimawazo kuwa ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na wananchi kuleta mabadiliko.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 9, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mkandara na Kinyau, nashukuru kwa kunielewa!!

  Tatizo upinzani hautaki kukosolewa ila kinachotakiwa kukosolewa ni chama tawala tu!! Hili kwangu halikubaliki. Kama nimeweza kuikosoa CCM bila aibu wala hofu, wapinzani wasitarajie kuwa wao watafumbuwa macho kisa tu ati ni wapinzani!! Tena wao tutawamulika zaidi kwani hatuwajui, na hatujui kama tukiwapa nchi mambo yatakuwaje, maana hadi sasa sijajua watafanya nini, ni watafanya hivyo kivipi!

  Anayejua tunaomba mtuelemishe!
   
 14. M

  Mwendapole Old JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2007
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 249
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Well said my brother. I for one, cant stand people who dont understand the essence of digesting issues.

  The way i understand it, you put threw out a challenge for us to digest, analyse, discuss and then reach a conclusion-be it positive or negative

  So why are we not analysing this issue?

  Nionavyo mimi upinzani wa TZ bado mchanga sana. Baada ya kumaliza uchaguzi walikuwa wanatakiwa sasa hivi wawe busy kuandaa mikakati ya kushinda ujao. Nilitegemea wawe mstari wa mbele kukata issue hapa ili kuiweka CCM kiti moto--kukata issue kwa maana ya kuonyesha dosari zilizo ndani ya CCM na ku-propose solution..kwa jinsi hii sisi watazamiaji tunaweza ju-judge uwezo wao wa kuainisha mambo na kusaidia wa-TZ Sasa kama suala ni kukosoa tu, si hata wazee kule kijijini wanaweza kufanya..come up with concrete facts, datas,analysis and propose viable soulutions..tusika kukashifiana, hii haisaidii mtu..na kama MJJ haelewi basi mwerleweshe kwa hoja..hii ndio kuelimishana..The way things are going, tutawaona wapinzani wamekaa kimya hadi kampeni zianze ndio nao waanze..this is not the way to get to the state house.

  Mi nashauri wapinzani waji-organise, waweke mikakati yao kama upinzani na wala sio kama chama kimoja kimoja; sipendi kuona wagombea urais 6,au 7 kutoka vyama vidogovidogo vya upinzani, hii ni kuirahisishia kazi CCM Its time you people come together as your counterparts in Kenya did.

  MJJ, hata mimi siamini kuwa katakapokuwa kama NARC watafanya miujiza, no way, we all know that Rome was never made in one day..It took 45 yrs for CCM to get us where we are, yet we have a long way to go, sembuse chama kipya!

  Believe me, hata wapinzani wakipewa madaraka leo; tutalia kuliko tulivyolia na Richmonduli..Leo tunajadili CHADEMA as a family business, na bado hawana madaraka, je wakipata itakuwaje? mpaka wakina Mtei, Mbowe etc. na wakwe zao wote wapatiwe post hii forum si itakuwa ime-jam kwa complaints?

  Lets tackle issues seriously..and as I said elsewhere..kama mtu hana hoja asome za wenzake anyamaze asilete kashfa, hapa sio mahali pake
   
 15. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Well said Mwendapole. Issues should be tackled seriously na sio kwa kashfa.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jan 9, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tatizo, linakuwa kama hawajui kudiscuss issue! hapo ndipo tuna tatizo.
   
 17. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lazima wakubali kukosolewa, ndiyo sehemu ya utamaduni wa demokrasia wanayoitetea. Lakini hawapaswi kukubali kupotoshewa ujumbe unaowahusu. Nadhnai hapo ndipo wanapowaka, kwa sababu kwa miaka mingi wamekuwa victims wa propaganda za CCM. Hivyo wanapojibu mapigo wanakuwa wanataka kuweka records right, si kukataa kukosolewa.

  Au domo la CCM hulijui wewe? Na bahati mbaya wao hawapambani na CCM tu, wanapambana pia na dola kwa kuwa inatumiwa vibaya; badala ya kuwalinda watanzania inawalinda viongozi wa CCM. Ndicho kisa cha wapinzani kuja juu. Kama kungekuwapo level ground hata yasingetokea.

  Wanapambana na upotoshaji ama wa makusudi au wa kutokujua!!!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 9, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kichwamaji, level ground is not given as a gift but is taken as a right! Haitoshi kujaribu kuweka rekodi straight kwa maneno bali pia kwa kutumia nafasi zilizopo kujingea hoja katika jamii.
   
 19. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #19
  Jan 9, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni bahati mbaya kwamba sijapata nafasi ya kupita hapa kwenye jarida letu tangu jana. Pamoja na michango katika mada zilizokuwepo, nimekutana na hii thread mpya ya Mh. Mzee Mwanakijiji.

  Niliamua kuanza kuisoma hii maana huwa namumini sana huyu mheshimiwa katika kuibua mambo kwa lugha nyepesi hadi kwa lugha ya mbwembwe ya mazingaombwe na ushairi! Lakini nasikitika kwamba huyu mheshimiwa sijui kitu gani kimetokea hapa maana katika siku za karibuni kweli amebadilika; sio Mwanakijiji niliyemjua. Naanza kujiuliza hivi ni yeye au kuna mtu amevamia jina lake. Maadamu hajakanusha kwamba sio yeye itabidi niendelee kuamini tu kuwa ni yeye. Labda tu ameokoka. Basi ngoja nami nikabiliana na huyu mlokole wetu mpya.

  Kwanza, hakuna hata sehemu moja popote pale katika jarida hili, kwenye vyombo vya habari, katika sera au katika mikutano ya hadhara ambapo wapinzani wamewahi kusema kuwa wao wakiingia madarakani basi matatizo yote yatakuwa yamekwisha. Ndio nasema huyu mheshimiwa labda ameokoka kwa sababu sio kawaida yake ku-make sweeping statements namna hii.

  Wanachosema wapinzani ni kuwa CCM imeirudisha nchi nyuma sana. Hatupigi hatua, hasa katika kipindi hiki cha JK. Mifano ipo wazi kabisa kuonesha kuwa hatuendi mbele kuanzia kwenye vigezo vya takwimu za kiuchumi za kitaalamu (macroeconomic indicators) kama vile kukua kwa pato la taifa, thamani ya shilingi, n.k. hadi kwenye maisha ya kila siku ya mtanzania.

  Kwa mfano takwimu za leo zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi wa Taifa umeshuka katika kipindi cha mwaka mmoja cha JK. Thamani ya shilingi imeshuka kuliko maelezo tangu hao wasanii waingie madarakani. Katika maisha ya kawaida, karibu kila bidhaa muhimu imepanda zaidi ya mara 100 katika kipindi cha mwaka mmoja cha ndugu yetu JK. Kwa mfano sukari ilikuwa inauzwa katika ya sh. 800-1200 hadi Mkapa anaondoka; sasa hivi inauzwa kati ya sh. 2400-3600! Hivi ni baadhi ya viashirio kuwa CCM wanaendesha serikali vibaya.

  Sitaki kurudia mambo ya mikataba ya umeme. madini, rushwa, n.k. Haya hata wewe umekiri katika mawasilisho yako japo kwa kebehi. Sijui kwamba kama ni tatizo au la, hiyo nakuachia mwenyewe.

  Kikubwa zaidi ambacho tunapigia kelele serikali hii ya chama cha majambazi ni uongo. Kwa kipindi cha chini ya mwaka mmoja serikali ya JK imeongopa zaidi ya mara tano. Mbili kati ya hizi ni muhimu kuzitaja:

  i)Rais mzima alidanganya wananchi kuhusu umeme wa Richmond kuwa ungeanza Octoba. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza Rais kusema uongo bila aibu katika historia ya nchi yetu. Yaani hata hakuwahi kujutia
  ii) Serikali ya CCM wamedanganya mara tatu kuhusu mradi wa mabasi yaendayo kasi. Kwanza walisema ungeanza Agosti 2006; halafu wakasema utaanza January 2007. Sasa leo wamesema utaanza March 2009 karibu na uchaguzi mkuu wa 2010!

  Sasa katika mambo yote haya unataka wapinzani wasisema. kazi ya nini basi? Kwa hivyo wanachosema wapinzani ni kuwa nchi haiendi mbele kimaendeleo. Hi ni kwa sababu alipoiachia Nyerere, Mwinyi akaja akaturudisha nyuma, akaja Mkapa akaturidisha nyuma kutoka pale alipotuachia Mwinyi. Huyu kaka yangu JK ndo inaonekana anaturudisha nyuma tena kwa kasi mpya ya ajabu. Ndiyo, tutasemaje kama ameweza kuongeza deni la nje kwa $385milion chini ya mwaka mmoja katika kipindi chake cha uongozi? Halafu unataka tumpigie makofi, kwa yepi hasa?

  Katika matatizo haya, wapinzani hatusemi eti tutayamaliza kama ukungu. Tunachosema ni kuwa: 1) Hatutakuwa wanafika kwa kuwapa wananchi ahadi za ghiliba ili watupigie makofi. Tutasema kile ambacho tunataka kukifanya na ambacho tuna uwezo nacho. 2) Tutaweka misingi imara ya demokrasia ili kwamba wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Na hapa ndipo palipo na matatizo. Viongozi wa CCM wanajua wapo juu ya sheria; wanachosema wao basi kinatosha. Ndio maaana mikataba ya maana wanasaini kisirisiri lakini Taifa zima linaumia.

  Mambo muhimu yanayotakiwa kwenye katiba hawataki kuyaweka maana hawataki kujifunga. Sasa nchi zozote zisiongozwa kidemokrasia lazima ziishie ilipoishia CCM. Ni ghiliba mtindo mmoja; hata mtu akiteuliwa UN wanachukua sifa wao. Mtu akipata scholarship ya kusoma nje wanasema ni kazi ya CCM. Watu wanahangaika na msongamano hakuna barabara Dar, wao wanasema eti kwa kuwa wameleta maendeleo kwa kasi mpya hadi magari yamejaa barabara hazitoshi! Yaani ni usanii tna ghiliba tu ndo kinachoendelea. Kwa mtindo tusifie kitu gani hasa?

  Kwa kifupi, hakuna njia ya mkato katika kuiletea nchi yetu maendeleo maana uharibifu uliofanyika ni mkubwa. Lakini tunahitaji kupiga hatua, na tuonekana kwamba tunapiga hatua. Sasa hivi hatupigi hatua, na ushahidi upo kedekede. Tukisema tusionekana kwamba eti sisi tunafikiri tutamaliza matatizo kama ukungu.

  Usiwalishe wapinzani maneno. I believe you are not playing part of CCM gimmicks and manipulations!
   
 20. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ukweli usiopingika kuwa walio wengi wanaamini hivyo ila ukweli ni kwamba CCM imetusaidia sana na kutufikisha hapa tulipo,ww fanya tathmini shule ya msingi umelipa Tsh 200/= kwa mwaka je fedha hii inatosha kumlipa mwalimu anayekufundisha kwa mwezi?jibu hapana basi serikali hii ya CCM tunayoichukia ndio inayojitoa muhanga kwa kuwalipa walimu,ila ni kwamba huwezi pendwa na wote na kuchukiwa na wote
   
Loading...