Kabla ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964, Zanzibar pamoja na korido lote (km 10) la mwambao wa Pwani ya Afrika Mashariki vikijumuisha visiwa vya Lamu na Mafia vilitawaliwa na Ukoo wa Sultan Sayyid wa Oman.
Sultan aliitawala Zanzibar na mwambao wote kuanzia Tanga hadi Lindi, korido lote toka Tanga hadi Tabora na Kigoma ili kusaidia biashara zake za utumwa na kusafirisha pembe za ndovu kupeleka nchi za mashariki ya mbali kupitia Kongo.
Leo waarabu wale wale wa Oman na Dubai wanataka kumiliki bandari zote zilizo kwenye maeneo yale yale, wameongeza na bandari zote za nchi kavu na zilizo kwenye maziwa makuu, kama hiyo haitoshi wanataka kujimilikisha njia kuu zote kutoka bandari kuu za Dar es salaam na Tanga hadi zilipo bandari za nchi kavu na maziwa makuu yaani bandari za Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.
Kama huu sio ukoloni mamboleo ni nini. WaTanzania tushituke tuendelee kupiga kelele hadi mkoloni na vibaraka wake wajue watanzania wa leo sio wa miaka ile ya 1800.