Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 2,113
- 3,975
Hadithi ni tafsiri ya hadithi The Ransom of the Red Chief.
Kulikuwa na mji huko uliokuwa sehemu tambarare kama chapati, uliitwa Summit. Wakazi wake walikuwa wakulima waungwana na walioridhika na maisha.
Mimi na Bill tulikuwa na mtaji wa jumla ya dola mia sita, na tulihitaji dola elfu mbili zaidi ili kukamilisha mpango wetu wa utapeli kwenye mji mmoja huko magharibi ya Illinois. Tuliongea changamoto yetu hiyo mbele ya hoteli. Tulijiambia kuwa mapenzi kwa watoto yana nguvu sana kwenye maeneo ya vijijini, kwa sababu hiyo na nyinginezo, mpango wa utekaji unaweza kufanikiwa zaidi kwenye maeneo hayo kuliko maeneo yaliyo karibu na magazeti ambayo hutuma waandishi wa habari kupeleleza na kufanya watu waanze kuongelea mambo yaliyotokea.
Tulifahamu kuwa mji wa Summit hauwezi kutuletea upinzani mkubwa zaidi ya polisi wadogo, na labda pengine mbwa kadhaa wavivu na maneno makali kutoka gazeti la Mkulima. Kwa hiyo mambo yote yalionekana yako sawa.
Tulimchagua mtoto wa pekee wa raia mmoja maarufu aliyeitwa Ebenezer Dorset kama mhanga wetu. Bwana huyo alikuwa anaheshimika na mtu wa msimamo, alikuwa ni mtoa mikopo ya nyumba, alikuwa kauzu ambaye hakuona aibu kuacha sahani ya michango ipite bila kuweka chochote, na hakusita kuwafilisi walioshindwa kumlipa. Mtoto wake alikuwa ni mvulana wa miaka kumi aliyekuwa na madoa madoa usoni, na nywele zake zilikuwa na rangi nyekundu. Mimi na Bill tulikubaliana kuwa Ebenezer atatoa fidia ya dola elfu mbili mara moja kirahisi, lakini ngoja nikusimulie ilivyokuwa.
Kama maili mbili hivi kutoka mji wa Summit kulikuwa na kilima kidogo kilichokuwa kimesongwa na miti ya mierezi. Upande wa nyuma wa kilima hiki kulikuwa na pango. Humo ndimo tulihifadhi mahitaji yetu.
Jioni moja baada ya jua kuzama tulifika mbele ya nyumba ya Mzee Dorest kwa gari la kukokotwa na farasi. Mtoto wake alikuwa barabarani akimtupia mawe mtoto wa paka aliyekuwa ng’ambo ya nyumba yao.
“Mtoto!” aliita Bill. “Ungependa kupata pipi na kupanda gari?”
Mvulana yule alirusha kipande cha tofali kilichompata Bill sawia kwenye jicho.
“Hili litamuongezea mzee wake dola mia tano zaidi,” alisem Bill.
Mvulana yule alipambana kama dubu; lakini mwishowe tuliweza kumlaza garini na kuondoka. Tulimchukua mpaka kwenye pango na nikamfunga farasi kwe. Baada ya giza kuingia nilirudisha gari kwenye kijiji tulikoliazima, umbali wa kama maili tatu kisha nikarudi mlimani kwa mguu.
Bill alikuwa akijifunga plasta kwenye majeraha yake. Moto ulikuwa unawaka kwenye muingilio wa pango, na mvulana alikuwa akiangalia kahawa iliyokuwa ikichemka. Manyoya mawili ya ndege yalikuwa yamechomekwa kwenye nywele zake nyekundu. Nilipoingia alinionyeshea kijiti na kusema:
“Umelaaniwa wewe mwenye sura iliyopauka. Unathubutuje kuingia kambi ya Chifu Mwekundu, mtawala wa nyika?”
