Je, Hoyce Temu kamponza Diwani Athumani?

Je, Hoyce Temu kamponza Diwani Athumani?

Kuna reshuffle imefanyika kwenye idara ya usalama, kwa macho ya kawaida inaweza kuonekana hili ni la kawaida, lakini kumbadili DG wa usalama si jambo dogo hata kidogo! Seniors wengine wanaweza kubadilishwa muda wowote wakizingua lakini sio kwa DG

Tumeaunza mwaka na kashfa ya balozi wetu UN Geneva kutuhumiwa kuuza siri za nchi kwa 'maadui' ama kwa watu wenye nia ovu na nchi yetu.. Hili si jambo dogo na kwa baadhi ya nchi hilo ni kosa la uhaini na hakuna adhabu nyingine zaidi ya kitanzi

Idara ya usalama wa nchi ndio ina jukumu la kulinda mkoba/mikoba yote inayohusika na 'siri' za nchi! Anapitokea mtu hata kwa nafasi yake kubwa ya kiuongozi akafanikiwa kupenya, kudukua na kuondoka na kabrasha lolote lenye habari nyeti za taifa bila DG kupata taarifa ama kuchukua hatua, huyo ndiye mwajibikaji no 1...!

Hii kashfa ya Temu ikija kuthimbitika list ya watakaotumbuliwa ni ndefu ila kwasasa tubaki na hili la Mzee wetu Diwani aliyebadilishiwa majukumu na kama hili la Ms Temu ndio limesagia kunguni
Vipi kuhusu swala la ajali ya ndege kule Bukoba; wewe unaona lilikuwa ni tukio la kawaida sana?

After all, Hoyce hajafanya kitu chochote kwenye post aliyoteuliwa na Rais, labda tu Kiingereza cha Wanasheria ni kigumu watu hawajaelewa kilichoandikwa kwenye document inayosambaa mitandaani

Chances ni kwamba Hoyce anachafuliwa tu humu kwenye mitandao kwa sababu tuhuma zinazoongelewa kwenye document hazihusiani na kazi anayofanya sasa, ni za nyuma. Na kama tuhuma hizo zingekuwa ni za kweli, basi chances ni kwamba mama asingemteua Hoyce kwa sababu zinaonyesha kuwa ni za nyuma kabla ya uteuzi wake, zingine zina adte back to as far as 2018!

Hoyce anaweza kuwa anchafuliwa tu!

T14 Armata

Kama anamuondoa DG wa TISS alafu anamuacha HOYCE mwenyewe ina maana gani? Unahakika Samia huwa anafanya Vetting? Hujui kuwa kuna wazee wa Vimemo huko nyuma waligombana na Hayati kisa alikataa vimemo vyao? Sio mara ya kwanza Samia kuteua mtu wa ajabu katika nyazfa kubwa! Rejea uteuzi wa Katibu mwenezi wa CCM kuwa DG wa TPDC mwaka juzi.
Mh Azza kuwa RC wa Simiyu, watu wakalalamima akatenguliwa
 
Kama anamuondoa DG wa TISS alafu anamuacha HOYCE mwenyewe ina maana gani? Unahakika Samia huwa anafanya Vetting? Hujui kuwa kuna wazee wa Vimemo huko nyuma waligombana na Hayati kisa alikataa vimemo vyao? Sio mara ya kwanza Samia kuteua mtu wa ajabu katika nyazfa kubwa! Rejea uteuzi wa Katibu mwenezi wa CCM kuwa DG wa TPDC mwaka juzi.
Kwa ushahidi ulionao wewe, ebu tueleze hapa kinagaubaga; Hoyce amefanya kosa gani?
 
Analihitaji hizo reservations za Hoyce? Mtu kama aliwahi kuteua katibu mwenez CCM Wilaya akawe DG tena TPDC mpaka watu wakapiga kelele ndo akaja kutengua utashangaa ya Hoyce? Rais tulienae unatakiwa umjue wa aina gani! Huyu ashughulishi ubongo wake, huyu ni wale wa vimemo tu anateua! Hayo yakutaka mpaka amjue huyu ni wa wapi alipita wapi aliyaweza Magufuli pekeake hawa wengine.
Huyo uliesema kayaweza ndio mara 100 ya mama labda km mtukuma mwenzako
 
Nadhani umemkuza mno kuliko uhalisia. Issue zake ni binafsi na kama wengine walivyosema, ni kesi za nyuma kabla hata hajapelekwa Uswizi.

Swali linakuja kwa nini mtu ambaye hana uzoefu na diplomasia alipewa ubalozi tena sehemu nyeti huku wakijua ana makandokando tena huko huko ndani ya UN? Walikuwa wanataka kuachieve nini? Je hawakudhani hiyo ingeweza kuleta mazingira mabaya ya kazi kati ya ofisi ya ubalozi wetu na UN huko Uswizi?

Mfumo wetu wa kupata viongozi na watumishi wa umma ulivurugika toka zamani, huu tu ni mfano wa jinsi system ilivyooza. Tutamlaumu bure kwa kumteua ila jiulize na yeye amefika hapo kwa uwezo gani?
Nimesoma rasimu na hukumu ya kesi UN dhidi ya Hoyce Temu.
Ufisadi mtupu.
Na bado akateuliwa kwenda Uswiss kuiwakilisha nchi kwenye mahusiano na un.
Kuna mtu serikalini kichwa chake si kizuri.
 
hii ilikuwa funga kazi , in short tuseme tu anahitaji kushauriwa na watangulizi wake
Mtangulizi gn wa kumshauri samia wa tanzania hamchelewi kusahau huyo mtangulizi utawala wake simlikuwa mnasema ndio ufisadi ulikuwa mkubwa leo atoe ushauri gn
 
Hoja yako ni mfu na haina maana kabisa, kama ingekuwa hivyo hata huyu aliyepewa angeondolewa maana alikuwa Naibu DGIS, pia Diwani hajapata demotion amepanda juu, anakuwa chief of Staffs sio cheo kidogo kama unavyodhania.

Balozi zetu zote ziko na 80% ya watu wa TISS, JWTZ na POLISI.
Sio rahisi hivyo, na hakuna mtu ameuza siri za nchi kwa maadui kama inavyoaminishwa, na nikwambie kama hujui kitu tulia na uache kukurupuka.

Nchi yetu top secret hawezi pewa BALOZI. Top secret zetu access yake sio rahisi kama inavyodhania ww, TISS sio kwamba wao ndio wana kila taarifa, always agency zingine zinafanya kazi kukeep hizo secret, na wakati mwingine DGIS anakosa taarifa muhimu na watabe wanamfikishia RAIS direct.

Suala la Usalama wa nchi yetu achana nalo, wewe ni mtoto sana, usijidanganye na influence za hapa jukwaani Dogo.
Nilimsikia jakaya 'rais ana vyombo vingi vya kumpa taarifa' nikahisi siyo TISS peke yake wanaokusanya na kuchakata taarifa
 
Hoja yako ni mfu na haina maana kabisa, kama ingekuwa hivyo hata huyu aliyepewa angeondolewa maana alikuwa Naibu DGIS, pia Diwani hajapata demotion amepanda juu, anakuwa chief of Staffs sio cheo kidogo kama unavyodhania.

Balozi zetu zote ziko na 80% ya watu wa TISS, JWTZ na POLISI.
Sio rahisi hivyo, na hakuna mtu ameuza siri za nchi kwa maadui kama inavyoaminishwa, na nikwambie kama hujui kitu tulia na uache kukurupuka.

Nchi yetu top secret hawezi pewa BALOZI. Top secret zetu access yake sio rahisi kama inavyodhania ww, TISS sio kwamba wao ndio wana kila taarifa, always agency zingine zinafanya kazi kukeep hizo secret, na wakati mwingine DGIS anakosa taarifa muhimu na watabe wanamfikishia RAIS direct.

Suala la Usalama wa nchi yetu achana nalo, wewe ni mtoto sana, usijidanganye na influence za hapa jukwaani Dogo.
Umenena kweli mkuu, lakini tukubaliane ukweli.
Toka DGIS. mtu mwenye mamlaka makubwa na mapana, hadi kuwa Katibu Mkuu Ikulu, by all means anaongoza watu pengine wasiozidi 50!!
Aaaah yetu masikio!
 
Well, issue za hoyce ni yeye na aliyekua muajiri wake UNDP, sidhani kama zina uhusiano na TISS.
May be tuseme baada ya kuwa rufaa yake huko kwa aliyekua muajiri wake imeshindikana tuseme atumbuliwe kwakua ameonekana hakufit ila has nothing to do na Diwan. Pia masuala ya Hoyce yamepita sio ya sasa hizo ni rulling za mambo yake kipindi cha nyuma...kwa tamaduni za wanasiasa wetu hiyo ngoma ni ndogo sana wanaweza funika kombe! Labda UN walete pressure kua huyu mtu aliwe kichwa! Wakuu Someni hukumu hiyo ya rufaa attached ili kuelewa issue zenyewe tofauti na mtandaoni watu wanavyoongea!
Tatizo sasa ni kwamba kilichoandikwa kwenye document hakihuisani na ajira yake ya sasa; na ni taarifa za kuanzia zamani mno. Hii case kama ilikuwepo, mama lazima angeijua mapema na asingemteua.

After all, hivi chombo kikubwa kama UNDP kinaweza kuweka taarifa kama hizi PUBLIC, au kuziachia zikakaangukia kwenye mikono baki? This document is forged na possibly mteule hana tuhuma zozote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom