Polisi wa Nchi za Ukanda wa Mashariki mwa Afrika waungana na Rwanda kumbukumbu mauaji ya kimbari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,416
5,778
Shirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki Wameungana na Polisi wenzao kutoka Nchini Rwanda kuuwakumbuka Wananchi waliopoteza maisha katika mauaji ya kimbari Nchini Rwanda.

Akiongea leo Aprili 14,2024 katika Shule ya Polisi Tanzania Mkoani Kilimanjaro Mkurungenzi Mkuu wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Ukanda wa Mashariki mwa Afrika Apollo Afrika amesema wamekuwa wamekuwa wakifanya maadhimisho ya kumbukumbu wananchi waliopoteza maisha katika mauaji ya kimbali yaliyotokea miaka 30 iliyopita nchini Rwanda.

Mkurungenzi Huyo mbali na kubainisha hilo amesema wanatumia kumbukumbu hiyo kama funzo Kwa wananchi wengine kutojiingiza katika machafuko ambapo alibainisha kuwa kipindi cha maauji hayo nchini Rwanda yalikuwa yakitisha ambayo alisema yalichafua taswira ya Nchi hiyo.

Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime pamoja na kushiriki kumbukumbu hiyo amewataka waandishi wa habari kuzingatia Maadili katika kuwahabarisha wanaanchi ili kuepusha taharuki na Migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama katika Maeneo ya ukanda huo.

Nao baadhi askari walioshiriki wa kumbukumbu hiyo iliyofanyika shule ya Polisi Tanzania TPS Moshi Kilimanjaro wamebainisha kuwa wametumia siku hiyo kuwa kumbuka na kuwaombea wananchi waliofariki katika mauaji ya kimbali Nchini Rwanda.
 
Back
Top Bottom