Je, kuna uhusiano wa Kenya kuuza nyama Uarabuni na kupanda bei ya nyama Tanzania?

KAKA NASOKI

Senior Member
May 25, 2016
191
212
Tulisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Kenya wamepata tenda ya kupeleka nyama Uarabuni na shehena ya kwanza ya tani 500 imeshaondoka.

Kwa uelewa wangu Tanzania ndio yenye mifugo kwa wingi kuliko nchi zote East Africa, ila baada ya kupata tenda hiyo ghafla nyama Bongo ikapanda, je kuna uhusiano wowote?
 
Uhusiano upo, tanzania hatuna viwanda vya nyama ambavyo vinakidhi ubora ndio maana hata mahotel ya kitalii yanaagiza nyama nje. Kwa mikoa ya kasikazini mifugo mingi huvushwa kwenda kenya.
 
Tilisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Kenya wamepata tenda ya kupeleka nyama Uarabuni na shehena ya kwanza ya tani 500 imeshaondoka. Kwa uwelewa wangu Tanzania ndio yenye mifugo kwa wingi kuliko nchi zote East Africa, ila baada ya kupata tenda hiyo ghafla nyama Bongo ikapanda je kuna uhusiano wowote?
Mafanikio siku zote yanatesa watu wa kipato cha chini. Mungu saidia Sisi wa kipato cha chini
 
Tulisikia kwenye vyombo vya habari kuwa Kenya wamepata tenda ya kupeleka nyama Uarabuni na shehena ya kwanza ya tani 500 imeshaondoka.

Kwa uelewa wangu Tanzania ndio yenye mifugo kwa wingi kuliko nchi zote East Africa, ila baada ya kupata tenda hiyo ghafla nyama Bongo ikapanda, je kuna uhusiano wowote?
Inawezekana. Wakati corona ilivyoingia, kenya walipata deal la kusupply vegetables europe. Walikuwa wanakuja tz wananunua na kupeleka kenya, ili waweze kuongezea mzigo, ukamilike.
 
Uhusuano upo kwa hivi sasa wakenya wamejaa kwenye minada ya mifugo huku Kanda ya ziwa, wamesababisha bei kupanda sana ya mifugo ukitaka kuthibitisha hili nenda mpakani tarime,Sirari malori na malori yaliyobeba mifugo yakipitishwa hapo
 
Ndiyo

Thread Closed.
 
Mafanikio siku zote yanatesa watu wa kipato cha chini. Mungu saidia Sisi wa kipato cha chini
mhn! kama tutakuwa tayari kuvumilia njaa ya siku mbili kwa kutengeneza mfumo wa kwetu tunaweza kusogea na sivinginevyo. changamoto tulionayo watanzania hatuko tayari kubebana kwa uchanga wetu wakati wa hatua za awali. wezetu wako tayari kununua bidhaa za ndani hata kama ubora uko chini lakini sio sisi.
tupo tayari kumlazimisha mkulima aliyechuma papai lenye ubora na limechumwa leoleo kwa shilingi 1000/- tukiomba tupunguziwe kwa shillingi 500/- lakini tunapoenda supermarket tunanunua bila ubishi papai lilolo kaa wiki mbili kwa 5000/- tena lisilo na ubora.
hivyo kwa kifupi safari ni ndevu sana..
vipato vingi halali vya watu wa chini vinategemea biashara haramu za maskini wenzao bodaboda bila wadangaji hawana biashara mjini, saloon bila nyumba ndogo hakuna wateja. ni shida kwa kweli!
 
Back
Top Bottom