January Makamba: TANESCO sasa wamesitisha miradi ya ujenzi wa maofisi na kuelekeza fedha kukarabati miundombinu ya Ugavi

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,960
Leo Mh. Makamba kupitia account yake alikuwa akijibu suala la umeme kukatika. Lakini majibu yake yamejaa walakini.

Makamba anasema umeme zamani ulikuwa haukatiki kwa sababu watu walikuwa na hofu ya kufukuzwa hivyo walihakikisha umeme haukatiki, hali iliyopelekea kutofanya rapair.

Sasa hivi mfumo wa ugavi umechoka na ndio maana umeme unakatika Sana. Hivyo wanafanya rapair ili kuondoa huo uchakavu wa mfumo.

Bado hajasema utachukua muda gani hadi hizo repair kuisha na umeme kuacha kukatika.
Makamba ameonyesha kwamba kukatika umeme ni sawa kabisa na ni haki yetu, ndio maana anasema tulishangilia umeme ulipokuwa haukatiki huku mfumo ukiwa umechoka.

Lakini pia mheshimiwa unataka kusema huo mfumo kipindi chote cha jiwe mwendazake uliacha kuchoka ukawa unakusubiri wewe kuwa waziri ili uanze kuchoka?

Mheshimiwa wewe ukiwa kama binadamu wengine una tabia ya kusahau, Ila internet haisahau.
Mwezi uliopita September 17, ulikuwa na kikao na Tanesco na ukawapa wiki mbili umeme kuacha kukatika la sivyo utawafukuza.

Leo umesahau? Wiki mbili zimepita na sasa ni zaidi ya mwezi, bado tatizo lipo na wewe umekiri mwenyewe.

Mh. Makamba watu wanachotaka umeme uwepo muda wote ili shughuli zao ziende, hizo sababu zingine haziwahusu sana maana zipo ndani ya uwezo wenu.

Screenshot 2021-11-20 at 17.02.02.png



Screenshot_20211029-110457_1.jpg
 
Bado naona Approach ya Waziri Makamba ipo sawa sawia. Huwezi kufanya kazi kwa mashinikizo yasiyo na msingi. Alichokisema ilikuwa ndio anaingia Wizara hiyo sasa kapata data zote za mfumo wote wa ugawaji wa umeme ambao unahitaji marekebisho na kufanya hivyo lazima wakate umeme.

Maintenance ndio chanzo kikubwa kwa mifumu mingi Africa kufa, watu wengi hatuna mazoea ya kutenga pesa kwa ajili ya maintenance. Anakuja waziri anasema usikate umeme akiogopa kutumbuliwa kumbe mfumo wote unaendelea kuchakaa na kuongeza upotevu wa umeme.

Tusiwe wanazi tumwache afanyekazi yake. It too early to compare. Tuliona nguvu njingi zikitumika bila ya mafanikio ya kudumu na oungo mwingi na majigambo. Nchi hainendi kwa mihemko bali inaenda kwa kuwa na Strategic plan na kuzitekeleza.
 
Kwa hayo majibu simply anakimbia uwajibikaji kwa kasoro zinazotokea kwenye wizara yake.

Suala la umeme kukatika ni mwiba kwa awamu zote, hata wakati wa Magufuli umeme ulikuwa unakatika na tukaambiwa tatizo ni hilo hilo la uchakavu wa njia za kuzalisha na kusambaza umeme.

Awamu nyingine tuliambiwa kina cha maji kimepungua kwenye mabwawa ya uzalishaji umeme ndio maana baadae Magufuli akaamua kujenga Stiglers Gorge.

Vyema Makamba azijue changamoto kwenye wizara yake hazijaanza wakati huu na azitafutie majibu, asitoe lawama kwa awamu iliyopita kisa ilikuwa inatisha watu na hivi ni sawa na anamaanisha sasa kwasababu hawatishwi ndio wawe wazembe.
 
Huyu wizara anayoiweza, ni wizara ambazo haina pressure..

Wizara inayomfaa ni wazara ya mazingira.. Ndio wizara pekee anayoiweza..

Hizi zingine tunamtaka tu ubaya
Leo Mh. Makamba kupitia account yake alikuwa akijibu suala la umeme kukatika. Lakini majibu yake yamejaa walakini.

Makamba anasema umeme zamani ulikuwa haukatiki kwa sababu watu walikuwa na hofu ya kufukuzwa hivyo walihakikisha umeme haukatiki, hali iliyopelekea kutofanya rapair...
 
Walakini uko wapi, wakati unapewa jibu la kisomi...mlikuwa mnaongopewa huku mfuko mzima wa umeme unaharibika... Huwa nafikiria Hayati alikuwa na dhumuni gani na hii Nchi.
Yaaano wakati wa Kikwete miaka 10 ulikiwa unakatika kwa sababu walikiwa wanarepair, sasa bado unasema maoaka mitano umeme haukukatika kwa kuwa watu walikuwa wanaogopa kutumbulia.. sasa walichorepair miaka 10 yakikwete ilikuwa ninini?
 
