Na wanaohakikishia wenzao kuwa yapo ndo waliwaho kufa?
Biblia ni historia halisi. Imebainisha ukweli mwingi sana unaojibu maswali makuu yote kuhusu maisha ya mwanadamu yaliyopita, ya sasa na baadaye.
Mtu anayeamini uwepo wa Mungu, anashindwaje kuwa na hakika ya maisha ya baadaye? Anashindwaje kutambua kwamba maisha ya dunia na kaburi siyo mwisho wa mambo?
Mungu aliumba kwa kusudi la kudumu milele kwa viumbe Wake.
Pamoja na kwamba mpango Wake umevurugwa na dhambi, lakini bado ameandaa njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kurejesha mahusiano yake kwa Muumba wake.
Iwapo Mungu ndiye msingi, basi mauti kamwe haiwezi kuwa ukuta wala ukingo. Kuna maisha baada ya Kiama.
Ni muhimu pia kujikumbusha kwamba si kila mtu ataonja mauti. Kuna watu watakaokuwa wangali hai wakati wa kuja kwa Kristu Yesu. 1 Thesalonike 4:16, 17
Usemi mashuhuri kwamba ^kila nafsi itaonja mauti^ unaenezwa na Shetani kupitia malaika wake, kwa lengo kuu la kuwapotezea tumaini watu ambao wamechagua kumpenda na kumtii Mungu.
^Amin, amin, nawaambia, yule alisikiaye neno Langu na kumwamini Yule aliyenipeleka, yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali
amepita kutoka mautini kuingia uzimani.^ ~Yohana 5:24