“Sasa ametulia,” alisema Bill huku akikunja suruali yake na kukagua majeraha zaidi kwenye ugoko wake. Tunaigiza kama Wahindi. Tunafanya onyesho. Mimi naigiza kama Mzee Hank, mtega wanyama na mateka wa Chifu Mwekundu, na kutakapokucha nitakatwa ngozi yangu ya kichwa. Hakyanani mtoto huyu anapiga mateke!”
Ndiyo ilivyokuwa, mtoto yule alionekana kufurahia kabisa maisha. Furaha ya kuweka kambi pangoni ilimfanya asahau kuwa yeye ni mateka. Mara moja akanipa jina Jicho la Nyoka—Mpelelezi. Na akatangaza kuwa asubuhi mashujaa wake wakirudi kutoka vitani nitafungwa mtini na kuchomwa moto.
Baada ya muda kidogo tukapata chakula cha usiku, alijaza nyama, mkate na chachandu mdomoni na kuanza kuongea. Hotuba yake ilikuwa kama hivi:
“Ninafurahia hili. Sijawahi lala kambini, lakini nilikuwa na mnyama niliyemfuga, na kwenye sherehe yangu ya kuzaliwa ya mwaka jana nilikuwa nina miaka tisa. Nachukia kwenda shule. Panya walikula mayai kumi na sita ya kuku wa shangazi yake Jimmy Talbot. Kuna Wahindi halisi kwenye pori hili? Nataka chachandu zaidi. Miti inayojongea ndiyo inafanya upepo uvume kwa kelele? Tuna watoto wa mbwa watano. Hank nini kinafanya pua yako iwe nyekundu. Baba yangu ana pesa nyingi. Je, nyota ni za moto? Jumamosi nilimchapa Ed Walker mara mbili. Sipendi wasichana. Huwezi kukamata vyura mpaka utumie kamba. Mafahari hutoa kelele zozote? Kwa nini machungwa ni ya mviringo? Mna vitanda vya kulalia kwenye pango hili? Amos Murray ana vidole sita mguuni. Kasuku anaweza kuongea lakini nyani na samaki hawawezi. Vinahitajika vingapi ili kufika kumi na mbili?
Kila baada ya dakika kadhaa alikuwa akikumbuka kwamba yeye ni Mhindi msumbufu, alichukua bunduki yake ya kijiti na kunyata kuelekea kwenye mdomo wa pango, kuangalia wapelelezi wa Wazungu Mara kwa mara alikuwa akipiga ukelele wa vita uliomfanya Hank mwindaji atetemeke. Mvulana yule alimnyanyasa Bill tokea walipokutana.
“Chief Mwekundu,”nilisema. “Ungependa kwenda nyumbani?”
“Kufanya nini?” alisema. “Sifurahii chochote nyumbani. Nachukia kwenda shule. Napenda kukaa kambini. Hautanirudisha nyumbani, si ndiyo Jicho la Nyoka?”
“Siyo sasa. Tutakaa kidogo pangoni.”
“Hapo sawa!” alisema. “Sijawahi kuwa na furaha kama hivi maishani.”
Tulienda kulala kama saa tano usiku. Tulitandaza chini blanketi pana na kumuweka Chifu Mwekundu kati yetu.
Hatukuwa na hofu kuwa atakimbia. Alituweka macho kwa saa tatu. Akirukaruka na kuchukua bunduki yake na kupiga kelele kwenye masikio yangu na ya Bill hasa pale sauti za vijiti au majani nje ya pango vilipofanya fikra zake za kitoto ziwazie ujio wa genge la wahalifu. Hatimaye niliweza kulala usingizi wa mang’amung’amu, niliota nimetekwa na kufungwa mtini na haramia katili aliyekuwa na nywele nyekundu.
Mapema asubuhi niliamshwa na kelele za kutisha kutoka kwa Bill. Hazikuwa kelele za kuunguruma au kung’aka kama ambazo unaweza kutegemea kutoka kwenye viungo vya sauti vya mwanaume. Zilikuwa kelele za kutia aibu kama ambazo wanawake hutoa wanapoona mizuka au viwavi. Ni jambo la kutisha sana kumsikia mwanaume mnene na mwenye nguvu akipiga kelele bila kujizuia ndani ya pango, wakati wa asubuhi.
