Je unajua kuhusu hili? Ugunduzi mpya wakitaalam mfumo wa malipo kwenye tovuti yako kwa wale wenye kampuni iliyosajiliwa

sokoniinc

New Member
Mar 14, 2022
1
2
Kama unamiliki kampuni Iliyosajiliwa na una website yeyote ya mauzo mtandaoni. Unaweza ukaendelea kusoma.
Kwa wale wenye website tunajua kuwa, tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni mfumo wa malipo.

Mifumo ya malipo iliyopo haimruhusu mtanzania kuweza kutumia tovuti yako. Na kufanya manunuzi ya kitu akipendacho kwa urahisi.

Website au tovuti zetu zinahitaji sana mifumo sahihi ya malipo.Mifumo Iliyounganishwa na mitandao ya simu ili kupokea pesa.

Pesa izo zinatakiwa ziweze kupokelewa na mifumo tuliyoizoea kama mfumo wa Mpesa na AirtelMoney na TigoPesa.

Sasa tunapateje mifumo hii?​

Bila kukupotezea wakati kwa upande wetu tumekuja na mfumo wa malipo unaoweza kufanya kazi kwenye website yako.

Mfumo huu tumeutengeneza na unaunganishwa na Mpesa , Airtel money pia na Tigo pesa. Ili kuwezesha website yako kupokea pesa kwa wateja kiurahisi.

Nasisitiza tena. Kwa wale wenye makampuni iwe ni shule au ni kampuni binafsi tunaweza tukakufungia mfumo huu wa malipo ili uanze kupokea pesa kupitia website yako.

Swali : Je mnafanya makato yeyote kwenye mfumo wenu?
Jibu ni hapana hatufanyi makato yeyote ya asilimia kwenye mfumo wetu.

Je ni kwa wale tu wenye makampuni?​

Ndio ni kwa wale tu wenye makampuni binafsi yaliyosajiliwa ndio wanaweza kuutumia mfumo wetu wa malipo.

Kuna faida gani za kuwa na mfumo huu wa malipo kwenye website/tovuti yangu?​

  • Utaweza kupokea pesa ndani ya website yako na pesa iyo ikaenda benki kwa urahisi kabisa.
  • Pili, Utawarahisishia wateja wako namna ya kulipia huduma mbali mbali utakazo zitoa kwenye kampuni yako.
  • Tatu, Utahudumiwa na timu ya wataalam waliogundua mfumo huu, pale tatizo lolote likitokea. Tatizo lolote la kiufundi lipo juu yetu.
  • Nne, Kwa wale wenye tovuti zao uwe ni blogger au ni mjasiriamali mtandaoni. Na una kampuni iliyosajiliwa wakati wako umefika.Wakati wa kuwarahisishia wateja wako njia za malipo ya huduma uzitoazo kwa kupitia MPESA,TIGOPESA NA AIRTELMONEY.
  • Tano, Utafurahi jinsi mfumo huu unavopokea pesa kwa mteja kwa kutumia ussd push.Nikimaanisha mteja wako akitaka huduma yeyote unayoitoa kwenye tovuti. Na akifikia kununua huduma hiyo, atapata tu ujumbe wa kuweka pin na atakuwa ameshalipia.
  • Sita, Mfumo huu utakuonesha order zote za wateja wako, bei waliolipia, order namba, utaweza kuhakiki manunuzi kama huduma imeshafikishwa. Utaweza kuona umepata wateja wangapi kwa siku, wale walioishia njiani na wale walionunua. Na mfumo huu unaweza kuuza softcopy(kama vitabu mtandaoni) na bidhaa za kusafirishwa.

Inachukua mda gani hadi mfumo huu niwe nimeshaupata ndani ya tovuti yangu?
Ukishamaliza kujaza fomu zote na kukusanya kwa wataamu wetu wa Mpesa, Airtel na Tigopesa.

Na wakisha kupitisha kuwa unafaa kuunganishwa.

Kwa upande wetu tutakuunganisha hata ndani ya siku moja.

Mahali ambapo panachukua mda ni pale tu pa kuwa verified. Au kuhakikishwa na mitandao ya simu kama kampuni yako inafaa kuunganishwa.

Na mfumo huu nawezaje nikaupata.?​

Narudia tena kama una kampuni iliyosajiliwa. Na unahitaji tukufungie mfumo huu unaweza ukatupigia kwa namba 0756431032 au 0687226493 ulizia Eng Israel Ngowi. Ndio muhusika kamili.

kuhusu upatikanaji wa mfumo huu.

Ukinipigia ntakuunganisha na kitengo cha tehama AirtelMoney na Mpesa au TigoPesa. Ili wakuhudumie kwa swala zima la fomu.Fomu zote utakazotakiwa kujaza kabla haujapata mfumo wetu huu wa malipo.

Ukisha kusanya fomu ni vizuri ukawasubir kwa mda ili mitandao ya simu wapate mda wa kukuhudumia.

kufikia kukuhudumia, kama utahitaji msaada wowote wa kiufundi .Pia unaweza ukanipigia kwa namba izo hapo juu na nitakuwa Pamoja na wewe ili ukamilishe zoezi zima.

Je naweza nikauchukua mfumo huu na kumpa mtu mweingine?​

Hapana. Na ni vizuri ukajua kuwa, kila tunapo mfungia mteja mwingine tunafanyia mfumo wetu sanitization kwanza. Sanitization nikimaanisha kuondoa taarifa zilizobaki ndani ya mfumo ili na kuurudisha uweze kutumika upya na mtumiaji mwingine.

Na pia pale utakapo mpa mtu bila sisi kujua utakuwa unatengeneza muingiliano na mfumo wako. Na linaweza likawa tatizo baadae wewe kuto kupokea ela yako.

Kama unamiliki tovuti Zaidi ya moja, tunaweza tukarudia kukufungia mfumo huo huo kwenye tovuti zote zakwako tu.

Kwa sasa tuna chaji Sh 200,000 tu. kwa wale wanaohitaji kufungiwa kwa mtandao mmoja.

Hatuchaji kwa website bali kwa kila mtandao utakaohitaji uongezeke.

Na kwa wale ambao watahitaji kufungiwa na Tigopesa ni vizuri mkawa mnatumia AWS amazon webservices. Ili mfanye kwanza configuration ya VPN.

Mwisho.​

Sio tena vigumu kama ulivokuwa unafikiria. Kwa sasa kufunga mifumo hii ya malipo kwenye tovuti yako ni kwa urahisi kabisa.

Kumbuka kwa wale wenye makampuni ni vizuri ukaanza mapema. kujaza fomu, za watu wa mitandao ya simu ili upate huduma ya mfumo huu mapema.

Yawezekana una kampuni na unaona haikuhusu. Lakini ndio mfumo pekee ambao utarahisishia wateja wako, Wawe ndani ya kampuni au nje ya kampuni, Kulipia huduma na bidhaa unazoziuza kabla ya kuhudumiwa.

Urahisi ni pale tu mteja atakapoona inahitajika tu kuingiza namba ya simu na kulipia bidhaa aipendayo mtandaoni.

Pia kama una kampuni na unahitaji wataalam wa kukutengenezea kwanzia tovuti/website mpaka kukuunganisha na mfumo huu pia piga namba izo hapo tutakuhudumia.

Kila tovuti tuna chaji kutokana na wingi wa taarifa unazotaka kuziweka kwenye tovuti yako.

Usisite kuchukua hatua. Tupo kwenye ulimwengu ambao shughuli zote zinafanyika mtandaoni. Wahi uwe wa kwanza kuwarahisishia wateja wako. Warahisishie Njia ya kulipia huduma zote utakazozitoa kwenye kampuni yako mtandaoni.

Tupo Arusha AICC conference kama utakuwa arusha unaweza kututembelea
AICC conference Kilimanjaro hall room 314 office called Sokoniinc.
 
Back
Top Bottom