Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali lakini mtu mwenye akili zake timamu ni lazima ajiulize. Ukimya wetu, msitufanye mazuzu kuna...

Nimesoma comments almost zote inaonekana wengi hamjui tabia za serikali yetu.

Kuchelewesha kutoa taarifa za msiba kulianzia kwa Magufuli, wakatuficha mwanzo mwishowe wakasema kweli, hii tabia imeendelea hata kwa Mzee Mwinyi, nae ikawa hivyo hivyo.

Siamini kama Magufuli aliuwawa na yeyote, ni Corona ndio ilimuondoa kwa sababu hakuchukua hatua yoyote kujilinda licha ya wasaidizi wake baadhi kutangulia kufa.
 
Wanabodi,

Hapa duniani kuna fani mbalimbali za shughuli, na shughuli kuu ya kwanza duniani baada ya Mungu kumuumba binadamu, ilikuwa ni shughuli ya kutengeneza watoto au kuumba viumbe. Kwa vile Adamu na Hawa au Adamu na Eva, wao waliumbwa na Mungu mwenyewe, hivyo shughuli yao kuu ya kwanza ilikuwa ni kutengeneza watoto ili kujenga familia, kwa kuumba viumbe wengine!

Ile shughuli ya kutengeneza watoto ili kujenga familia, au uumbaji wa viumbe vipya, ndio shughuli kuu ya kwanza ya binadamu hapa duniani!, (the oldest professional) na viumbe wote, duniani kabla ya kuzaliwa ni lazima kwanza shughuli hiyo ifanyike, ndipo kiumbe kiumbwe, na ndipo kizaliwe, hivyo japo wengi wanahesabu siku ya kuzaliwa ndio siku yao ya kwanza duniani na watu wanasherehekea siku ya kuzaliwa, yaani birthday.

Hiyo siku ya kuzaliwa, ni siku tuu ya kuingia duniani, lakini sio siku ya kuumbwa!, siku unazaliwa, ujue uliumbwa miezi 9 nyuma!, kwa vile hata wazazi waliokuumba, hata mama aliyekubeba tumboni mwake, anakuwa hana uhakika halisi ni siku gani kiumbe kipya kimeumbika tumboni mwake, kwasababu anayeumba sio binadamu ni Mungu!, jukumu la binadamu ni kufanya tuu tendo la kuumba, lakini muumbani ni Mungu!. Nimeileta hadithi hii ya uumbaji ili kuelezea ndio shughuli kuu ya kwanza duniani.

Baada ya uumbaji shughuli kuu ya pili ni ujenzi wa familia, ulezi, makuzi na shughuli mbalimbali za kuendesha maisha na humu ndimo mwisho wa siku kunakuja kuibuka fani mbalimbali, wa mama wa nyumbani, wapishi, wasaidizi wa kazi, wake, vijakazi, waalimu, madaktari, madereva, wajenzi, wahubiri, matatibu, hata wanga, wachawi na washirikina, zote ni fani.

Kila fani, ina misingi yake mikuu, msingi mkuu wa fani ya ualimu ni kufundisha wengine, msingi mkuu wa fani ya udaktari ni kutibu na kuokoa maisha, msingi mkuu wa fani ya uongozi ni kuwaongoza wengine, msingi mkuu wa fani ya uandishi wa habari ni kuripoti, kueleza ukweli, ili kuueleza huo ukweli, mwandishi yeyote mzuri wa habari, ni lazima awe na uwezo wa kuhoji, mimi kwa sasa nimekuwa ni mtu mzima, lakini enzi zangu za ujana, nikiwa newsroom enzi zangu za kipindi changu cha Kiti Moto, kuna watu walikuwa wakialikwa, wanakimbia!, kilichokuwa kinawafanya wakimbie si uoga tuu wa kuogopa kuhojiwa maswali magumu.

Mahojiano yangu ya mwisho ya maswali magumu, ni yale niliyoyafanya ile siku ya tarehe 4 November, pale mahali, ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kualikwa pale, na ndio ikawa mara yangu ya mwisho,
View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=Y4_YWeCK8EmY6LVw
kilichobakia ni barua zangu tuu za kuomba mahojiano ambazo sikuwahi kujibiwa mpaka wengine wameitwa walikoitwa, na mimi nikiendelea kuziandika tuu kuomba mahojiano, na kuendelea kusubiri na kusubiri, angalau msaidizi wa sasa she is very gentle kwa kukueleza lazima uwe na subra sana maana barua za maombi ya mahojiano ni nyingi, foleni ni ndefu ila tunaendelea kusubiria, na hata tukipata fursa, siku hizi, tumeishajizeekea hatuna tena yale maswali magumu ya type ya kiti moto!.