Niliamka haraka haraka kuangalia nini kimetokea. Chifu Mwekundu alikuwa amekaa kifuani pa Bill huku mkono mmoja ukiwa umezikusanya nywele za Bill. Kwenye mkono mwingine alikuwa ameshika kisu kikali ambacho tulikuwa tunakitumia kukatia nyama. Alionekana anafanya bidii kabisa kujaribu kuchuna ngozi ya kichwa ya Bill, kama tu alivyosema atafanya jioni iliyopita. Nilimnyang’anya kisu na kumuweka pembeni. Lakini kutokea hapo ujasiri wote ukawa umemuisha Bill. Alilala upande wake lakini hakuweza kulala tena muda wote mvulana yule alipokuwa nasi. Niliweza kulala kidogo, lakini jua lilipokaribia kutoka nilikumbuka kuwa Chifu Mwekundu alisema kuwa jua litakapotoka nitafungwa mtini na kuchomwa moto. Sikuwa na wasiwasi wowote; niliamka na kuwasha kiko changu kisha nikajiegemeza pembeneni ya jiwe.
“Sam mbona unaamka mapema sana?” aliuliza Bill.
“Nani, mimi?” nilisema. “Ahh, ninasikia maumivu begani. Nadhani kukaa itasaidia.”
“Muongo,” alisema Bill. “Unaogopa kuwa utachomwa mtini jua litakapotoka, unaogopa atatekeleza ahadi yake. Na bila shaka atafanya hivyo iwapo atapata kiberiti. Hali si hali Sam, unafikiri kuna mtu atalipa pesa ili kumrudisha nyumbani nunda kama huyu?”
“Hilo halina shaka,” nilisema. “Watoto watundu kama huyu ndiyo ambao wazazi wanawapenda na kuwadekeza. Haya, wewe na Chifu amkeni na muandae kifungua kinywa, mimi nitaenda kwenye kilele cha mlima na kuchunguza yanayoendelea.”
Nilipanda juu ya kilele cha kilima na kuangaza huku na kule. Nilipokuwa napanda nilitarajia kuwa nitaona kundi la wanakijiji wakiwa na miundu na nyuma za kuchotea majani, wakiwasaka watekaji. Lakini nilichoona ni hali tulivu na mtu mmoja akilima shamba lake kwa jembe la kukokotwa na nyumbu. Hakukuwa na pilikapilika zozote, wala wajumbe wakienda huku na kule wakibeba habari za wazazi waliohamaki. Eneo lile la Alabama lilijaa amani na utulivu. “Pengine”nilijisemea, “Bado haijajulikana kuwa kuna mbwamwitu wamenyakua kondoo. Mungu wasaidie mbwamwitu!” Nilishuka kilimani ili kwenda kupata kifungua kinywa.
Nilipofika nilimkuta Bill amebananishwa ukutani huku akihema kwa nguvu, mvulana yule alikuwa akitishia kumponda na jiwe lenye ukubwa wa tunda la kokoa.
“Ameniwekea kiazi cha moto mgongoni.” Alisema Bill. “Na kisha akakisaga kwa miguu yake. Nami nimemzaba makofi. Hivi Sam una bunduki?”
Nilimnyang’anya mvulana jiwe na kusuluhisha ugomvi wao. “Nitakumaliza,” Mvulana alimwambia Bill. “Hakuna mtu amewahi kumpiga Chifu Mwekundu na asidhurike. Kuwa makini sana.”
Baada ya kifungua kinywa mvulana alichukua kipande cha ngozi kilichofungwa kwa kamba kutoka mfukoni mwake na kukifungua huku akielekea nje ya pango.
“Anataka kufanya nini?” alisema Bill kwa wasiwasi. “Unadhani anaweza kukimbia?”