Duh engineer...
Machine zina maintenance schedule, usipofanya repair hata rais awe kiduku zitazingua tu..
Machine hazijafanyiwa maintenance ndani ya miaka mitano? Nazo ziliogopa zikapiga kazi?
Basi jiwe alikuwa bora, kama mashine na mabwawa yote yalimuogopa jiwe umeme ukawa wakutosha. Sasa kama ni hivyo kwanini waliwaondoa madirectots wote wa makao makuu ya umeme?
 
Bada naona Approach ya Waziri Makamba ipo sawa sawia. Huwezi kufanya kazi kwa mashinikizo yasiyo na msingi. Alichokisema ilikuwa ndio anaingia Wizara hiyo sasa kapata data zote za mfumo wote wa ugawaji wa umeme ambao unahitaji marekebisho na kufanya hivyo lazima wakate umeme. Maintenance ndio chanzo kikubwa kwa mifumu mingi Africa kufa, watu wengi hatuna mazoea ya kutenga pesa kwa ajili ya maintenance. Anakuja waziri anasema usikate umeme akiogopa kutumbuliwa kumbe mfumo wote unaendelea kuchakaa na kuongeza upotevu wa umeme. Tusiwe wanazi tumwache afanyekazi yake. It too early to compare. Tuliona nguvu njingi zikitumika bila ya mafanikio ya kudumu na oungo mwingi na majigambo. Nchi hainendi kwa mihemko bali inaenda kwa kuwa na Strategic plan na kuzitekeleza.
Unaamanisha kipindi makamba anatoa hiyo kauli ya wiki mbili alikurupuka? Maana ilibidi awasikilize kwanza Tanesco ndio atoe kauli.
Pili, hiyo mifumo ilikuwa inamsubiri makamba awe waziri ili.ianze kuchoka?
Tatu, unakubali kabisa kukatika umeme ni haki yatu kwa kuwa Kuna repair huwa zinafanyika?
 
Kwa hayo majibu simply anakimbia uwajibikaji kwa kasoro zinazotokea kwenye wizara yake.

Suala la umeme kukatika ni mwiba kwa awamu zote, hata wakati wa Magufuli umeme ulikuwa unakatika na tukaambiwa tatizo ni hilo hilo la uchakavu wa njia za kuzalisha na kusambaza umeme.

Awamu nyingine tuliambiwa kina cha maji kimepungua kwenye mabwawa ya uzalishaji umeme ndio maana baadae Magufuli akaamua kujenga Stiglers Gorge.

Vyema Makamba azijue changamoto kwenye wizara yake hazijaanza wakati huu na azitafutie majibu, asitoe lawama kwa awamu iliyopita kisa ilikuwa inatisha watu. hivi ni sawa na anamaanisha sasa kwasababu hawatishwi ndio wawe wazembe.
Yes ni kukimbia uwajibikaji.

Makamba ni Kama anatupia lawama waziri aliyepita kwa kutokatika umeme kisa walikuwa hawafanyi repair.

Ila kasahau hata wakati wa JK umeme ulikuwa ukikatika sana hadi kukaanza mgao wa umeme.

Lakini yote kwa yote Ina maana hiyo mifumo ilikuwa inamsubiri yeye ili iwe mibovu?
 
Unaamanisha kipindi makamba anatoa hiyo kauli ya wiki mbili alikurupuka? Maana ilibidi awasikilize kwanza Tanesco ndio atoe kauli.
Pili, hiyo mifumo ilikuwa inamsubiri makamba awe waziri ili.ianze kuchoka?
Tatu, unakubali kabisa kukatika umeme ni haki yatu kwa kuwa Kuna repair huwa zinafanyika?
Yes nakubaliana na wewe kwa kauli alizozitoa mwanzo was really premature alistahili kujipa muda wa kutosha kulielewa shirika lilipifikia. ila kuchoka kwa mifumo sio la leo ni la siku nyingi na halijawahi kufanyiwa kazi kwa uhakika sasa tusubiri nini ili lifanyike? Huu ndio muda wake vumilia ili mfumu mzima usidondoke ua kuleta madhara zaidi kwa wananchi. It is the right time to do the repair. Sio kuyanyanganya mashirika yote fedha zake na kukusanya kwenye chungu hazika na kuanza kuzigawa kwa kijiko cha chai. Wakileta actual cost for repair katibu mkuu hazina anakata bila hata kuwasilina na shirika lenyewe. Huu mfumo pia ni chanzo cha matatizo haya. Tuwaache wairekebishe nchi kwanza, it too early to say all that.
 
Walakini uko wapi, wakati unapewa jibu la kisomi...mlikuwa mnaongopewa huku mfuko mzima wa umeme unaharibika... Huwa nafikiria Hayati alikuwa na dhumuni gani na hii Nchi.
Majibu hayana mashiko, Sawa tuseme kipindi Cha mwendazake watu walikua wanatishiwa na kuogopa kufanya repair na kisababisha uchakavu ndio sababu ya umeme kukatika,

Vipi kuhusu enzi za jakaya ambapo watu walikua hawatishiwi, repair zilikua zinafanyika na umeme ulikua unakatika Hadi siku tatu mfululizo? Enzi ambazo ukipita kariakoo kichwa kinauma kwa ngurumo za jenereta?

Tusiwafananishe watz na ming'ombe, kitendo Cha wao kutokua kwenye mifumo haimaanishi kwamba hawajui kitu
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom