Janeth Rithe ajitosa Uenyekiti Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565

Janeth Rithe amechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa ngome ya wanawake ya chama cha ACT- Wazalendo, huku akianika vipaumbele vyake 10 atakavyovitekeleza endapo atafanikiwa kuchaguliwa Machi 2, 2024.

Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kuhakikisha ngome ya wanawake inakuwa muundo nchi nzima kwa mujibu wa mwongozo, kuweka pragramu za kuhakikisha wanawake wengi wanajiunga na chama hicho na kuwasaidia wanawake kuwa wagombea kwenye nafasi za udiwani na ubunge kwenye chaguzi zijazo.

Rithe maarufu kama ‘jike la simba' atachuana na Severina Mwijage ambaye anatajwa kuwa na uzoefu katika siasa na pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho na alishawahi kuwa mbunge wa viti maalumu.

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 19, 2024 baada ya kuchukua fomu hiyo, Rithe amesema amedhamiria kuibadilisha na kuimarisha ngome ya wanawake, ili kuwa chachu ya kuleta ushindi ndani ya chama hicho.
 
Vyeo vyote vya juu ni kwa Muslim brotherhood,nyie wengine msubili kwanza.Kama huamini angalia ngazi za juu ni baraza la idi.
 
Back
Top Bottom