“Sidhani,” nilisema. “Haonekani kama anapendelea kukaa nyumbani. Lakini inatakiwa tuanze kufanya mipango ya kupata fidia. Inaonekana mji haujashtushwa kabisa na kupotea kwake, au pengine bado hawajui kama ametoweka. Ndugu zake watakuwa wanadhani kalala kwa shangazi au kwa jirani fulani. Vyovyote vile, leo lazima watamtafuta. Usiku wa leo itabidi tupeleke ujumbe kwa baba yake na kudai dola elfu mbili ili kumrudisha.”
Wakati tukiendelea na maongezi tukasikia mlio wa kivita-kama ule ambao Daudi atakuwa alifanya alipompiga Goliati. Ulikuwa ni mlio wa kombeo ambalo alikuwa amelitoa mfukoni mwake. Wakati huo alikuwa akilizungusha kichwani mwake.
Nilikwepa, nikasikia mshindo, pia nikamuona Bill akishusha pumzi kama vile farasi aliyevuliwa tandiko. Jiwe lenye ukubwa wa yai lilikuwa limempata Bill nyuma ya sikio lake la Kushoto. Alipepesuka na kudondokea kwenye moto, karibu ya sufuria lililokuwa na maji ya moto kwa ajili ya kuoshea vyombo. Nilimuinua na kumwagia maji ya moto kichwani kwa muda wa nusu saa.
Basi Bill aliketi, na huku akiugulia maumivu ya sikio alisema, “Sam, unajua ni mtu gani wa kwenye biblia ninayempenda sana?”
“Tulia kwanza,” nilisema. “Utakuwa sawa muda si mrefu.”
“Mfalme Herode,” alisema Bill. “Hautaondoka na kuniacha hapa peke yangu, sivyo?”
Nilienda nje na kumtikisa mvulana yule kwa nguvu.
“Kama hautatulia,” nilisema. “Nitakupeleka nyumbani sasa hivi. Utatulia au hautatulia?”
“Nilikuwa natania tu,” sikupanga kumuumiza Mzee Hank. Lakini kwa nini alinipiga? nitatulia kama hautanipeleka nyumbani na ukiniruhusu kucheza kama skauti
“Mi siujui huo mchezo,” nilisema. Wewe na Bwana Bill ndiyo mtaamua. Ndiye mtashinda naye. Mi natoka kidogo, kwa ajili ya biashara. Haya njoo ufanye urafiki naye na kumuomba msamaha kwa kumuumiza, la sivyo unaenda nyumbani sasa hivi.”
Niliwashikanisha mikono na Bill kisha nikamchukua Bill pembeni na kumwambia kuwa naelekea Poplar Cove, kijiji kidogo kilichokuwa umbali wa maili tatu toka kwenye pango, naenda kuchunguza nini kinajili juu ya utekaji uliofanyika huko Summit. Pia nilifikiri itakuwa vizuri kuandika barua kwa Mzee Dorset siku hiyo, barua ya kuhitaji fidia na kutoa maelekezo ya jinsi ya kuilipa.
“Unajua Sam,” alisema Bill. Nimesimama nawe bila kupepesa macho hata kwenye misukosuko-kwenye kamari, msako wa polisi, kuvamia treni na vimbunga. Sijawahi tetereka mpaka tulipomteka huyu nunda. Hutaniacha naye kwa muda mrefu, sivyo?”
“Nitarudi mida ya mchana,” nilisema. “Unapaswa kumfanya kijana afurahi na kutulia hadi nitakaporudi. Haya na tuandike barua kwa mzee Dorset.”
Basi mimi na Bill tukakaa na kuanza kuandika barua. Bill alinibembeleza sana kuwa tuweke fidia dola elfu moja mia tano badala ya dola elfu mbili. “Sidharau mapenzi ya mzazi kwa mtoto, lakini hapa tunashughulika na binadamu. Si rahisi kwa binadamu kutoa dola elfu mbili nunda kama huyu. Naona dola elfu moja mia tano ni kiasi sahihi. Ikilazimu nitaongezea inayopungua.”
Nikakubaliana naye ili kumridhisha. Tukaanza kuandika barua:
Ndugu Ebenezer Dorset:
Tunaye kijana wako, tumemficha eneo la mbali sana kutoka Summit. Itakuwa ni kupoteza kwako au kwa hata wapelelezi hodari kujaribu kumtafuta. Namna pekee unayoweza kumpata ni kwa kutumia njia hizi: Tunahitaji dola elfu moja mia tano. Pesa iwekwe saa sita usiku wa leo kwenye sanduku ambamo pia utaweka majibu yako, kama ilivyoelekezwa hapo chini. Kama umekubaliana na matakwa haya tuma majibu yako kupitia mjumbe mmoja leo saa mbili na nusu usiku. Baada ya kuvuka kijito cha Bundi kwenye njia ya kuelekea Poplar Cove kuna miti mikubwa mitatu iliyotengana kwa umbali wa kama mita mia moja. Karibu na uzio wa shamba la ngano lililoko upande wa kulia. Chini ya nguzo ya uzio iliyo mkabala na mti wa tatu kuna sanduku. Mjumbe aweke jibu ndani ya sanduku hilo na kurejea Summit mara moja.
Kama ukijaribu ujanja wowote, au ukashindwa kutimiza matakwa yetu basi hutamuona kijana wako tena.
Kama ukilipa pesa kama ulivyoelekezwa basi kijana wako atarejeshwa ndani ya saa tatu akiwa salama kabisa. Maelekezo haya ni ya mwisho, kama hautayatimiza basi hakutakuwa na mawasiliano zaidi.
WANAUME WAWILI
Nilimaliza kuandika barua hiyo na kuitia mfukoni. Nilipokuwa karibu kuondoka mvulana yule alinijia na kusema: “Jicho la Nyoka ulisema ukiondoka ninaweza kucheza mchezo wa Skauti Mweusi “Ndiyo unaweza kucheza,” nilisema. “Bill atacheza nawe. Kwanza mchezo wenyewe ukoje?”
“Mimi ni Skauti na natakiwa kwenda na farasi kuwaonya Wazungu kuwa Wahindi wanakuja. Nimechoka kuigiza Mhindi, nataka kuwa skauti.”
“Haina shida,” nilisema. “Sioni kama kuna madhara. Nadhani bwana Bill atakusaidia.”
“Ninatakiwa kufanya nini?” alisema Bill huku kimuangalia mvulana yule kwa mashaka.
“Utakuwa farasi,” alisema skauti. “Inama kwa mikono na magoti. Nawezaje kwenda bila farasi?”
“Bill unatakiwa umfanyie anavyotaka mpaka mambo yetu yatakapokaa sawa.”
Bill aliinama kwa miguu na mikono. Sura yake ilikuwa kama ya Sungura aliyenaswa mtegoni.
“Kuna umbali gani huko tuendako?” Aliuliza Bill kwa sauti ya hofu.
“ Maili tisini,” alijibu mvulana yule. “Na inatakiwa uende kasi ili tufike kwa wakati. Haya twende!”
Hapo skauti alimrukia Bill mgongoni na kumbana mbavuni kwa miguu yake.
“Sam fanya haraka. Natamani tusingeandika fidia ya zaidi ya dola elfu moja. Na wewe acha kunipiga mateke, la sivyo nitasimama nikushughulikie.”
Nilielekea Poplar Cove na kurandaranda karibu na ofisi ya posta, nikiongea na warugaruga waliokuja kufanya biashara. Mtu mmoja mwenye mandevu alisema amesikia kuwa mji wote wa Summit umekasirika kutokana na kupotea au kutekwa kwa kijana wa Mzee Ebenezer Dorset. Hicho ndicho nilitaka kusikia. Nilinunua tumbaku. Nilizuga kwa maongezi kisha nikatuma barua yangu na kuondoka. Mtu wa posta aliniambia kuwa mchukua barua atafika baada kama saa moja kuchukua barua za kwenda Summit.
