Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Mkuu cha kwanza kabisa amini kama Mungu yupo na siku ya mwisho siku ya kulipwa matendo yako yote uliyofanya Dunian ipo pia, so kuna maisha mengine baada ya kifo yapo na utayakuta...
Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?
 
Everybody knows that ^a long time^ doesn't mean forever. Does it?

You really have some splanin' to do!

Acha uvivu na ufinyu wa akili, wewe. Hoja na maswali yote yanategemea hoja na maswali yaliyopita.

Shule ulisomea wapi kwani?
Nimesema uliza swali moja ujibiwe hoja kwa hoja. Hapa unaonyesha upunguani wako kwa kuandika sana uonekane unajua wakati hujui kitu na hujui nasimamia wapi unachojua ni matusi

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Hapa kuna maswali mawili yanachanganywa na kupewa majibu tofauti kama mtoa mada mlinzi mlalafofofo alivyouliza. Swali lake lilikuwa Je kuna sehemu nyingine tunaenda na maisha kuendelea tukizikwa au Je tukizkwa maisha yanaendelea huko twendako? Jibu ni hapana kulingana na Biblia. Tukizikwa hakuna maisha yanayoendelea kama maneno ya mhubiri 9:5 na 9: 10 na iko kama Molodekai alivyosema kuwa ukifa ndio mwisho wa yote hakuna utendaji unaondelea kama alivyoambiwa ingawa hakuendelea kuwauliza maswali waliomwambia maana hawaishi hapo tu

Baada ya kifo inakuwa kama mtu aliyelala usingizi ambapo kunakuwa hakuna utendaji wowote wa mtu huyu ni mpaka atakapoamshwa ndio anaendelea kutenda.


Swali la pili linalochanganywa na la kwanza ni je, kuna maisha baada ya kifo au tumaini lolote? Kwa mujibu wa Biblia jibu ni ndiyo. Watu wote walio makabuirini wanasubiri ufufuo. Ukisoma maneno ya Yesu kwenye Luka 20:37, na barua mbili za Paulo, 1
Wakorintho 15:52, 1 Wathesalonike 4: 16 yote yanataja juu ya tumaini ambalo wanadamu wanalo baada ya kufa. Vinginevyo kama hakuna tumaini lolote la wakati ujao basi kumtumikia Mungu kwetu ni bure.

Hivyo kwa mtazamo wa Biblia
1. Je tukifa tunaendelea kuishi? Jibu ni Hapana tunaendelea kusubiri ufufuo

2. Je kuna maisha baada ya kifo? Jibu ni NDIYO kwa kuwa kuna ufufuo mbele yetu wa wote waliolala makabuirini.




Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?
Mashahidi gani hao uwazungumziao wewe? Mashahidi wa Yehova wanaamini katika ufufuo.
 
Kwahiyo wewe baada ya kusoma kuwa umetokana na nyani kama ulivyoelezwa na wakiokuletea dini yako na hiyo tamthilia ya biblia unaamini hivyo?

Au yote unayohubiliwa na wachungaji tena wengine umekuwa nao eti kwa sababu tu wamesoma biblia unaamini wayasemayo ni kweli?

Acha ujinga kwanini hizo biblia na misafu zisimtaje MUASISI wetu hata mmoja tu aliyetoa ushuhuda wa neno la MUNGU woooote ni wazungu na waarabu tu?

WHY?
 
Mkuu cha kwanza kabisa amini kama Mungu yupo na siku ya mwisho siku ya kulipwa matendo yako yote uliyofanya Dunian ipo pia, so kuna maisha mengine baada ya kifo yapo na utayakuta...
Maisha mapya yapo kwakuwa umeelekezwa kupitia biblia au msahafu?na je waliokuwepo kabla ya dini inakuwaaje.

Hizi dini zenu za michongo zilianzishwa na kuletwa na wazungu hawa hapa chini:-
 
Write your reply...kwani razalo aliefufuliwa na yesu anasemaje
Binadamu hajawahi kufufuka au kufufuliwa na binadamu mwenzake i.e.yesu

Razalo ni mzungu na yesu ni mzungu,je kuna Mwafrika aliyewahi kufufuliwa na yesu?
 
Ndio kuna hali nyingine ingawa sio maisha kama haya.Yakoje..mimi sijui lkn niko na uhakika 100% yapo
Mbwa,miti,samaki,mawe,n k pia vitakuwa na maisha mapya?

Kitu ambacho hakijawahi kutokea hapa duniani hakitokaa kitokee ndani ya maisha na kufa.

Hakuna maisha baada ya kufa viumbe vyote viliumbiwa hapa duniani hivyo vitafia hapa dunia ilipo roho na nafsi ya MUNGU aliyeviumba.

Ujinga huo umezidi kipimo.
 
Makaburi hamna watu kuna mifupa na masalia ya miili ya wafu.

Hao waliokuaminisha kuwa kunakufufuka kwa mujibu wa biblia kwanini wanashuhudia kila siku mabaki ya wafu wakarne nyingi kiasi kwamba kama kungekua na ufufuo basi hayo mabaki yangekuwa yameshafufuka kwa awamu ya kwanza na ya pili au hata ya tatu.
 
Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?
Momi naamini hakuna mwisho wa dunia ndiyo maana idadi ya watu inaongezeka kupitia kuzaliana hadi dunia ijae na si hivi karibuni.

Kinachoweza kutokea labda ni dunia kuelemewa kwa idadi ya uzito wa viumbe vinavyozaliana na kwa uwezo wa MUNGU kukatoa muujiza wowote wa mabadiliko ya uwepo wa ninadamu,hilo tu!!
 
Ndio kuna hali nyingine ingawa sio maisha kama haya.Yakoje..mimi sijui lkn niko na uhakika 100% yapo
Ndiyo kabisa,hali hiyo yaweza kuwa ni kujaa kwa dunia na kuelemewa kwa idadi ya watu kuwa kubwa na kupungua kwa viumbe wengine kama wanyama na mimea kutokana na overpopulation tukio ambalo linawezatokea baada ya miaka mingi saaaana siyo UFUFUKO !!!
 
Mimi naamini kuna Mungu na maandiko matakatifu pamoja, matukio na uumbaji ndio vinatusaidia kuamini uwepo wa Mungu na ufufuo kwa wakati ujao. Kama huna imani kuwa Mungu yupo na ana nguvu basi hata haya mengine kuzungumza nawe ni kujisumbua tu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
πŸ‘πŸ‘πŸ™πŸŽπŸ’πŸŽ–οΈπŸ†
 
Mkuu haya maswali ni muhimu sana katika harakati za kujitambua. πŸ‘πŸ‘πŸ™
 
Mkuu huwezi kutetea hoja yako kwa kutumia kitabu chenye maneno yanayotiliwa shaka na mtoa hoja!

Kama kweli Biblia ni kitabu cha Mungu kwanini kisiwepo baada ya uumbaji kama manual book?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…