Je kwanini sherehe nyingi za harusi hufanyika usiku?

Je kwanini sherehe nyingi za harusi hufanyika usiku?

Sherehe za usiku wa manane siziwezi. Muda wangu wa mwisho kwenye sherehe ni saa nne usiku. Zaidi ya hapo watabaki waendelee waliozoea kukaa hadi usiku wa manene. Sipendi kabisa sherehe za usiku mwingi.
 
Mambo kibao ukumbini yaani hadi maharusi wanatoka wamechoka hoi hakuna kung'ata tena
ule usiku wa nyamnyam
fulu mawazo.
 
Yaani wewe mlokole unataka twende harusini tukale nyama na kunywa bia saa tano asubuhi? Hujitambui wewe. Kama harusi yako unataka kuwapa watu chai na maandazi kafanyie nyumbani kwako, na hatuji!
Siyo suala la ulokole mkuu, Bali ni suala la kujali muda na kuepusha kurefusha mambo bila sababu za msingi , hivyo vitu vinaweza kuliwa mapema Tu bila shida mbona
 
Watu wengi mchana bado wapo wanawatumikia waajiri wao.
Inawezekana mkuu, lakini matukio mengi ya sherehe yanafanyika mwisho wa wiki , wengi wanakuwa na nafasi ya kuhudhuria mapema
 
Ili tunaotoa mchango laki mbili watuwekee shingo ya kuku
 
Mchana muda wa kutafuta pesa, usiku ndio tunakua free sasa..!!
Hii ni kwa waalikwa, na unajua shughuli ni watu, hivyo mchana haiwezi kunoga kibongo bongo..
Mkuu naona ni suala la mazoea Tu, shughuli kunoga haihitaji Giza Ili inoge ! Inaweza kufanyika mapema Jioni au mchana na bado ikafana
 
Kwamba wengi wanapendelea usiku ili ku limit idadi ya wahudhuriaji mkuu.?
Zaidi ni uchoyo na ubinafsi kulleta matabaka kubagua maskini , Kuondoa hamasa ya ndoa na harusi kwa watoto na vijana wanaponaguliwa kushiriki nk nk
 
Mkuu naona ni suala la mazoea Tu, shughuli kunoga haihitaji Giza Ili inoge ! Inaweza kufanyika mapema Jioni au mchana na bado ikafana
Hatusemehi kunoga, tunasemea ushiriki wa watu nyakati za mchana wengi wapo kwenye mishe zao (Kwa wageni waalikwa) tofauti na wenyeji wao wanakua washapanga ratiba zao mapema.
 
Hizi harusi za usiku nyingi ni ushenzi na uhuni mtupu. Kwanza ni harusi za kibaguzi na kichoyo, kuna mavazi ya kikahaba wanavaa wanawake, ni full ulevi. Harusi safi hufungwa mchana na sherehe yake ni mchana peupe bwana na bibi harusi wapate muda wa kwenda kuzinduana mapema na bi harusi aamke mapema alfajiri tayari kuwajibika kwa mambo ya nyumbani kwake
 
Hakika Giza Siyo zuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom