The-unknown
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 1,636
- 1,863
Kila mtu atampa majibu yasiyo ya kweli kulingana na namna waonavyoDanganyaneni tu hapa ila wakati ukifika ndio mtajua kumbe aliyekuwa hajui sio Zombie peke yake
Kila mtu atampa majibu yasiyo ya kweli kulingana na namna waonavyoDanganyaneni tu hapa ila wakati ukifika ndio mtajua kumbe aliyekuwa hajui sio Zombie peke yake
Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?Mkuu cha kwanza kabisa amini kama Mungu yupo na siku ya mwisho siku ya kulipwa matendo yako yote uliyofanya Dunian ipo pia, so kuna maisha mengine baada ya kifo yapo na utayakuta...
Nimesema uliza swali moja ujibiwe hoja kwa hoja. Hapa unaonyesha upunguani wako kwa kuandika sana uonekane unajua wakati hujui kitu na hujui nasimamia wapi unachojua ni matusiEverybody knows that ^a long time^ doesn't mean forever. Does it?
You really have some splanin' to do!
Acha uvivu na ufinyu wa akili, wewe. Hoja na maswali yote yanategemea hoja na maswali yaliyopita.
Shule ulisomea wapi kwani?
Mashahidi gani hao uwazungumziao wewe? Mashahidi wa Yehova wanaamini katika ufufuo.Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?
Kwahiyo wewe baada ya kusoma kuwa umetokana na nyani kama ulivyoelezwa na wakiokuletea dini yako na hiyo tamthilia ya biblia unaamini hivyo?Kama we hutaki kuamini vitabu vya dini Basi usiwahi kusema Kwamba hamna maisha baada kifo kwa sababu unaongea kitu usichokijua,
Ukiulizwa je Kuna maisha baada kifo sema sijui ,Kama vile ulikuwa hujui Kama utawahi kuishi duniani Ila umeishi ndo umejua Kuna maisha duniani.
Wanasayansi hamuamini msichokiona Wala kukiskia Sasa mbona unaamini kuwa hamna maisha wakati hujafa subiri ufe ndo upate jibu.
Kwa sisi tunaomini dini tunasema yapo kwa sababu tunaamini tusiyo yaskia Wala kuyaona Ila kwa elimu inyotoka kwa muumba ,
Imani inaambatana na elimu ,Soma ujue Kisha amini.
Je viumbe vingine vyenye uhai vinaenda huko pia vikifa?na je vinapitia mafundisho yapi ili kujiandaa?
Maisha mapya yapo kwakuwa umeelekezwa kupitia biblia au msahafu?na je waliokuwepo kabla ya dini inakuwaaje.Mkuu cha kwanza kabisa amini kama Mungu yupo na siku ya mwisho siku ya kulipwa matendo yako yote uliyofanya Dunian ipo pia, so kuna maisha mengine baada ya kifo yapo na utayakuta...
Binadamu hajawahi kufufuka au kufufuliwa na binadamu mwenzake i.e.yesuWrite your reply...kwani razalo aliefufuliwa na yesu anasemaje
Mbwa,miti,samaki,mawe,n k pia vitakuwa na maisha mapya?Ndio kuna hali nyingine ingawa sio maisha kama haya.Yakoje..mimi sijui lkn niko na uhakika 100% yapo
Makaburi hamna watu kuna mifupa na masalia ya miili ya wafu.Hapa kuna maswali mawili yanachanganywa na kupewa majibu tofauti kama mtoa mada mlinzi mlalafofofo alivyouliza. Swali lake lilikuwa Je kuna sehemu nyingine tunaenda na maisha kuendelea tukizikwa au Je tukizkwa maisha yanaendelea huko twendako? Jibu ni hapana kulingana na Biblia. Tukizikwa hakuna maisha yanayoendelea kama maneno ya mhubiri 9:5 na 9: 10 na iko kama Molodekai alivyosema kuwa ukifa ndio mwisho wa yote hakuna utendaji unaondelea kama alivyoambiwa ingawa hakuendelea kuwauliza maswali waliomwambia maana hawaishi hapo tu
Baada ya kifo inakuwa kama mtu aliyelala usingizi ambapo kunakuwa hakuna utendaji wowote wa mtu huyu ni mpaka atakapoamshwa ndio anaendelea kutenda.
Swali la pili linalochanganywa na la kwanza ni je, kuna maisha baada ya kifo au tumaini lolote? Kwa mujibu wa Biblia jibu ni ndiyo. Watu wote walio makabuirini wanasubiri ufufuo. Ukisoma maneno ya Yesu kwenye Luka 20:37, na barua mbili za Paulo, 1
Wakorintho 15:52, 1 Wathesalonike 4: 16 yote yanataja juu ya tumaini ambalo wanadamu wanalo baada ya kufa. Vinginevyo kama hakuna tumaini lolote la wakati ujao basi kumtumikia Mungu kwetu ni bure.
Hivyo kwa mtazamo wa Biblia
1. Je tukifa tunaendelea kuishi? Jibu ni Hapana tunaendelea kusubiri ufufuo
2. Je kuna maisha baada ya kifo? Jibu ni NDIYO kwa kuwa kuna ufufuo mbele yetu wa wote waliolala makabuirini.
Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
Momi naamini hakuna mwisho wa dunia ndiyo maana idadi ya watu inaongezeka kupitia kuzaliana hadi dunia ijae na si hivi karibuni.Hivi, mfano wa wanaojiiti mashahidi wa Jehova,si watu tunaishi nao? Wao imani yao ni kwamba unaishi,lakini ukifa,biashara imeisha. Ina maana hawajielewi? Kati ya wanaotambua uwepo wa hayo maisha baada ya kifo na wasiotambua,yupi mkweli, yupi muongo!?
Ndiyo kabisa,hali hiyo yaweza kuwa ni kujaa kwa dunia na kuelemewa kwa idadi ya watu kuwa kubwa na kupungua kwa viumbe wengine kama wanyama na mimea kutokana na overpopulation tukio ambalo linawezatokea baada ya miaka mingi saaaana siyo UFUFUKO !!!Ndio kuna hali nyingine ingawa sio maisha kama haya.Yakoje..mimi sijui lkn niko na uhakika 100% yapo
Mimi naamini kuna Mungu na maandiko matakatifu pamoja, matukio na uumbaji ndio vinatusaidia kuamini uwepo wa Mungu na ufufuo kwa wakati ujao. Kama huna imani kuwa Mungu yupo na ana nguvu basi hata haya mengine kuzungumza nawe ni kujisumbua tuMakaburi hamna watu kuna mifupa na masalia ya miili ya wafu.
Hao waliokuaminisha kuwa kunakufufuka kwa mujibu wa biblia kwanini wanashuhudia kila siku mabaki ya wafu wakarne nyingi kiasi kwamba kama kungekua na ufufuo basi hayo mabaki yangekuwa yameshafufuka kwa awamu ya kwanza na ya pili au hata ya tatu.
👍👏🙏Hakuna maisha baada ya kifo kama isivyowezekana kuwepo kifo kabla ya kutungwa mimba yako
👍👏🙏🎁💐🎖️🏆Wewe umewahi kufa ukajua kuna maisha baada ya kifo?
Wewe unaona sawa kuwa aminisha wengine kuna maisha baada ya kifo, Na Hujawahi kufa!!
Ila unaona si sahihi wengine kusema hakuna maisha baada ya kifo.
Leta uthibitisho wa kifo chako na thibitisha maisha baada ya kifo.
Mkuu haya maswali ni muhimu sana katika harakati za kujitambua. 👍👏🙏Biblia ni Hadithi za kutungwa na kusadikika wala hakuna ulicho jibu zaidi ya stori stori Uchwara tu.
Kama Mungu aliumba kwa kusudi la kudumu milele viumbe wake, Kwa nini viumbe vinakufa?
Yani tayari Mungu huyo ana ji Contradict mwenyewe kwenye uumbaji wake.
Viumbe vinakufa, Halafu unasema Mungu aliumba viumbe vidumu milele!!!
Contradiction.
Mungu huyo, Hakujua kwamba mpango wake utavurugwa na dhambi?
"Mpango wa Mungu" mnayedai ni mkamilifu na muweza wa vyote, Una vurugwaje na dhambi?
Mungu alishindwaje kuumba Dunia isiyo na mauti?
Kama Mungu alitaka tuwe Mbinguni, Kwa nini Aumbe binadamu duniani?
Mungu huyo, Alishindwaje kuumba Binadamu tuwe Mbinguni directly.
Swali lako ulitakiwa uwaulize waliowai kufa, sisi tulio hai tutajuaje?

tatizo hao hawaongeiMkuu huwezi kutetea hoja yako kwa kutumia kitabu chenye maneno yanayotiliwa shaka na mtoa hoja!Siyo kweli. Akiolojia na sayansi vinathibitisha juu ya ukweli na usahihi wa Biblia.
Habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni mambo halisi, kama tusomavyo kuhusu matukio ya vita vya dunia, au hata migogoro ya sasa baina ya Palestina na Israeli.
Yaliyomo kwenye Biblia, siyo tu kwamba ni habari za kihistoria, bali pia ni uvuvio mtakatifu ulioandikwa na watu halisi wakiomcha Mungu, mfano Musa, Daudi, Sulemani, Daniel.
Watu hawa wote ni wahusika halisi katika historia, wala si wahusika dhahania (fictional characters).
Ujumbe wao mahususi wa uvuvio kutoka kwa Mungu umetufikia sisi kupitia Biblia.
Viumbe vinakufa kwa sababu ya dhambi, kwa sababu ya uchaguzi mbaya wa Lusifa ama Shetani, kwa sababu mwanadamu alikubali naye kufuata njia ya Lusifa, akamwasi Mungu.
Lusifa alitumia uhuru wake vibaya. Mwanadamu naye alitumia uhuru wake vibaya.
Kufa kwa viumbe haina maana kwamba mpango wa kuishi milele umetoweka. Kifo kimekuja kwa sababu ya dhambi.
Lakini pia mauti siyo mwisho wa mambo. Kuna maisha baada ya mauti, kwa wale ambao wamechagua kuufuata mpango wa Mungu wa wokovu kupitia Yesu Kristu.
Alijua. Mungu anajua mwisho toka mwanzo. Anajua yote. Isaya 46: 9, 10. Kila kitu ki wazi mbele Yake. Ebrania 4:13.
Hii ndiyo maana Biblia inasema mpango huo uliandaliwa muda mrefu tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo 13:8
Kutokea kwa dhambi haina maana kwamba mpango Wake umezuiwa. Dhambi katika mpango wa Mungu, ni sawa mfano wa njia mbovu kwa msafiri.
Mungu hakushtukizwa na dhambi wakati akimuumba Lusifa, malaika walioasi na hata mwanadamu ambaye ameanguka.
Alijua na aliliona hilo mapema, ndiyo maana akaandaa mpango mahususi, mkamilifu ili kukidhi hali hiyo ya dharura kabla ya kutimia kwa mpango Wake.
Ukamilifu wa mpango huo uko katika makusudi husika, namna ya utekelezaji na hatimaye matokeo yake.
Mungu angeweza kutumia njia nyingineyo, lakini uchaguzi Wake wa kuanza kushughulikia dharura ya dhambi ndilo jambo bora zaidi ambalo lingekuwa na manufaa kwa viumbe Wake wanadamu kwa malaika, milele na milele.
Kuasi kwa Lusifa kuliambatana na hoja zake mahususi (incendiary postulations) dhidi ya Mungu ambazo pekee zingeweza kujibika kikamilifu mazima milele (completely & finally forever), kwa mujibu wa silika takatifu na yenye upendo ya Mungu, kwa kuwaruhusu viumbe Wake wenye utashi huru japo ^wachungulie^ ng'ambo ya pili na kuhabiri maisha nje ya Mungu.
Kwa maneno mengine, kuasi kwa Lusifa ilikuwa fursa ya Mungu kumthibitishia vinginevyo dhidi ya fikra zake kinyume na Muumbaji.
Unapozungumzia Mungu mwenye upendo timilifu na mwanadamu (au hata malaika) mwenye utashi huru, ni rahisi kutambua kwa nini viumbe wenye uwezekano wa kutenda dhambi waliumbwa.
Ni kana kwamba Mungu, ili kudhihirisha upendo Wake wa juu zaidi kwa mwanadamu na malaika na viumbe Wake wengine wenye nadhari za juu za maarifa, aliamua kuumba nafsi zenye utashi huru zikiakisi utashi Wake Mwenyewe.
Mwanadamu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu. Huo ndio upeo wa upendo wa Mungu.
Kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa umauti ni kutotambua silika na baraka kuu ya Mungu kwa viumbe Wake -- upendo.
Pia, kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa na dhambi na mauti ni sawa na kudai kwamba kwa nini Mungu asingetuumba tukiwa watii tarasili (automatic obedients), tulio radhi wakati wote, na tusio tayari katu wala wenye uwezekano wowote kabisa wa kubadili msimamo huo -- watii halaki (blind obedients), unaweza kusema.
Kama hilo angelifanya Mungu, basi tusingekuwa tumeumbwa katika ^sura na mfano Wake.^
Kwa namna hiyo, tusingekuwa tunamtumikia kutokana na moyo wa upendo, bali kwa kusukumwa na hulka asili ndani yetu iliyotarakibiwa awali (intrinsically preprogrammed nature) -- tungekuwa mithili ya roboti.
Matokeo yake, tungekosa utashi huru, ambayo ni tunu bora zaidi miongoni mwa amana alizotubarikia Maulana.
Pamoja na tunu hii kuu, ukaja pia uwajibikaji kwa upande wa mwanadamu kuhusu matumizi husika. Na ndipo hatari kuu ikafuatia. Lakini huo haukuwa mwisho wa mambo.
^Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.^ ~ 1 Korintho 15:22
Mungu hajashindwa kitu, na wala kushindwa hakupo katika asili Yake takatifu.
Ubongo wa mwanadamu ndio unakataa kukubali mambo jahara aliyoyafunua Mungu kuhusu mpango Wake kwetu.
Hivi inawezekanaje Mungu wa milele, aliyeumba vitu vyote, hata ahusishwe na msamiata wa kushindwa?
Ni wazi kwamba kudai Mungu ameshindwa, hilo tu kwa lenyewe ni kumkufuru.
Kila jambo analotenda Mungu, kila kitu anachoruhusu kitendeke, huwa kina kusudi maalumu.
Na ndiyo maana dunia, baada ya dhambi, wadhambi, Shetani na malaika zake kutokomezwa milele, bado itakuwa sehemu ya kutimizia lengo hilo la awali la Mungu
^1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye atafanya maskani Yake pamoja nao, nao watakuwa watu Wake. Naye Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na Yule aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yule mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yule ashindaye atayarithi haya, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yule afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo.^ ~Ufunuo 21