Tetesi: Huduma kwa wateja (call centre) kuhusika WIZI na UTAPELI kwa mawakala wa fedha wa mitandao ya simu

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,198
5,720
Habari,

Ni matumaini yangu mnaendelea vizuri pamoja na harakati za ujenzi wa taifa letu la Tanzania.

Nia ya uzi huu ni kukumbusha na kuamsha makampuni ya simu yanayotoa huduma za kifedha hasa Tigopesa, Mpesa, Airtel Money n.k, pamoja mamlaka za kiserikali kama wizara na mamlaka ya mawasiliano pamoja na jeshi la polisi kuchukua hatua stahiki kukomesha swala hili

Kampuni hizi zimerahisisha saana huduma za kifedha na kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi, lakini leo nataka kuzungumzia wizi unaoendelea katika mitandao ya simu ambayo mawakala wanakutana nao kila uchwao.

Katika kipindi cha wiki nzima nimekutana na malalamiko ya mawakala kudai kuibiwa katika njia zia zinazoleta utata.

Kwakua shughuli zangu zinahusisha kufanya transaction za kifedha kwa njia za simu basi imekua kawaida kusimuliwa na mawakala mikasa wanayokutana nayo, na hivi karibuni mawakala karibu 10 ndani ya wiki moja wanakutana na kisanga hiki... nimeshtushwa saana.

Mazingira wanayokutana nayo;
Mteja anakuja kutoa pesa, wao wanapokea ujumbe unaowajulisha kwamba mteja amefanikiwa kutoa kiasi fulani cha pesa kwenye namba yake, hivyo akishajiridhisha anampatia pesa taslimu mkononi mteja(tapeli) mara moja anaondoka zake.

Kuja kushtuka unakuta kwamba ule ujumbe hukuwa wa kweli ni pindi anapouliza salio ama kumuhudumia mteja mwingine kwakumwekea kwenye simu.

Kwanini huduma (call centre)kwa wateja wanahusika?
Mawakala wakishafikwa na changamoto hii ushirikiano unakua mdogo mno... majibu ni kama hivi .... enhh ndo ushaibiwa, .... ushatapeliwa hakuna jinsi...! Baada ya majibu hayo hakuna msaada wowote unaweza pewa wakati kila kitu kimefanyika ki mtandao (hawaoni transaction wala namba iliyotuma msg)
Mazingira yanayoshabgaza zaidi inakuaje matapeli na wezi hao

wajue taarifa ya salio lilipo kwenye flot yangu, kama si kuwasiliana na mtoa huduma (call centre) mwenye access na taarifa zangu?

Na kwann pasiwe na njia rahisi kufuatilia huu utapeli na wizi?

Mitandao ya simu inatakiwa itambue watu waliowapa dhamana kutatua matatizo ya wateja wao ni binadamu na lolote ama chochote kinaweza kutokea pasipo usimamizi maalum wa kuzuia changamoto za kibinadamu katika kutimiza majukumu yao...

Hawa watoa huduma baadhi yamkini watakua na mtandao wao unaoratibu huu ujambazi na wizi.
Tunaomba maamlaka husika Wizara ya habari na TCRA mlitolee ufumbuzi swala hili kwakutunga sheria kali kwa makampuni ya simu yatakayozembea kusimamia na kulinda maslai ya mawakala wake kwenye utapeli na wizi wa namna hii.

Pia wizara ya fedha hili swala ni muhimu kuliangalia japo kwa uchache wao ila wanasisimua pato la taifa sasa mnapo acha kulisemea hawa mawakala wanafunga biashara yao ya uwakala nanyi serikali mnakosa mapato.

Muhimu
Wengi wa mawakala ni wenye mitaji midogo ambayo hio pia inaibiwa na kuwafanya washindwe kukua na hatimaye kufa kabisa, tunawasihi mzuie wizi huu sisi wateja wenu tunapata changamoto saana.

#Sauti ya mawakala fedha
 
Mimi ofisini kwangu nimezaba sana vibao madogo wanaopangwa na matapeli kwamba nenda kwa wakala fulani, akuwekee laki 2 au laki moja halafu usiwe karibu na watu sana😂😂😂 wakifika nawalamba makofi baada ya muda akili inakaa sawa. Maana ilizidi sana kwa siku wanakuja hadi wanne
Wanamtandao wao hao jamaa kule kwenye system wanawapa tagert nanyi mnakua targeted
 
Ni uzembe kuamini hivo...kuibiwa mawakala no ujinga wao...na labda hukosoma mkataba wakala anaoingia na kampuni husika
 
Mimi ofisini kwangu nimezaba sana vibao madogo wanaopangwa na matapeli kwamba nenda kwa wakala fulani, akuwekee laki 2 au laki moja halafu usiwe karibu na watu sana😂😂😂 wakifika nawalamba makofi baada ya muda akili inakaa sawa. Maana ilizidi sana kwa siku wanakuja hadi wanne
Ulikuwa unajuaje kama hao ni matapeli na si wateja wa kawaida?

Maana haujatuwekea njia zililokuwa zinakusaidia katika utambuzi.
 
Back
Top Bottom