Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Swali zuri sana Mkuu
Sijawahi kuacha kwenda kanisani kutubu dhambi zangu maana kwa namna moja au nyingine huwa tunamkosea Mungu pasipo kutambua, pamoja na kuwaombea ndugu/familia/marafiki zangu wote kwani Mungu ni mwingi wa rehema na haishiwi rehema na uwezo wa kusamehe ni mwenye huruma sana kwa waja wake na wote wenye Imani,Pili Sijawahi kuacha kutoa sadaka na fungu la kumi,Tatu na Mwisho nimefunga ndoa ya kikristo na wanangu wawili wamebatizwa kanisani.

Umebarikiwa Rural Swagga
 
nakumbuka tulivotimuliwa UD halafu kitaa kitambo kinoma, one day sina hata nauli ya kuelekea geto(mbezi ya kimara) najiandaa kutembea na mguu nkakutana na mshkaji akanipa 500, bila kuomba wala nn yaani hapo ndipo unapoamini mungu yupo

au una nauli ya kwenda mjini na kurudi halafu konda anasahau kukudai nauli
yaan hapo ndio napafurahia namuona konda ka Malaika
 
Msweet .... Daaaah! Nimependa huo ujumbe "VITA HII HAITAISHA MPAKA NIMETANGAZWA MSHINDI" Bonge moja la meseji ambayo kwa watu makini tunazidi inatujaza tumaini kubwa mnoo.

Na ndicho kilichotokea..... Trust me ......!!!!
 
Kwa mtu ambae hajawahi kupitia hali mojawapo kati ya hizo hawezi kuamini....Ila mimi nilishapitia hata pesa ya pipi kifua haionekani.....Na elimu yangu ya chuo kikuu niliosha magari,niliuza bangi,nilikaba,kinyozi etc....(tena nchi ya watu) Na kanisani sikuwahi kukosa nilimuomba sana Mungu sikuacha hata siku moja.Huwezi kuamini leo hii nakula pipa mpaka mikanda imenitoa sugu..Na niko na nidhamu iliyotukuka ya fedha.Kwa kifupi maisha ni mazuri boss of my own company/business...Even hustlers wish they had a hustle like mine.Respect to all the hustlers out there

Hongera sana kaka Rural Swagga .... Nimependa hapo kwenye nidhamu iliyotukuka ya fedha.... Tungefurahi sie vijana wenzio utukumbushe tena na tena bila kuchoka mambo kadhaa kuhusiana na hilo.... Tujikague zaidi na kuboresha tulipojisahau. Asante sana Kaka.
 
Naamini kila binadamu anapitia mapito ila yanatofautiana.Ila mungu humpitisha mja wake katika pito flani. Naamini hata pito ninalopitia ntapitishwa wakati ukifika
 
Kwanza nmeshusha pumzi aiseeeee,maisha yana changamoto sana sio siri,nakumbuka wakati naanza tu kujitegemea nkafanya kazi km miezi nane Kampuni ikapunguza wafanyakazi kwa kudai ukata umeikumba Kampuni aiseee zile nyakati sitazisahau ,mtt anatakiwa kwenda shule sina kazi ,nadaiwa kodi ya nyumba khaaa ,nilikuwa nalia ,ukienda kwenye maofisi ya watu kuomba kazi unakutana na karaha tupu,ila Mungu wetu ni mwema kamwe hawezagi kutuacha aiseee
 
The world is not fair!!
Ila jamani usiombe kufilisika tena bora ubaki na huo umaskini wako uliozoea kuliko kuzishika afu zikaja kupeperuka utajuta!
Kuna watu tulichezea maisha hii nchi hii ilifikia mtu akilalamika hali ngumu ya maisha unamshangaa huyu jamaa niaje!
ila sasa ndo unaona kwann hali ni tete asubuhi unajibonda mihogo unavuta ndefu hadi usiku unajibonda ugali kachumbari unalala lazma uombe kifo
 
jamaa aliparalyze mwili mzima miez michache kabla hajagraduate MD(muhas)...jamaa alikua mtu poa sana aisee kuumwa kwake ghafla kulituskitisha wengi...lakin Mungu mwema baada ya mwaka na zaidi wa kuugua sasa anaendelea vizuri sana i hope atarud skuli soon....tusiache uomba wakuu
 
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.

Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)

Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.

Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.

Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.

Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.

Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.

Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.

Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.

Natumia muda kuwaombea maadui

f077592e4c5aa05c1d2e35ac99a56ca1.jpg
Maombi ni mazuri! Usikate tamaa, ila niushauri tu. tenga mudapia wakutafuta kazi ili ufanye yote mawili kwa pamoja usielemee sana maombi. All in all utakuja kuinuliwa na utaikumbuka siku ya leo!
 
Kuna mahali inafika unaona kama dunia haitaki ushirikiano nawe,unaona wote ni kama wamekutenga hakuna anaejali matatizo yako hata wale wa karibu yako hawakuoni.

Unabaki wewe na Mungu wako tu,ni kipindi kigumu kwakila mtu. Tumepita na tunaendelea kupita kwenye changamoto mbalimbali....

Muhimu ni kua karibu na Mungu zaidi na atakuvusha salama.
Hapo ndio kila mmoja humkumbuka muumba wake. Kumtegemea mwanadamu ni kubaya sana
 
Back
Top Bottom