Ukame, gharama za Ng'ombe vyatajwa kupandisha bei ya Nyama nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Bei ya ng’ombe katika Soko la Pugu kwa wiki inayoishia Novemba 23, imepanda kwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na wiki iliyopita, hali iliyosababisha nyama kuuzwa kwa bei ya juu.

1669880317633.png

Katika kipindi cha mapitio, bei ya ng’ombe wa daraja la kwanza ilipanda kutoka Tsh. milioni 1.9 wiki iliyopita hadi Tsh. milioni 2.1 wiki hii, kulingana na bodi ya nyama nchini.

Meneja wa shughuli za masoko wa bodi hiyo, John Chasama alisema hali hiyo inatokana na uhaba wa ng’ombe unaosababishwa na kukosekana kwa malisho. Alisema bei ya ng’ombe wa daraja la pili ilipanda kutoka Sh1 milioni wiki iliyopita hadi kufikia Sh1.15 milioni wiki hii.

“Ukame umechangia kuongezeka kwa bei ya ng’ombe kwa sababu ng’ombe wenye afya sasa hawapatikani. Huwezi kuuza ng’ombe wasio na afya sokoni kwa sababu hata nyama yao haiwezi kuwa nzuri, kwa hivyo lazima uende mbali kutafuta wenye afya, ambayo gharama ni kubwa.”

Kupanda kwa bei ya ng’ombe ilibidi kulazimu walaji wa nyama kutoboka zaidi mfukoni ili kupata bidhaa hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa mifugo na mazao ya mifugo, Joel Meshaki alisema bei ya jumla ya nyama tangu Oktoba mwaka huu imepanda hadi Sh7,500 na Sh8,000 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya awali iliyokuwa ikiuzwa karibu Sh6,000 na Sh6,500.

Hiyo iliathiri bei ya reja reja ambayo matokeo yake ilipanda hadi kati ya Sh9,000 na Sh10,500 kulingana na maeneo husika.

“Mabadiliko ya hali ya hewa, yamesababisha ukame uliochangia kupungua kwa malisho ya mifugo na kupunguza ubora wa ng’ombe wanaohitajika sokoni kwa wakati. Tunatarajia bei kupanda zaidi kutokana na uhaba wa ng’ombe sokoni. Tofauti na mwaka jana, mwaka huu bei imepanda mapema, ukizingatia tunaelekea msimu wa sikukuu, kuna uwezekano bei itapanda zaidi,” alisema Meshaki.

Pia, alisema mwaka jana bei ya jumla haikufikia Sh8,000.

Bei ya juu zaidi katika mwaka huo ilinukuliwa kati ya Sh7,200 na Sh7,500.

Ng’ombe kati ya 450 hadi 500 huchinjwa kila siku katika machinjio ya Vingunguti wakati machinjio ya Ukonga huchinjwa ng’ombe 500 hadi 550 kwa siku.

Alisema katika kipindi hiki mwaka jana walikuwa wakichinja ng’ombe 550 hadi 600 katikati ya wiki na ng’ombe 650 hadi 1,000 mwishoni wa wiki.

MWANANCHI
 
Uku usukuma. Kwetu ng:eek:mbr zimeshuka bei, alisho hamna watu wanaogopa zisije kufa wanauza harka ngombe ya laki tatu unapata 180-200k
 
Back
Top Bottom