January Makamba: Bwawa la Nyerere limebakiza Mita 2 za Ujazo ili kuwa na uwezo wa kuzalisha Umeme

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,108
49,811
Hatimaye mashine ya kwanza kuanza kuzalisha umeme,

Mambo tayari huko 🔥🔥🔥
Hongera Serikali, Hongera Rais na Hongera Waziri Makamba
=======

1685558385724.png

Picha: WAZIRI wa Nishati, January Makamba
Serikali imetangaza kuwa, wiki moja ijayo kina cha maji katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) litakuwa na uwezo wa kuanza kuzalisha umeme.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 31, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka 2023/24 ambayo ameliomba Bunge lipitishe jumla ya Sh3.048 trilioni.

Waziri Makamba amesema kuwa ujazo wa maji uliofikiwa katika Bwawa hilo ni mita za ujazo 163, lakini kiwango kinachotakiwa bado mita za ujazo mbili.

“Mheshimiwa Spika, ninafurahi kulitaarifu Bunge lako kuwa, wiki ijayo hata tukiamua kuanza uzalishaji wa umeme tunaweza kwani kiwango cha chini cha uzalishaji maji tumebakiza mita za ujazo mbili tu,” amesema Makamba.

Hata hivyo Waziri amesema kuwa uzalishaji wa umeme utakaoanza rasmi katika mwaka huu wa fedha, utaingizwa katika gridi ya Taifa June 2024 sambamba na umeme wa jua.

MWANANCHI
 
Kwa hiyo kesho linaanza?
🤣🤣🤣🤣

Mbunge wa Tandahimba, Katani Katani amemuomba Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kama inawezekana wabunge wachache tu wachangie mjadala huo kutoka na wizara hiyo kufanya vyema katika utendaji kazi zao, hivo bunge lipitishe bajeti yao kiasi cha Sh3.048 trilioni wakafanye kazi.

Katani ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 31, 2023 wakati alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2023/2024 bungeni jijini Dodoma. 📸 Edwin Mjwahuzi.
 
Waongo waongo tu umesahau treni tuliambiwa litaanza lini?

Back
Top Bottom