Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Leo Mh. Makamba kupitia account yake alikuwa akijibu suala la umeme kukatika. Lakini majibu yake yamejaa walakini.
Makamba anasema umeme zamani ulikuwa haukatiki kwa sababu watu walikuwa na hofu ya kufukuzwa hivyo walihakikisha umeme haukatiki, hali iliyopelekea kutofanya rapair.
Sasa hivi mfumo wa ugavi umechoka na ndio maana umeme unakatika Sana. Hivyo wanafanya rapair ili kuondoa huo uchakavu wa mfumo.
Bado hajasema utachukua muda gani hadi hizo repair kuisha na umeme kuacha kukatika.
Makamba ameonyesha kwamba kukatika umeme ni sawa kabisa na ni haki yetu, ndio maana anasema tulishangilia umeme ulipokuwa haukatiki huku mfumo ukiwa umechoka.
Lakini pia mheshimiwa unataka kusema huo mfumo kipindi chote cha jiwe mwendazake uliacha kuchoka ukawa unakusubiri wewe kuwa waziri ili uanze kuchoka?
Mheshimiwa wewe ukiwa kama binadamu wengine una tabia ya kusahau, Ila internet haisahau.
Mwezi uliopita September 17, ulikuwa na kikao na Tanesco na ukawapa wiki mbili umeme kuacha kukatika la sivyo utawafukuza.
Leo umesahau? Wiki mbili zimepita na sasa ni zaidi ya mwezi, bado tatizo lipo na wewe umekiri mwenyewe.
Mh. Makamba watu wanachotaka umeme uwepo muda wote ili shughuli zao ziende, hizo sababu zingine haziwahusu sana maana zipo ndani ya uwezo wenu.