Niliporudi pangoni sikuwakuta Bill na mvulana. Nilizunguka karibu na pango, na nikaita kama mara mbili hivi japo ilikuwa hatari kufanya hivyo, hakukuwa na majibu.
Basi nikawasha kiko changu na kuanza kuvuta huku nikisubiri yatakayojili.
Bada ya kama nusu saa nilisikia kelele kutoka vichakani, kisha nikamuona Bill akitokea huku akipepesuka. Nyuma yake alikuwepo mvulana, akitembea kwa makini na kunyata kama skauti, huku akiwa na mkenuo mkubwa usoni. Bill alisimama, alivua kofia na kujifuta jasho. Mvulana naye alisimama nyuma yake.
“Sam,” alianza kusema Bill. “Nadhani utafikiri labda mimi ni msaliti. Lakini sikuwa na namna. Mimi ni mwanaume mtu mzima, nina silka ya kujilinda. Lakini kuna wakati silka hiyo inashindwa kufanya kazi. Mvulana ameondoka. Nimemwambia aende kwao. Zamani kulikuwa na mashujaa ambao walikuwa tayari kufa kuliko kuchia kitu fulani walichokipenda, lakini hakuna hata mmoja wao aliyepitia mateso kama niliyopitia. Nilijaribu kuwa mvumilivu ili tutimize lengo letu lakini kuna ukomo wa uvumilivu.
“Tatizo nini?” nilimuuliza
“Niliendeshwa, maili tisini. Na baada ya Wazungu kuokolewa nilipewa mchanga kama shayiri. Na kwa kama saa nzima nililazimika kumueleza kwa nini barabara huenda na kurudi na majani ni kijani. Nakwambia ukweli Sam, binadamu ana kikomo cha uvumilivu. Nilimkwida kwenye kola na kumshusha huko bondeni. Njiani alinipiga mateke ya miguuni na kuniuma vidole.
“Lakini amekwisha kwenda,” Aliendelea kusema Bill. “Amekwenda kwao. Nimemuonyesha barabara ya kwenda Summit na kumsindikiza kwa teke. Samahani tumepoteza pesa za fidia, lakini hakukuwa na jinsi. Ilikuwa iwe hivyo au mimi niende hospitali ya vichaa.
“Bill,” Nilisema. “Kwenye familia yenu kuna historia ya ugonjwa wa moyo?”
“Hapana,” alisema Bill. “Ni malaria tu na ajali. Kwanini unauliza?”
“Basi kama ni hivyo geuka nyuma uangalie.”
Bill aligeuka na kumuona mvulana. Rangi ilimbadilika. Akakaa chini kwa kuishiwa nguvu, kisha akaanza kung’oa nyasi na kuokota vijiti. Kwa muda wa saa moja nilikuwa na wasiwasi juu ya afya yake ya akili. Mwisho nikamwambia kuwa mpango wangu ni kukamilisha biashara yetu haraka iwezekanavyo. Na kuwa kama Mzee Dorset atakubaliana na mpango wetu basi kufikia leo usiku tutakuwa tumepata pesa zetu na kuondoka. Basi Bill akachangamka kidogo na akamkubalia mvulana yule kucheza kama Mrusi kwenye vita kati ya Wajapan na Warusi.
Nilikuwa tayari nimeishaandaa mpango wa kupata pesa ya fidia bila ya kukamatwa. Mti ambao barua, na baadaye pesa vilipaswa kuwekwa ulikuwa karibu na barabara iliyokuwa na mashamba meupe pande zote. Kama polisi wangekuwa wanasubiri wangeweza kumuona mtu akija kupitia mashambani au barabarani tokea mbali. Lakini nilijiandaa. Saa mbili na nusu usiku nilikuwa nimeishafika na kujificha juu ya mti nikimsubiria mjumbe.
Muda ule ule niliowaambia kijana mmoja alifika kwa baiskeli. Aliona kasha chini ya nguzo ya uzio. Alitumbukiza karatasi na kisha akaendesha baiskeli yake kuelekea Summit.
Nilisubiri kwa kama saa zima ndipo nikajiridhisha kuwa hali ni shwari. Nilishuka mtini. Nikaichukua ile karatasi na kutokomea vichakani. Baada ya nusu saa nikawa nimeishafika pangoni. Nilifungua barua karibu na taa kisha nikaanza kumsomea Bill. Iliandikwa hivi:
Mabwana Wawili
Ndugu:
Nimeipata barua yenu leo. Kulingana na fidia mnayoitaka juu ya mtoto wangu nadhani ni kiasi kikubwa sana, na haya ndiyo majibu yangu, na natumaini mtakubaliana nayo. Mrudisheni Johnny nyumbani na mnilipe dola mia mbili na hamsini, nami nitakubali kumchukua kutoka mikononi mwenu. Mnatakiwa mje usiku maana majirani wanajua kuwa amepotea, na sitahusika na watakachofanya wakimuona mtu anamrejesha.
Wenu
Ebenezer Dorset
“Anathubutuje,” Nilisema. “Dharau gani hii?”
Lakini nilipomuangalia Bill nilikuta uso wake unaonyesha hisia tofauti kabisa.
“Sam,” Alisema Bill.”Dola mia mbili hamsini kitu gani? Hiyo pesa tunayo. Kuishi usiku mmoja zaidi na mtoto huyu kutanifanya nitarukwa na akili, unataka iwe hivyo?”
“Kusema ukweli Bill,” Nilisema. “Huyu mtoto hata mimi amenichosha. Tutamrudisha kwao, tutalipa fidia na kwenda zetu.”
Basi usiku ule tukampeleka kwao. Tulimshawishi kwa kumwambia kuwa baba yake kamnunulia bunduki na viatu, na kuwa siku inayofuata tutakwenda kuwinda dubu.
Kama saa sita hivi za usiku tukawa tumefika nyumbani kwa Dorset. Muda ambao ningetakiwa kuwa nachukua dola elfu moja mia tano kwenye sanduku chini ya mti, kama mambo yangetuendea kama tulivyopanga. Badala yake Bill alikuwa akihesabu dola mia mbili hamsini na kumkabidhi Mzee Dorset.
Mvulana yule alipogundua kuwa tunataka kumuacha alianza kupiga mayowe na kumng’ang’ania Bill miguuni kama luba. Baba yake alifanya kazi ya ziada kumbandua.
“Unaweza mshika kwa muda gani?” aliuliza Bill.
“Sina nguvu kama hapo zamani,” alisema Mzee Dorset. “Nadhani kama dakika kumi hivi.”
“Zinatosha,” alisema Bill. “Ndani ya dakika kumi nitakuwa nimevuka majimbo ya kusini, ya kati na ninakaribia mpaka wa Canada.”
Pamoja na giza lile, na jinsi Bill alivyokuwa mnene, na jinsi nilivyokuwa na mbio, lakini kabla sijamfikia tayari alikuwa umbali wa nusu maili kutoka Summit.
Unaweza kuisoma hii na nyingine nyingi ndani ya maktaba.co.tz
Mwisho
FIDIA YA NUNDA
Lilionekana kama jambo zuri, lakini subiri mpaka nikusimulie. Tulikuwa huko kusini, Alabama—mimi na Bill Driscoll tulipopatwa na wazo la kuteka mtu ili tulipwe fidia. Kama Bill alivyokuja kusema, “ilikuwa kama kichaa cha muda hivi”; lakini hatukujua hilo mpaka hapo baadaye.Kulikuwa na mji huko uliokuwa sehemu tambarare kama chapati, uliitwa Summit. Wakazi wake walikuwa wakulima waungwana na walioridhika na maisha.