Pamoja na jukumu kuu la mwandishi wa habari ni kuhoji na kuripoti ukweli, lakini sio lazima kila ukweli uripotiwe, kabla ya mwandishi wa habari kuripoti chochote, anapaswa afanye tathmini ya kitu kinachoitwa kwa Kiingereza Objectivity, yaani huu ukweli ninaotaka kuuripoti, ukijulikana, utaisaidia jamii?, hivyo ukikutana na tukio la ukweli kabisa, lakini ukaona ukweli huo ukijulikana, hautaisaidia jamii, wewe kama mwandishi makini, unapaswa kuuhifadhi ukweli huo na kutouripoti, ukweli ambao hautasaidia kitu jamii husika.

Mfano mzuri, mimi kama mwandishi wa habari, ninazo taarifa halisi ya asili halisi ya mtu fulani, siku unapokutana na taarifa kama hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli unashangaa kwasababu unajua kuna watu na vyombo ambavyo should know better!.

Inapotokea hao ambao they should have known better, ikitokea hawajui, then unajikuta unalazimika kukausha Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Ijumaa ya Tarehe, 12 mwezi March, mwaka 2021, mimi nikiwa ni mshitiri (subscribers) wa akaunti ya mtandao wa YouTube wa mwandishi mmoja Mtanzania anayeishi ughaibuni, alipandisha kwenye mtandao wake, taarifa ya kutokea kifo cha kiongozi fulani wa nchi fulani, lakini viongozi wa nchi hiyo, wameamua kufanya siri!.

Mwandishi huyo, alisema, yeye amepenyezewa taarifa hiyo na jamaa zake ambao ni watu wa "sehemu", na wameamua kumpenyezea yeye, kwa vile na yeye alikuwa ni mtu wa "sehemu", kabla ya kuikimbia nchi na kutokomea ughaibuni, baada ya kushikwa sikio, na watu wenzake wa "sehemu" kuwa wanaitafuta roho yake, ndipo akaamua kukimbilia ughaubuni kuinusuru roho yake ndio maana mpaka sasa bado yupo, vinginevyo angeisha kuwa mavumbi siku nyingi!.

Taarifa ya msiba huo ikasababisha sintofahamu kubwa huku nyumbani!, mara Balozi wetu wa Zimbabwe ambaye na yeye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ile Idara ya "sehemu", akatoa taarifa kukanusha!, Balozi wa Tanzania nchini Namibia (Kipilimba): Rais Magufuli yuko mzima anachapa kazi, yaani kijana wa sehemu apenyeze nyeti, kisha bosi wake akanushe!.

Mara Waziri Mkuu wa JMT akatoa taarifaa, jamaa yuko ana chapa kazi mnataka aende Kariakoo!, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Mara VP wa nchi hiyo akjatumwa Tanga kwenda kumwakilisha bosi wake kwenye tukio!.

Kwa vile nchi yetu ni nchi ya JMT yenye pande mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wenzetu kule Zanzibar, toka baada ya kuipokea taarifa hiyo Machi 12, wao walisitisha shughuli zote na ratiba zote za kiserikali za shamra shamra na kufuta ziara zote, huki sisi huku bara tukiendelea as if nothing happened!.

Na baada ya siku 5 tangu nilipopokea taarifa hii, ndipo Taifa tungatangaziwa rasmi kuhusu msiba huo mzito!. Taarifa hiyo iliishitusitusha dunia na Watanzania wote kuhusu msiba wa mkuu wa nchi, laki kwa wale ambao tulipokea taarifa ya msiba huu siku 5 kabla, sio kuwa hatukushitishwa na taarifa rasmi ya msiba, bali sasa tulisumbuliwa na shauku ya kuhoji ukweli ni upi kuhusu msiba huu, ni ile taarifa ya siku tsano zilizopita au taarifa rasmi ndio ukweli wenyewe?, Watanzania wana haki ya kuelezwa ukweli wa nini haswa kilitokea kama ukweli ukweli huo unaelezeka, ila kama ukweli huo haulezeki, then Watanzania bado tuna haki ya kuelezwa kuwa ukweli tarehe halisi ya tukio lile haielezeki ila ile Machi 17 ndio tuichukulie ndio tarehe rasmi ya kutangazwa tukio, kwasababu hata tarehe 25 Desemba, inayatangazwa ndio siku ya kuzaliwa Masiha, ni siku tuu iliyoteuliwa, lakini siku rasmi ya kuzaliwa Masiha, sio hiyo tarehe 25 Desemba, bali ndio siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake.

Familia nyingi za Kiafrika, haswa sisi watu wa Kanda ya Ziwa, tukilewa huwa tuna kelele sana, hivyo ndani ya familia nyingi, huwa tunashuhudia kuna siku baba amepata kinywaji na kikamkolea, anarudi amelewa, anapgizana kelele na Maza, na kuna sometimes Maza anatembezewa kichapo, watoto mnajua, lakini hamuwezi kuuliza, wala kutangaza, inabaki ni siri za familia, ila watoto wa kizazi cha kisasa kizazi cha kuhoji, siku zote huwa wana dukuduku, kimetokea nini hadi Maza atembelee kisago?!.

Sasa kwa tukio kubwa kama lile la tarehe 17 Machi, kama ni kweli lilitokea tarehe 12 Machi, na watu wakakaa na mtu wao siku 5 nzima ndipo waje watutangazie, dukuduku ya kuhoji, walikuwa wanafanya nae nini siku zote 5?. Bado naendelea kusisitiza kuzingatia issues za morality kwenye kuusema ukweli Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Kutokana na kutoelezwa ukweli ni nini haswa kilitokea, wazushi nao wanapenyezea hapo hapo agenda zao, eti baada ya kutokea kilichotokea ile tarehe 12, haikutangazwa kwasababu kuna kiongozi mmoja wa kidini wa imani fulani, aliwahakikishia anaweza kumrejeshea uhai wake, na akakubaliwa, hivyo hizo siku tano toka tarehe 12 Machi tukio lilipotokea, hadi tarehe 17, lilipotangazwa, juhudi za kumpambania maisha yake, zilikuwa zinaendelea, na baada ya juhudi zote kushindikana ndipo sasa tukatangaziwa rasmi!.

Sisi kizazi cha kuhoji, bado tuna dukuduku, kwa ule msemo wa sterling hauwawi, kama sterling wa filamu alikuwa amelala toka Machi 12, mpaka tulipotangaziwa ile Machi 17, who was running the show?, ni nani walimweleza Waziri Mkuu aseme Mwamba anachapa kazi?!, ni nani walimpangia VP safari ya Tanga ili kumzuga, as if nothing happened, wakati wenzetu upande wa pili wa Zanzibar wao waliahirisha kila kitu?!.

Hitimisho
Japo sio lazima kuhoji kila kitu kwa kuuliza maswali, kakini likitokea jambo lisilo la kawaida, mtu yeyote mwenye akili zake timamu, sio lazima ahoji au kuuliza, lakini ni zazima ajiulize ilikuwaje na ilitokeaje tokeaje?!. Huu ukimya wetu, wa ku observe things, to note things bila kuongea, au bila kuuliza, naomba kusitafririewa kuwa ni mazuzu!, kunapotokea vitu ambavyo Watanzania wanapaswa kuambiwa ukweli, Watanzania tuambiwe ukweli bila kujali ukweli huo ni mtamu au mchungu kiasi gani, ukimya wa Watanzania kutohoji hoji kila kitu, kusitafsiriwe kuwa Watanzania ni mazuzu, kunapotokea jambo, tuelezwe tuu ukweli, tutaelewa. Natoa wito kwa viongozi wetu, mnapoona watu hawahoji hoji sana kama enzi zile, mjue ni wameamua kutohoji hoji sana, na sio kuwa hawaoni, au hawajui, hivyo viongozi wetu msituchulie poa, mkatuona kama mazuzu!, Watanzania sio mazuzu!, kuna siku itafika, ukweli bayana utajulikana, hawa watu watawaonaje?.

Ukweli Usemwe

Paskali

Hoji sasa hivi current issue hili la Magufuli lilishapita. The page of Magufuli was/is closed. Nchi inachangamoto nyingi mno kwasasa. Plz hoji kwa niaba ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom