Je, hakuna uwezekano wa mitandao ya simu kuruhusu kufuta au kuhariri ujumbe mfupi (sms)?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,822
Sina ujuzi wowote kwenye masuala ya mawasiliano lakini najaribu kuwaza kama kwenye WhatsApp kila siku maboresho yanafanyika why not kwenye jumbe za kawaida za simu?

Kwani hakuna uwezekano wa kutufanyia tuweze kurekebisha ujumbe tunaotuma. Kwa mfano mngeweka mtu aweze kuhariri au kuufuta kabisa ujumbe alioutuma ndani ya dakika kadhaa kisha zikipita hizo dakika basi kwa mtumiwa ujumbe kusiweze kufutika mpaka aamue mwenyewe.

Kwa kuchomekea pia kuna vitu vinaboa kwenye miamala ya simu ambapo naona nmb mkononi tu ndo wamesolve huo usumbufu; kumuuliza mtu mtandao wakati akiweka tu namba ya simu mtajua ni mtandao gani. Ilitakiwa akisema tuma pesa basi aletewe ingiza namba na siyo longolongo nyingine kwani namba ya nida ina kazi gani?
 
Back
Top Bottom