Yaani Mungu ameniumba(achana na kuwa nimezaliwa mi sijaumbwa),napotea, ananiangalia tu hana habari?
Ni kwamba wewe ndiye umeamua kupotea huku ukijiangalia.
Vinginevyo ukiri hapa kwamba wewe ni akili hamnazo.
Unachukua pesa zako mwenyewe, unaenda baa kununua pombe, unalewa mwenyewe then unaendesha gari na kufa kwenye ajali.
Mwisho wa siku kifo chako asingiziwe injinia aliyeliunda gari?
Shame on you.
je,walipaa kwenda wapi kama siyo kurudi palepale walipoanzi kupaa?au wako hewani wanazunguka/wanaelea tu?
Akili gani hii? Pamoja na ulimwengu huu wa utandawazi, unashindwa kuchota maarifa japo kwenye Google?
Wanasayansi wataalamu wa anga wenyewe wamenyoosha mikono yao juu kuhusu kile wanachoshuhudia angani huko, wewe ni nani ubishe?
Halafu nani alishaenda huko juu, akarudi palepale alikoanzia?
Una ufinyu mkubwa wa elimu ya jiografia kiasi kwamba unashindwa kutambua tofauti ya kuzunguka katika anga la dunia na kutoka nje ya wigo wa dunia hadi anga za mbali.
Unakufa kimwili kiroho unaendelea kuishi
Mwanadamu ni nafsi hai, ambaye ni muunganiko wa mavumbi (mwili) na pumzi ya Mungu (uhai).
Anapokufa, kinyume chake hutokea: anakuwa mavumbi baada ya pumzi ya Mungu kumtoka.
Kimsingi, unapokufa unarudi katika hali ileile ya awali ya kutokuwepo, hadi wakati wa ufufuo.
Kwamba mtu akifa anakuwa roho, siyo fundisho la Biblia bali la umizimu na mashetani.
Ndiyo maana wengine wanadai wamewahi kukutana na wapendwa wao ambao tayari walishakufa.
Hayo ni mashetani kwenye mwonekano wa mwanadamu.
Solid proof kwenye spiritual world?.
Kama kitu hakina uthibitisho, hakifai kabisa kuaminiwa. Ukristu wala siyo dini ya ^amini tu,^ bila kuwa na ushahidi wa hakika.
We need solid proofs before we believe anything.
Reference za Bible hapana, ni za kuandikwa na watu waliotumia zaidi ya miaka 500 wakiiandaa Bible ila waitumie kwa manufaa yao.
Umeshawahi kuisoma Biblia hata mara moja kweli? Au unaipinga tu kimkumbo wakati hujui nini kilichomo?
Kama kungekua na mbingu, maisha mapya, kula asali na maziwa basi Wazungu wangeficha Bible zisifike Africa, hakuna Mzungu anatupenda watu weusi.
Kwa hiyo elimu, afya na maendeleo uliyo nayo leo Afrika amekuleteeni Mkushi?
Halafu ninyi Waafrika kumbe mnapendana eti?
Kumbe Wazungu ndio waliotekeleza mauaji ya kimbari Rwanda 1994?
Halafu juzi kati nchini Afrika Kusini waliokuwa wakiwatimua watu weusi humo kama mbwa mwizi kwa kisingizio cha kuhodhi nafasi zao za kazi, kumbe walikuwa ni Wazungu?
Warwanda na Waganda wanaoendesha biashara haramu Kongo na kuivuruga amani humo, kumbe ni Wazungu?
Kumbe mafisadi, walarushwa, wapigadili, watakatishaji, wahujumu-uchumi na wababaishaji wanaotawala serikali karibu zote za Afrika na kuyanyonga kimaendeleo, kumbe ni Wazungu?
Sikiliza wewe Mkushi, mwanadamu ni yuleyule tu, bila kujali rangi ya ngozi yake, kabila, dini, cheo, utaifa, hadhi, utajiri, nk.
Mkushi, Mchina, Mwamerika, Mhindi, Mulaya na Mwafrika, wote wanaweza kuwa wema sana ama wakatili kupindukia.
Binadamu yeyote akimwacha Mungu, afadhali ukutane na dubu aliyenyang'anywa watoto wake, kuliko ukabiliane naye (Mithali 17:12).
Ndiyo maana Injili ya Yesu Kristu inapaswa kuhubiriwa kote hadi kwa Waisraeli waliomkataa Yesu, pamoja na kuwa lilikuwa taifa teule.
Kama Mungu angekua na mpango wa binadamu kuishi milele, basi asingeshindwa kumzuia shetani asilete madhara kwenye mpango wake kwani yeye ni ndio mwenye ngunvu.
Wala Mungu hajashindwa na kamwe msamiati wa kushindwa haukai sambamba na Jina Lake tukufu.
Mungu anatenda kazi akifuata ratiba, nia na makusudi Yake.
Tatizo la dhambi lina muda wa ukomo wake. Ingawa Yeye si chanzo chake, lakini haikumshtukiza.
Aliona tangu awali kwamba dhambi ingetokea ulimwenguni, akafanya maandalizi ambayo kwayo waasi wangerejeshwa Kwake tena, na hatimaye uovu huo kutokomezwa usiwepo milele na milele.
^Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana Mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine; Mimi ni Mungu, wala hakuna aliye kama Mimi, nitangazaye mwisho tangu mwanzo na tangu zamani za kale, mambo yasiyotendeka bado. Nikisema, shauri Langu litasimama, Nami nitatenda mapenzi Yangu yote.^ ~ Isaya 46:9, 10
What this mean is that it's not without stupendous reason that the wise God allowed sin, suffering and death, not only to continue eating into His creation, but to intrude in the first place.
How this? He would have created Lusifer, the originator and instigator of evil without possibility of sinning (in which case he would have been some form of mindless drone -- incapable of occupying a special place to which he was designed).
Second, God would have prevented evil from being perpetuated further to the innocent angels and later on into our world, by annihilating him just before he could infect others and wreack havoc on the world.
In this case, the innocent angels would have never understood firsthand about the justice of God, thus driving them to live in fear of, instead of in love to, God.
This measure being implemented, would've perpetuated doubt, distrust and evil even further among previously faithful angels.
Is it then unreasonable to have a God who
could permit evil, given His attributes of love, holiness, perfection, morality, omniscience and omnipotence?
Are these two features -- evil and good -- mutually exclusive? The answer is Yes and No.
Yes, in that God can never be good and evil at the same time. And He isn't. God is good, He has always been, and always will He be.
No, in the sense that there is possibility of sin running parallel in God's creation, as it is the case now.
God's creation is not the same as God's character or God's Person. His creation is not some extention of His own nature. The creation is apart from God -- not connected to God.
So, in creating free moral beings to reflect His own image and likeness, and endowed with the capacity to experience love in the truest sense, God went all the way to risk His own character.
Isn't this best among His marvelous gifts to be humbly grateful for and exercised accordingly?
What do we learn? God can overrule even the darkest acts in order to bring about His ultimate purpose to the glory of His holy name.
Never even once can He suffer from scarcity of means. Does that imply, then, that evil is commendable and is to be condoned? Far from it!
MAMBO YOTE YA BIBLE NI MAJIBU KWA AKILI ILIYOFIKA MWISHO KUFIKIRI. NI SILAHA KWA WAJANJA
Haya wewe akili kubwa nipe jibu. Ndani ya chembe za atomu kuna nini, baada ya viasili vyake vinavyojulikana (protoni, elektroni, nyutroni, nk) na pia baada ya nishati msingi kwenye viasili hivyo?
I mean, ukienda ndani zaidi na zaidi, mwisho wake wapi?
If energy is considered to exist, it is surely something -- a thing. Isn't it? What then is further inside that thing we conventionally call energy?
Pili, ulimwengu unasemekana unatanuka wakati wote kuelekea kwa nje. Wapi?
Kwa sababu kama ni nje, it means tayari huo bado ni mwendelezo wa ulimwengu. You can never have nje that is not part of the world. Can you?
Je, mipaka yake iko wapi na baada ya mipaka hiyo kuna nini?
To make it simple: How far in can you go inside any smallest object, and how far out can you go towards the edge of the universe?
Is it even logical to term it the edge of the universe? Since the very word presupposes there is space further away, in which case we are not talking about the furthest end.
How do you understand the concept of space and time?
Uongo Tu, yule jamaa si alimuamsha kutoka usingizini
Kristu alimfufua Lazaro baada ya kukaa kaburi siku 4 mpaka akaoza na kunuka (Yohana 11:17, 39).
Kama kuna usingizi wa namna hiyo, basi ntahitaji ufafanuzi baadaye.
Kristu pia alifufuka kutoka kwa wafu, pamoja na watakatifu wengi wametajwa kwenye Biblia.
Ufufuo wa wafu ni uhalisia usiopingika.
Lazaro, alikua kaburini tayari yapata siku tatu.
Siku 4
Yan mungu alete Dini, watu Fulani Tu 😂, alafu wengine wabaki kupokea mapokeo Tu,
Huyo mungu ni mchoyo Sana wa elimu, halafu ni mbaguzi
Unaonesha jinsi gani wewe mwenyewe ulivyo na roho ya ubaguzi, uchoyo na ubinafsi.
Hutaki kunyonya ziwa la mama yako, kisa walishapita kaka na dada zako. Shame on you.
Jibu ni kwamba "the truth sits upon the lips of dying man"
A dying person is not a dead person. Sorry, try again.
we subili siku ufe ndio utajua
By then you would be too late to decide for eternal life. Time is now.
maana hakuna aliyewahi kufa na kurudi kuleta mrejesho.
Uongo mkubwa.
Utakwenda kuishi huko huko ambako ulikuweko kabla ya kuja hapa duniani. Jaribu kujiuliza babu na babu na babu hadi babu yako wa kwanza walikuwa wanaishi wapi!
Huo sasa ndio umizimu wenyewe.
Sawa , si ndio Njie mlisema jua Lina lizunguka jua,
Mara sijui jua lilisimama.
Kama tungeendelea kusikiliza upumbavu wenu basic Dunia isingekuwa kisayansi na kitchonogia
Unapaswa kujifunza kutofautisha kati ya mafundisho ya watu wanaojiita Wakristu na mafundisho halisi ya Biblia.
Hujui mtu anaweza kuwa mwanasheria lakini bado akaipotosha katiba? Akaitafsiri isivyo?
Kuhusu suala la dunia kuwa katikati ya mfumo wa jua, huo ulikuwa mtazamo wa watu. Wala siyo fundisho la Biblia na kamwe haliwezi kuhafifisha dini ya Ukristu.
Pili, kuhusu jua kusimama huo ni muujiza wa hakika usiopingika.
Ni uzushi,je mbona watu hawaendelei kufufuana?
Kufufuana ili iweje na kwa kusudi gani, wakati kifo lazima kiwakabili tena, kabla ya Kristu kurudi?
Muujiza wa Lazaro, watakatifu wengi waliofufuka wakati wa tukio la Kalvari ilikuwa na kusudi maalumu.
^Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho Yake.
^Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini.
^Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka.
^Makaburi yakafunguka na miili mingi ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa.
^Wakatoka makaburini, na baada ya Yesu kufufuka, waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi.^ ~Mathayo 27:50-53
Ukitaka kuona muujiza kama huo, usijali utashuhudia wakati itakapolia parapanda ya Mwana wa Adamu.
Ni sawa na bikra maria kuzaa mbona mabikra hawaendelei kuzaa?
Yaani wamzae Yesu mwingine, au? Maana unauliza swali kana kwamba hufikirii kwa makini.
Siyo kila tukio unaloona kwenye Biblia, lazima lirudiwe au lifanyike hivyohivyo.
Lile tukio lilikuwa na kusudi lake maalumu. Yesu mtakatifu alipaswa kuzaliwa na bikra safi.
bikra angekuwa na mme ambaye ni baba wa Yesu?
Baada ya hapo Mariamu aliolewa na Yusufu, wakazaa watoto wa kiume na wa kike (Mat 13:55, 56).
Kabla ya kumzaa Yesu, Mariamu alikuwa mchumba aliyeposwa na Yusufu, na wala hakuwa wamekutana kimwili (Mat 1:18).
Ukatoliki huchukia sana andiko hilo la Mathayo 13. Wanatamani hata lingenyofolewa leo.
^Wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka kutoka katika watu.^ ~ Luka 16:31
Hapa tutakudanganya tu mkuu, hakuna mwenye jibu la uhakika yote mitazamo tu
Hili jibu lako ndio mtazamo wako tu. Hakuna swali lisilokuwa na majibu ya uhakika. Wake up!