Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,218
View: https://youtu.be/NlMzNWph_tE?si=ZEn2izCLvieZG_Th
Vijana sasa hivi hawajuia yaliyo tokea miaka 60 iliyopita.
Namshukuru Mungu, mimi nilishuhudia hata kama ni kiduchu na nilikuwa mdogo sana.
Tukiishi Temeke miaka hiyo, na kambi kuu za jeshi Mgulani zilikuwa karibu sana.
Nilikuwa na miaka saba wakati huo na tulikuwa tunakaa nyumba ya mwarabu mmoja Temeke, Baba yangu ni mjeshi.
Kwa mara ya kwanza mwaka huo ndio nikasikia live sauti ya kutisha ya mlio wa sub machine gun ikitoa mlio kwa mbali.
Watu wote walijificha majumbani kwao na hakuna mtu alitoka nje.
Viumbe wa kuonekana vikirandaranda mtaani ni kuku na mbwa.
Mwenye nyumba wetu, mwarabu, alishukuru sana kuwa mpangaji wake alikuwa mwanajeshi, baba yetu, na literally alimpigia magoti kwa ajili ya ulinzi.
Maasi ya January 1964 yalimtikisa vibaya sana Mwalimu Nyerere ambaye kwa aibu kubwa ilibidi awaombe jeshi la mkoloni, ili limsaidie kuzima maasi.
Maasi yenyewe kimsingi yalikuwa kuwapa madaraka waafrika ndani ya jeshi, Africanisation.
Wimbi hili la maasi lilienea Uganda, Kenya na liliishia Zanzibar mwezi April ,1964.
Wana JF, tulikuwepo!