Serikali: Hakuna wanachodai Wastaafu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wameshalipwa na zoezi limeshafungwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 9, leo Septemba 8, 2023.

View: https://www.youtube.com/live/LESXSKjjWGg?si=4iBgpLPzLXEouZLk

View: https://www.youtube.com/watch?v=-LGuLfNhFWE

Mbunge Hawa Subira Mwaifunga ameuliza swali Bungeni; Je, Serikali ina mpango gani kulipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki?

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Silaoneka Kigahe anajibu kwa niaba ya Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, anasema:

“Madai yao yalilipwa kwa kuzingatia Sheria za Pensheni za Jumuiya hiyo, maridhiano ya Mwaka 1984, Sheria namba 2 ya 1987 na Hukumu ya Mahakama Kuu ya Mwaka 2005.

“Kwa kuzingatia miongozo hiyo, Serikali iliandaa utaratibu wa malipo na mirathi kwa waliofariki wapatao 31,831, zoezi hilo lilifanyika kwa miaka nane kuanzia Julai 2006 hadi Novemba 2013 lilipofungwa rasmi, kwa sasa Serikali inaendelea kulipa pensheni za kila mwezi kwa wastaafu.

“Kwa mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia Septemba 2023, Serikali imelipa Tsh. Bilioni 1.07 kwa wastaafu 1,746 na itaendelea kulipa Pensheni kwa wastaafu wanaostahili.”

Pia soma: Idara ya usalama wa Taifa na TAKUKURU wasaidieni wazee wastaafu wa East Africa community wanateseka na wanapigwa pesa
 
Imeisha hiyo, kwahiyo kumbe wazee wanapigwa tu mtaani kuwa bado wanadai
 
Back
Top Bottom