Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Biblia ni historia halisi. Imebainisha ukweli mwingi sana unaojibu maswali makuu yote kuhusu maisha ya mwanadamu yaliyopita, ya sasa na baadaye.

Mtu anayeamini uwepo wa Mungu, anashindwaje kuwa na hakika ya maisha ya baadaye? Anashindwaje kutambua kwamba maisha ya dunia na kaburi siyo mwisho wa mambo?

Mungu aliumba kwa kusudi la kudumu milele kwa viumbe Wake.

Pamoja na kwamba mpango Wake umevurugwa na dhambi, lakini bado ameandaa njia ambayo kwayo mwanadamu anaweza kurejesha mahusiano yake kwa Muumba wake.

Iwapo Mungu ndiye msingi, basi mauti kamwe haiwezi kuwa ukuta wala ukingo. Kuna maisha baada ya Kiama.

Ni muhimu pia kujikumbusha kwamba si kila mtu ataonja mauti. Kuna watu watakaokuwa wangali hai wakati wa kuja kwa Kristu Yesu. 1 Thesalonike 4:16, 17

Usemi mashuhuri kwamba ^kila nafsi itaonja mauti^ unaenezwa na Shetani kupitia malaika wake, kwa lengo kuu la kuwapotezea tumaini watu ambao wamechagua kumpenda na kumtii Mungu.

^Amin, amin, nawaambia, yule alisikiaye neno Langu na kumwamini Yule aliyenipeleka, yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.^ ~Yohana 5:24
Mungu ni nini? Na yuko wapi? Kazi yake katika maisha yako ni nini?

Unasemaje kuhusu mada iliyoandikwa humu siku za nyuma,ilikuwa inasema uingo mkubwa ulowahi kutokea duniani?! Unadhibitishaje kwamba kinachoongelewa si kweli?
 
Ndio maana ninasema ni vema tukaelewa vizuri mambo.

Kama wote tunakubaliana kwamba energy haifi, kwa nini tunahangaika na mwili?
Kwani energy ni akili au nafsi?
Energy ni kitu kinachosaidia mwili kufanya shughuli zake ambapo akili hufanya usimamizi wa shughuli hizo.
 
Biblia ni Hadithi za kutungwa na kusadikika wala hakuna ulicho jibu zaidi ya stori stori Uchwara tu.
Siyo kweli. Akiolojia na sayansi vinathibitisha juu ya ukweli na usahihi wa Biblia.

Habari zilizoandikwa kwenye Biblia ni mambo halisi, kama tusomavyo kuhusu matukio ya vita vya dunia, au hata migogoro ya sasa baina ya Palestina na Israeli.

Yaliyomo kwenye Biblia, siyo tu kwamba ni habari za kihistoria, bali pia ni uvuvio mtakatifu ulioandikwa na watu halisi wakiomcha Mungu, mfano Musa, Daudi, Sulemani, Daniel.

Watu hawa wote ni wahusika halisi katika historia, wala si wahusika dhahania (fictional characters).

Ujumbe wao mahususi wa uvuvio kutoka kwa Mungu umetufikia sisi kupitia Biblia.
Kama Mungu aliumba kwa kusudi la kudumu milele viumbe wake, Kwa nini viumbe vinakufa?
Viumbe vinakufa kwa sababu ya dhambi, kwa sababu ya uchaguzi mbaya wa Lusifa ama Shetani, kwa sababu mwanadamu alikubali naye kufuata njia ya Lusifa, akamwasi Mungu.

Lusifa alitumia uhuru wake vibaya. Mwanadamu naye alitumia uhuru wake vibaya.
Yani tayari Mungu huyo ana ji Contradict mwenyewe kwenye uumbaji wake.

Viumbe vinakufa, Halafu unasema Mungu aliumba viumbe vidumu milele!!!
Kufa kwa viumbe haina maana kwamba mpango wa kuishi milele umetoweka. Kifo kimekuja kwa sababu ya dhambi.

Lakini pia mauti siyo mwisho wa mambo. Kuna maisha baada ya mauti, kwa wale ambao wamechagua kuufuata mpango wa Mungu wa wokovu kupitia Yesu Kristu.
Mungu huyo, Hakujua kwamba mpango wake utavurugwa na dhambi?
Alijua. Mungu anajua mwisho toka mwanzo. Anajua yote. Isaya 46: 9, 10. Kila kitu ki wazi mbele Yake. Ebrania 4:13.

Hii ndiyo maana Biblia inasema mpango huo uliandaliwa muda mrefu tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo 13:8
"Mpango wa Mungu" mnayedai ni mkamilifu na muweza wa vyote, Una vurugwaje na dhambi?
Kutokea kwa dhambi haina maana kwamba mpango Wake umezuiwa. Dhambi katika mpango wa Mungu, ni sawa mfano wa njia mbovu kwa msafiri.

Mungu hakushtukizwa na dhambi wakati akimuumba Lusifa, malaika walioasi na hata mwanadamu ambaye ameanguka.

Alijua na aliliona hilo mapema, ndiyo maana akaandaa mpango mahususi, mkamilifu ili kukidhi hali hiyo ya dharura kabla ya kutimia kwa mpango Wake.

Ukamilifu wa mpango huo uko katika makusudi husika, namna ya utekelezaji na hatimaye matokeo yake.

Mungu angeweza kutumia njia nyingineyo, lakini uchaguzi Wake wa kuanza kushughulikia dharura ya dhambi ndilo jambo bora zaidi ambalo lingekuwa na manufaa kwa viumbe Wake wanadamu kwa malaika, milele na milele.

Kuasi kwa Lusifa kuliambatana na hoja zake mahususi (incendiary postulations) dhidi ya Mungu ambazo pekee zingeweza kujibika kikamilifu mazima milele (completely & finally forever), kwa mujibu wa silika takatifu na yenye upendo ya Mungu, kwa kuwaruhusu viumbe Wake wenye utashi huru japo ^wachungulie^ ng'ambo ya pili na kuhabiri maisha nje ya Mungu.

Kwa maneno mengine, kuasi kwa Lusifa ilikuwa fursa ya Mungu kumthibitishia vinginevyo dhidi ya fikra zake kinyume na Muumbaji.
Mungu alishindwaje kuumba Dunia isiyo na mauti?
Unapozungumzia Mungu mwenye upendo timilifu na mwanadamu (au hata malaika) mwenye utashi huru, ni rahisi kutambua kwa nini viumbe wenye uwezekano wa kutenda dhambi waliumbwa.

Ni kana kwamba Mungu, ili kudhihirisha upendo Wake wa juu zaidi kwa mwanadamu na malaika na viumbe Wake wengine wenye nadhari za juu za maarifa, aliamua kuumba nafsi zenye utashi huru zikiakisi utashi Wake Mwenyewe.

Mwanadamu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu. Huo ndio upeo wa upendo wa Mungu.

Kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa umauti ni kutotambua silika na baraka kuu ya Mungu kwa viumbe Wake -- upendo.

Pia, kudai kwamba Mungu alishindwaje kuumba dunia isiyo na uwezekano wa kufikwa na dhambi na mauti ni sawa na kudai kwamba kwa nini Mungu asingetuumba tukiwa watii tarasili (automatic obedients), tulio radhi wakati wote, na tusio tayari katu wala wenye uwezekano wowote kabisa wa kubadili msimamo huo -- watii halaki (blind obedients), unaweza kusema.

Kama hilo angelifanya Mungu, basi tusingekuwa tumeumbwa katika ^sura na mfano Wake.^

Kwa namna hiyo, tusingekuwa tunamtumikia kutokana na moyo wa upendo, bali kwa kusukumwa na hulka asili ndani yetu iliyotarakibiwa awali (intrinsically preprogrammed nature) -- tungekuwa mithili ya roboti.

Matokeo yake, tungekosa utashi huru, ambayo ni tunu bora zaidi miongoni mwa amana alizotubarikia Maulana.

Pamoja na tunu hii kuu, ukaja pia uwajibikaji kwa upande wa mwanadamu kuhusu matumizi husika. Na ndipo hatari kuu ikafuatia. Lakini huo haukuwa mwisho wa mambo.

^Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.^ ~ 1 Korintho 15:22
Kama Mungu alitaka tuwe Mbinguni, Kwa nini Aumbe binadamu duniani?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba Binadamu tuwe Mbinguni directly.
Mungu hajashindwa kitu, na wala kushindwa hakupo katika asili Yake takatifu.

Ubongo wa mwanadamu ndio unakataa kukubali mambo jahara aliyoyafunua Mungu kuhusu mpango Wake kwetu.

Hivi inawezekanaje Mungu wa milele, aliyeumba vitu vyote, hata ahusishwe na msamiata wa kushindwa?

Ni wazi kwamba kudai Mungu ameshindwa, hilo tu kwa lenyewe ni kumkufuru.

Kila jambo analotenda Mungu, kila kitu anachoruhusu kitendeke, huwa kina kusudi maalumu.

Na ndiyo maana dunia, baada ya dhambi, wadhambi, Shetani na malaika zake kutokomezwa milele, bado itakuwa sehemu ya kutimizia lengo hilo la awali la Mungu

^1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, Naye atafanya maskani Yake pamoja nao, nao watakuwa watu Wake. Naye Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao.

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

5 Na Yule aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yule mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.

7 Yule ashindaye atayarithi haya, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yule afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo.^ ~Ufunuo 21
 
Mungu ni nini?
Muumbaji. Nafsi. Mtakatifu. Yeye ni upendo. Ni mwenye huruma na mwingi wa fadhili. Haki, kweli, mamlaka na ukuu, ndizo sifa Zake.

Ni mweza yote. Anajua yote. Mkamilifu na mtimilifu katika kila namna. Hana dosari wala upungufu wowote ule katika asili Yake.

Alikuwepo milele, yupo, na anaishi milele kwa uweza wa nafasi Yake Mwenyewe.

Anaichukia dhambi kuliko, ila anampenda mdhambi upeo. Yohana 3:16.
Na yuko wapi?
^Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti Changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu Yangu.^ ~ Isaya 66:1

Zaburi 139:
7. Niende wapi nijiepushe na Roho Yako? Niende wapi niukimbie uso Wako?

8. Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10. Huko nako mkono Wako utaniongoza, Na mkono Wako wa kuume utanishika.

11. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

12. Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. ~ Zaburi 139.

Kazi yake katika maisha yako ni nini?
^Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani Yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.^ ~Yohana 15:5
Unasemaje kuhusu mada iliyoandikwa humu siku za nyuma,ilikuwa inasema uingo mkubwa ulowahi kutokea duniani?! Unadhibitishaje kwamba kinachoongelewa si kweli?
Weka kiunganisho (link)
 
nimesoma apa ulivyoanza tu sijaendelea uko mbele. umezingua mkuu.
Biblia inamzungumzia Ibrahimu, Babeli, Misri, wana wa Israeli, wafalme na falme za kale kama vile Rumi, Uyunani, nk.

Hao wote ni wahusika halisi kwenye historia ya Biblia na historia hasidini (secular history).

Nitafurahi kutambua wapi ulipo uzinguaji wangu. Kauli moja au mbili tu hazitoshi kubainisha wazi mantiki yako au suala unalolenga.
 
Kwani energy ni akili au nafsi?
Energy ni kitu kinachosaidia mwili kufanya shughuli zake ambapo akili hufanya usimamizi wa shughuli hizo.
Swali lako ni sawa na kuuliza: kwani mwili ni ubongo au moyo?

Kama kuna kitu cha thamani kwa mtu, kitu hicho ni akili.
 
Energy can not be created nor destroyed but can be transformed from one form to another, utaendelea kuwepo duniani but utabadili form of energy from ATP energy to( ....) energy, then mzunguko ni mrefu na utaendelea kubadili aina za nishati kwa miaka million kadhaa
 
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?
Mtafute mchungaji mmoja wa kanisa linalojiita!...la ufufuo na uzima...

Gwajima... Akusaidie namba za watu aliowafufua wakupe mrejesho wa huko...

Dini is the biggest scam ever...!(UONGO ULIOSUKWA KWA USTADI WA HALI YA JUU!!) Na watu magenius kwelikweli!

You only live ones in this world... And that's the anthem!....

Kama hakuna aliewahi kufa na akafufuka.....kuja kuhadithia.... Then the rest is the story!!! Kama story zingine! Za Netflix!!!
 
U c
 

Attachments

  • 3467d61dff0be55c1244f253d1e88938.jpg
    3467d61dff0be55c1244f253d1e88938.jpg
    23 KB · Views: 16
Muumbaji. Nafsi. Mtakatifu. Yeye ni upendo. Ni mwenye huruma na mwingi wa fadhili. Haki, kweli, mamlaka na ukuu, ndizo sifa Zake.

Ni mweza yote. Anajua yote. Mkamilifu na mtimilifu katika kila namna. Hana dosari wala upungufu wowote ule katika asili Yake.

Alikuwepo milele, yupo, na anaishi milele kwa uweza wa nafasi Yake Mwenyewe.

Anaichukia dhambi kuliko, ila anampenda mdhambi upeo. Yohana 3:16.

^Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti Changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu Yangu.^ ~ Isaya 66:1

Zaburi 139:
7. Niende wapi nijiepushe na Roho Yako? Niende wapi niukimbie uso Wako?

8. Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10. Huko nako mkono Wako utaniongoza, Na mkono Wako wa kuume utanishika.

11. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

12. Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. ~ Zaburi 139.


^Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani Yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.^ ~Yohana 15:5

Weka kiunganisho (link)

Kiunganishi chako hicho hapo
 
Yaani mtu upo hai unaacha kuishi, unaanza kufikiroa kuishi baada ya kufa.

Umeshasema kufa...maana yake hakuna maisha
 
Back
Top Bottom